mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Tuesday, August 23, 2016

Lowassa Apigilia Msumari Oparesheni UKUTA, Asema Haiwezekani Mtu Mmoja Azuie Kila Kitu

Leo nimezunguka katika majimbo ya Mbeya Vijijini ,Vwawa na Tunduma nikiwaeleza kuhusu Operation UKUTA,

UKUTA si fujo , UKUTA si machafuko na hatuna haja ya kufanya fujo , tunapiga kelele dhidi ya uvunjwaji wa haki ya kidemokrasia na katiba ya nchi unaofanywa na utawala huu wa awamu ya tano .

CHADEMA ni nani wakapambane na polisi ,polisi ambao ni watoto wetu ,ndugu zetu na hata wake na waume zetu ila tuwahakikishie hatutorudi nyuma pale katiba na haki ya kidemokrasia ikichezewa au kuwa chini ya mtu fulani .

Najua polisi watapiga watu ,wataumiza watu na hata kuua ila niwahakikishie wao na walio na mamlaka wataishia katika mahakama ya Kimataifa .

Siasa ni mazungumzo ,lazima tuzungumze milango yetu iko wazi kufanya mazungumzo ila kwa kuwa hawahitaji na sisi hatutorudi nyuma September Mosi ,tumejiandaa vya kutosha na sasa tuko ngazi ya kaya na wajumbe wetu wanakamilisha kazi katika kaya ili tarehe mosi sauti ya kutosha ipazwe kwa maandamano na mikutano kama tulivyokubaliana katika kata zetu na majimbo nchi nzima .

Haiwezekani hata kidogo mtu mmoja azuie kila kitu ,nchi hii ni mali yetu sote na inaongozwa na Katiba na sheria.

Kamati kuu ilipoamua katika suala la UKUTA haikukurupuka , kamati kuu yetu inaundwa na mchanganyiko wa wasomi wa kada mbalimbali ,wazee wenye busara na vijana machachari kamwe hawawezi kukukurupuka na UKUTA ni haki ya watanzania wote.

Pili naomba niwape siri ya ushindi 2020 ndugu zangu na wanachama wenzangu , tutashinda uchaguzi Mkuu 2020 kama tutafanya yafuatayo na kuyasimamia
Kwanza; Umoja ndani ya Chama na wanachama ,tuheshimiane ,tusameheane na tuimarishe chama chetu
"chama ndani ya Chama , chama nje ya chama na chama ndani ya Umma "- LOWASSA

Makundi yayumbisha CCM


KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Arusha, Medest Meikoki amesema kuyumba kwa chama hicho katika Jiji la Arusha na kusababisha upinzani kuongoza kutokana na makundi yaliyopo ndani ya chama hicho.

Akizungumza mjini hapa jana, Meikoki alisema aliamua kustaafu siasa baada ya kusulubiwa na makundi hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa na nguvu katika miaka ya 2000.

Alisema katika jiji hili kulikuwa na makundi mawili ya G7 na G13 ambayo yalikuwa na nguvu katika miaka hiyo.

Kada huyo, alisema bado baadhi ya wana CCM waliojeruhiwa na makundi hayo wana hasira dhidi ya chama chao na kuamua kukaa pembeni na kuacha wenye pesa wafanye watakavyo, lakini waliapa chama hakitachukua jimbo hilo kamwe.

Alisema hatua za ziada zinatakiwa kuchukuliwa na viongozi wa juu wa CCM wa kuwarudisha kundini waliojeruhiwa na makundi hayo bila ya sababu za msingi vinginevyo, upinzani utaendelea kuongoza.

Kada huyo aliendelea kusema kuwa makundi ya kisiasa ya G7 na G13 ndiyo yamekivuruga chama na kuifikisha siasa ya Arusha kuwa taabani kwani waliokuwa wakichaguliwa walikuwa ni viongozi wasiokuwa na sifa za kuongoza chama hicho.

Alisema, kundi la G7 lilikuwa kundi lenye uwezo mkubwa wa kifedha ambapo wafanyabiashara wakubwa wa Arusha, walikuwa katika kundi hilo na walikuwa wakiamua wanavyotaka na ukipingana nao unang’olewa.

Kada huyo alisema, kundi la G13 lilikuwa kundi la wanasiasa wenye kujua siasa za Arusha na nchi kwa ujumla na walikuwa wapambanaji lakini walikuwa ni watu wa kawaida tu wasiokuwa na fedha, lakini wenye mikakati ya kutaka chama kishike hatamu.

Alisema yeye aliwahi kushughulikiwa mwaka 2000 ndani ya chama na kundi la G7 kwani katika kura za maoni za ndani ya chama, alishinda lakini kundi hilo halikuridhika na likaamua kumtoa mwanaCCM na kumsimamisha upande wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) ili kupambana naye kwenye udiwani wa kata ya Darajambili.

Kada huyo alisema kundi hilo lilifanikiwa, kwani TLP ilishinda katika kiti cha udiwani katika kata hiyo na yeye kuanguka vibaya ingawa awali alishinda kwa kishindo katika kura za maoni ndani ya chama

Alisema baada ya kushughulikiwa mwaka 2000 aliamua kujikita katika kushauri badala ya kugombea na alipoamua kuingia tena kwenye siasa mwaka 2005, alishughulikiwa tena na akaamua kustaafu na kubakia kuwa mshauri hadi sasa.