mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Wednesday, June 1, 2016

Rais Magufuli Awatangazia Vita Wafanyabiashara ‘Wajanja’


Rais John Magufuli amesema Serikali yake itaendelea kupambana na wanaoingiza bidhaa zilizochini ya kiwango na wale wanaokwepa kodi.

Amesema kwa kufanya hivyo, wanachangia kuviua viwanda vya ndani ya nchi.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana kwenye hafla ya utaoji wa Tuzo ya Rais ya wazalishaji bora wa viwandani kwa mwaka 2015 zilizofanyika jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zimeandaliwa na Shirika la Wenye Viwanda Nchini (CTI).

Rais amesema pia hatawavumilia watendaji wote watakao wakwamisha wafanyabiashara wenye nia ya kuanzisha viwanda nchini kwa sababu zisizo za msingi na kuwaahidi kuwasaidia waweze kufanikisha ndoto zao.

Pia, amesema ni vizuri wafanyabiashara wote nchini wakatumia fursa zipatikanazo katika awamu hii ya uongozi wake, ili wasije kuzijutia baadaye.

“Nasema kwa dhati kutoka moyoni, you have my support, mkishindwa katika kipindi cha awamu ya tano basi hamtaweza tena,” alisema.

Rais Magufuli alisema nchi inapokuwa na viwanda vingi vitatoa ajira kwa Watanzania, vitaongeza mapato kwa Serikali na kuingiza fedha za kigeni kwa kuuza bidhaa nje ya nchi.

“Nina dhamira ya dhati ndani ya moyo wangu kuwasaidia wenye nia ya kuanzisha ya viwanda, siwachukii matajiri nawapenda matajiri,” alisema.

Rais Magufuli aliwapa moyo wafanyabiashara wenye viwanda kuanzisha vingine ili Serikali iweze kunufaika zaidi.

Alisema Tanzania ina rasilimali nyingi kama maliasili na madini na akawahakikishia wawekezaji kuwa lipo soko kubwa la bidhaa watakazozitengeza lenye watu milioni 160 katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Magufuli alisema sekta ya viwanda ni muhimili mkubwa wa uchumi katika nchi huku akitolea mfano wa nchi za China, India, Korea Kusini, Malaysia, Thailand na Vietnam  ambazo zimekuwa kwa kasi kwa sababu ya uwepo wa viwanda.

Alisema viwanda vinapoanzishwa nchini badala ya kuuza mali ghafi kwa bei ndogo zitatengenezwa bidhaa ambazo zitauzwa nje ya nchi na kutoa ajira kwa Watanzania.

“Badala ya kuuza ngozi tutengeneze viatu hapa hapa nchini au badala ya kuuza ng’ombe Comoro tumepeke nyama iliyosindikwa,” alisema.

Alisema nchi kama ya Sudan Kusini ina mahitaji makubwa ya unga wa mahindi.

“Lakini wanaofaidika na soko hilo ni Wakenya ambao wanakuja nchini wananunua mahindi, wanasaga na kuyapeleka huko,hivi wafanyabiashara tunashindwa hata kuanzisha viwanda vya kusaga mahindi,” alisema

Alisema Mkoa wa Arusha una ng’ombe wa  maziwa lakini yananunuliwa na Wakenya ambao wanayasindika kwenye viwanda vyao na kuja kuyauza hapa nchini.

Hata hivyo, alisema Serikali inaangalia uwezekano wa kuanzisha benki ya maendeleo ya viwanda kwa lengo la kutoa mikopo yenye masharti nafuu na riba ndogo.

Kuhusu kuondoa kwa changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo ya viwanda nchini, Magufuli alisema Serikali imeshatenga Sh1trilioni katika mwaka wa fedha ujao kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.

Pia, Serikali imeunda kamati maalumu itakayoangalia mazingira ya ufanyaji biashara nchini ikiwamo kodi na tozo mbalimbali.

“Nchi yetu inakuwa na kodi za ajabu ajabu, mfano zao la kahawa kulikua na zaidi ya kodi 30. Haya ndiyo tunayoyaangalia,” alisema.

 Kuhusu upatikanaji wa mitaji na riba kubwa zinazotozwa na benki, alisema katika kukabiliana na matatizo hayo Serikali inajiandaa kuanzisha benki ya viwanda itakayowasaidia wenye wawekezaji.

Kwa upande wake  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema Serikali imejikita katika kuhamasisha ujenzi wa viwanda vingi zaidi nchini.

“Tumeandaa mkakati wa pamba hadi inakuwa nguo, alizeti hadi mafuta na tunaendelea kufufua viwanda vilivyokufa,” alisema.

Akizungumzia changamoto zinazowakabiri wenye viwanda nchini, mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), Samuel Nyantahe alisema uchakavu wa miundombinu ya umeme na miundombinu ya barabara imekuwa ikiongeza gharama za uzalishaji.

Pia, alilalamikia uwapo wa utitiri wa kodi, mamlaka za usimamiaji biashara na uwapo wa bidhaa bandia zinazotishia bidhaa za ndani

Taarifa toka Ikulu kuhusu uteuzi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO


TAARIFA KWA UMMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Dkt. Alex L. Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb.), amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO kuanzia tarehe 31/5/2016 hadi tarehe 30/5/2019;
1.   Dkt. Samwel Nyantahe
2.   Dkt. Lugano Wilson
3.   Bw. David Elias Alal
4.   Mhandisi Stephen Peter Mabada
5.   Mhandisi Leonard R. Masanja

Aidha, Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb) amekamilisha uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kuanzia tarehe 30/5/2016 hadi 29/5/2019 wajumbe  hao ni :

    Bw. Abdalah H. Musa
    Dkt. Coretha Komba
    Bw. Felix M. Maagi
    Dkt. Lightness Mnzava
    Bw. John B. Seka

Uzinduzi wa Bodi hizo utafanyika Makao Makuu ya Mashiriki hayo Siku ya Alhamisi tarehe 2 Juni, 2016, saa 4:00 asubuhi kwa Bodi ya STAMICO na saa 8:00 mchana kwa Bodi ya TANESCO.

Imetolewa na;
KATIBU MKUU
31 MEI, 2016

Babu Tale Alimtelekeza Chidi Benz Sobber House - Mkuu wa Kituo


Akizungumza na E news ya East Africa Tv mkuu wa Bagamoyo sobber house amesema chanzo cha Chidi Benz kuondoka kwenye kituo chao ni kutelekezwa na waliompeleka.

Anasema tangia Chidi apelekwe pale hakukuwa na huduma zozote zinazotumwa kama walivyokubaliana na kila walipokuwa wanamtafuta Babu Tale hakuwa tayari kupokea simu wala kutoa ushirikiano.

Anasema pia kukosekana kwa vitu muhimu ndio vilifanya Chidi aondoke na wala hakutoroka.

Japo Sijajua ni vitu gani walikubaliana awe anapeleka.


My take, kama ni kweli hii ishu basi Tale amekosea sana hakufanya uungwana. Ni kama kamtumia Chidi kupata kick

Tuesday, May 31, 2016

Amboni Tanga: Watu 8 Wauawa kwa Kufichua vitendo vya Kihalifu



Watu kadhaa wa kijiji cha Mikocheni karibu na mapango ya Amboni mkoani Tanga wameuawa usiku wa kuamkia leo.

Inasemekana watu waliouawa wanadaiwa kufichua vitendo vya uhalifu kijijini hapo na kwamba miili ya watu hao waliouawa imepelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoani humo.

Chanzo : Radio One.

Mya Take : Ulinzi shirikishi unaweka rehani maisha ya raia wema.

Majambazi Yauwa na Wananchi Baada ya Kumpora Mfanyabiashara Sh Laki Tano


Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa na mwingine mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kujihusisha na ujambazi jijini Dar es Salaam.Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema tukio hilo lilitokea Mei 28 mwaka huu baada ya polisi kupata taarifa kuwa maeneo ya Mburahati kuna majambazi watatu, ambao walikuwa wanafukuzwa na kundi la bodaboda huku wakifyatua risasi.Sirro alisema katika ufuatiliaji askari walifika katika eneo hilo na kukuta jambazi mmoja akishambuliwa na wananchi baada ya silaha aliyokuwa akiitumia kuishiwa risasi.
Jambazi huyo alikutwa na silaha moja, bastola LLA yenye namba 649440. Alisema majambazi wengine wawili, walikimbia wakiwa na bodaboda yenye namba za usajili MC 444 BFY.
Polisi waliwakimbiza wakishirikiana na madereva bodaboda hadi kufika katika eneo la Kisukuru, ambako majambazi hao walianguka na kuangusha bastola yao aina ya Chinese Star, ndipo wananchi walianza kuwashambulia kwa mawe na fimbo.
Aliongeza kuwa majambazi hao, walishambuliwa baada ya muda mfupi walifariki dunia huku mwingine alifanikiwa kukimbia na begi dogo jeusi lililokuwa na fedha.Sirro alisema awali majambazi hao, walikuwa watatu wakiwa kwenye pikipiki maeneo ya Buguruni, ambapo walifanya tukio la uporaji wa Sh 500,000 mali ya Mushi Bakari, aliyekuwa na gari namba T 786 CZI Toyota IST ambaye walimjeruhi mkono wa kulia.

Diamond Platnumz Aonyesha Hadharani Bastola Yake


The CEO of Wasafi Records, Diamond Platnumz, has now joined the list of celebrities who are believed to be walking around with guns.
Well this comes days after he shared a photo on his gram posing with a gun in what looks like a photo studio.
This has left many wondering whether he is a licensed gun holders or he was just posing with it for fun and giggles.

Kilio cha Maisha Magumu: Je, Tulikuwa Tunategemea Vipato Haramu?


Kuna kilio cha maisha magumu kila kona. Utasikia wakina mama,wafanyakazi, vijana hata wazee wanadai kipindi hiki cha awamu ya tano pesa imekuwa ngumu sana!.

Ninajiuliza:
1:Serikali inatueleza Inazuia ufisadi, kubana matumizi yasio ya lazima, matokeo yake wananchi wanalia eti maisha yamekuwa magumu maana yake nini?

2:Makusanyo ya Kodi ya kuwahudumia wananchi yameongezeka sana lkn kilio kila kona, tatizo nini?

3:Je Maisha bora mtaani kipindi kilichopita yalikuwa matokeo ya wizi,ufisadi,matumizi mabaya ya pesa za umma na ukwepaji kodi?

4: Nasikia hotel zinakoswa wateja na taasisi nyingi zinazorota kutokana na kubana matumizi kwa serikali. Najiuliza hivi hawa jamaa walianzisha hizo taasisi/kumbi/hotel walikiwa na market strategy ya kutegemea wateja wawe serikali tu au?

5: je, unadhani nini kinakosekana ili kikiwepo Mafisadi waendelee kutumbuliwa,wakwepa kodi walipe, Gharama za maisha zishuke, Serikali iwe na pesa za kutosha, n.k na maisha ya wananchi yawe saaafi kwa matajiri na maskini kihalali? nini kinakosekana.

Najaribu kuwaza....