mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Thursday, July 21, 2016

Katiba Mkuu Chadema Dkt Vicent Mashinji Awafunda Bavicha, Awapatia Mbinu za Kushinda 2020


Katibu Mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dkt Vicent Mashinji amewataka vijana wa Bavicha kutokuwa wazembe wakufikiria bali kujipanga kwa ajili ya kushika dola mwaka wa uchaguzi mkuu 2020 huku akiwapatia kanuni za kushinda uchaguzi huo.

Akizungumza na vijana hao jana jijini Dar es salaam Mashinji aliwaambia vijana hao chama chao kimejipanga kushika dola hivyo wao kama vijana wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya kufanya uchaguzi na kuwatambua wanachama hai, pia kuhakikisha kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa vijana wanashiriki nafasi mbali mbali na kushinda

”Nataka niwape majukumu matatu ambayo mkiyafanya hayo 2020 tutashinda nakutangazwa, moja hakikisheni tunaingiza wanachama wapya na kuwahakiki walio hai, nendeni 2019 kwenye serikali za mitaa vijana mgombee na tupate viongozi ngazi ya chini viijana wasomi, na tatu kwa mwaka huu kila kijana ajue nafasi zitakozogombewa katika eneo lake hiyo itatusaidia kushinda nafasi nyingi za madiwani  kwa Tanzania bara na visiwani  na haya ndiyo majukumu makubwa ninayowapatia”   Alisema Mashinji.

Pamoja na hayo aliwataka vijana hao kuendelea kupigania haki za wanyonge na kushinda vita ya demokrasia bila kuvunja sheria huku akiwaasa kuwa askari mzuri na shujaa ni yule anayepambana bila risasi.

”Askari mzuri ni yule ashindaye vita bila kutumia risasi zake, mkawe mabalozi wa kuwatetea wanyonge na haki zao, msiwe waoga kudai katiba ya wananchi, pia kuna watu Geita, Shinyanga na Simiyu tunataarifa wanapigwa kisa itikadi ya upinzani wa vyama hivyo kama vijana mnatakiwa mpaze sauti kwa ajili yao”. aliwaambia Mashinji.

Hata hivyo Mashinji aliwaasa vijana hao kuwa wapole na kusubiri maamuzi ya viongozi wa chama kwani yanabusara. Aidha aliwapongeza vijana hao kwa kuwa na umoja wa kupigania haki na misingi ya demokrasia.

Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Patrobas Katambi alimweleza Katibu huyo wa chama kuwa wao wapo tayari kwa pambano japo wanasikiliza na kutii kauli ya chama hivyo wao  watatoa msimamo wao.

”Sisi vijana tupo tayari miili yetu ilale makaburini na tukumbukwe kama mashujaa waliokufa wakipigania haki, tumesikiliza maagizo ya viongozi wetu lakini pia sisi leo tutatoa msimamo wetu”.- Katambi

Monday, July 18, 2016

Askofu Gwajima Aibuka, Azungumzia Sakata lake Kanisani, Msaidizi wake Akanusha Kanisa Hilo Kufungiwa


KIONGOZI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, amefunguka kwa kuelezea safari yake aliyoifanya nje ya nchi hivi karibuni, baada ya taarifa mbalimbali kudai kuwa alilikimbia Jeshi la Polisi.

Akiongoza ibada kanisani kwake, Ubungo, jijini Dar es Salaam jana, Askofu Gwajima alisema aliondoka nchini kwenda Japan Juni 15, mwaka huu, kwa ndege ya Emirates.

Akitoa mahubiri katika ibada jana, Gwajima alisema alifika mjini Osaka Juni 16 na kuanza mkutano wa kuhubiri injili na siku zilizofuata alikwenda katika miji mbalimbali.

Askofu Gwajima ambaye aliingia kanisani hapo saa 5:00 asubuhi na kuanza kuhubiri dakika 15 baadaye, asubuhi alitumia muda wa saa tatu hadi saa 8:20 kumaliza mahubiri yake.

Baada ya kuanza kuhubiri, alielezea safari hiyo kwa kutaja miji aliyekwenda ikiwamo Nagoya alikohubiri kwa siku mbili, Karuizawa, Ibaraki, Hiloshima na Yanakochi.

“Safari yangu ilikuwa ya mafanikio sana. Tulisafiri salama na kuzunguka miji mbalimbali na tulirudi Jumatatu ya wiki iliyopita,” alisema Askofu Gwajima.

Kadhalika, katika mahubiri hayo, Gwajima aliwakumbusha waumini wa kanisa hilo kuhusu kuhama kwa kanisa hilo, kwa kuwatajia siku ya mwisho ya kumalizia michango kwa ajili ya ujenzi wa kanisa jipya kuwa ni Julai 30, bila ya kutaja sehemu ambayo kanisa hilo litahamia.

Hata hivyo, Askofu Gwajima wakati wote wa mahubiri, hakuzungumzia suala la kuhojiwa kwake na Jeshi la Polisi.

Wakati huo huo, mwandishi alizungumza na Msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonia Bihagaze, kuhusu tetesi za kufungiwa kwa kanisa hilo na kusema taarifa hizo si za kweli bali ni maneno ya mitaani.

“Hayo maneno si ya kweli. Si umeona ibada imeendelea kama kawaida na Askofu amehubiri? Maneno ya mtaani usiyalete kanisani,” alisema Bihagaze.

Julai 12, mwaka huu, Kikosi cha Polisi cha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) kilimkamata Askofu Gwajima wakati akitokea Japan kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya.

Baada ya kukamatwa, alipelekwa moja kwa moja Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya kuhojiwa, akidaiwa alitoa maneno ya uchochezi mwezi uliopita.

Jeshi la Polisi lilikuwa likimtafuta Askofu Gwajima baada ya kusambazwa mkanda kwenye mitandao ya kijamii unaodhaniwa una sauti yake.

Katika mkanda huo, Gwajima anapendekeza Rais mstaafu Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake, ambayo kwa sasa Rais Magufuli anayashughulika kwa staili ya utumbuaji majipu.

Pia Gwajima alisikika akimshauri Rais John Magufuli, kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) iwapo watakataa kumkabidhi uenyekiti na kwamba apeleke muswada bungeni, kuondoa kinga ili rais ashtakiwe kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani.

Tangu kusambaa kwa mkanda huo, Jeshi la Polisi lilikuwa likipiga kambi katika moja ya nyumba za Askofu Gwajima, iliyoko Mbezi Salasala jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kupiga kambi, jeshi hilo halikufanikiwa kumkamata na baadaye ilielezwa kuwa amekwenda nje ya nchi kuhubiri.

PAUL Makonda Afunguka na Kutolea Ufafanunuzi Kauli yake ya Kukamata Watu Wasio na Kazi Maalumu


Jukumu la Ulinzi na Usalama kwa ngazi ya chini lipo chini ya Serikali za Mitaa baada ya Serikali Kuu kuhamishia madaraka yake huko likiratibiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye kimsingi  kwa ngazi hiyo ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa husika.

Moja ya suala ambalo lilipata upotoshaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii ni kauli aliyotoa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya kutaka kuwatambua wakazi wa Dar es Salaam ambapo taarifa za kwenye mitandao ya kijamii zilizusha kwamba lengo lilikuwa ni kuwakamata watu wasio na kazi maalumu.

Kupitia Power Breakfast ya Clouds Fm Makonda amesema “Sikusema wasio na kazi maalumu wakamatwe kwa kuwa hatuna sehemu za kuwahifadhi hao wote watakaotiwa nguvuni, kimsingi huu ni upotoshwaji mkubwa uliofanyika kwenye mitandao ya kijamii, mimi nilitoa maelekezo kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wawafahamu na kuwatambua watu wao na shughuli wanazozifanya”.

Makonda amesema jukumu la ulinzi na usalama kwa ngazi ya Mkoa lipo chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa ambaye kimsingi ni Mkuu wa Mkoa na sio Meya wala mtu mwingine yeyote; ndiyo maana jukumu hilo ameamua kushirikiana na ngazi ya serikali ya mtaa kwani suala la ulinzi liliachiwa Jeshi la Polisi pekee na ndio maana lilionekana kulemewa.


“Hakuna mwenye uwezo wa kumzuia Mwenyekiti wangu wa Serikali ya Mtaa kwenda nyumba hadi nyumba akiwa na askari ili kuwatambua wakazi, suala la ulinzi ni jukumu letu sote … tukishindwa kuwatambua watu maana yake hata milioni 50 zitakazotolewa na Rais Magufuli ambapo Dar es Salaam itapata bilioni 28 na milioni 650 zitashindwa kuwafikia walengwa”. Alisema Makonda.

Kuhusu swala la ombaomba

Makonda amesema jumla ya ombaomba 687 walibainika kuwepo jijini Dar es Salaam huku asilimia 70 kati yao sio wakazi wa Dar es Salaam, na kusisitiza bado operesheni ya kuwaondoa inaendelea kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo hadi kufikia Agosti mwaka huu zoezi hilo litakamilika ili watoto ambao wanazurura wakiomba waweze kurejeshwa shuleni.

Juma Abdul Mchezaji Bora Ligi Kuu Msimu Uliopita


Abdul ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars amewashinda beki mwenzake, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shizza Kichuya.

Na kwa ushindi huo, Abdul mbali na kukabidhiwa taji na mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, pia atazawadiwa fedha Sh Milioni 9.2 wakati klabu yake, Yanga SC itazawadiwa Sh. Milioni 81.3 kwa kuwa bingwa, huku Sh. Milioni 40.6 zikienda kwa washindi wa pili, Azam FC, Sh Milioni 29 zikienda kwa washindi wa tatu, Simba SC na Sh. Milioni 23.2 zikienda kwa Prisons washindi wa nne.

Mlinda mlango wa Azam FC Aishi Salum Manula ameshinda tuzo ya kipa Bora akiwaangusha Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga na Benno Kakolanya wa Prisons na kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7 huku mfungaji bora Amissi Tambwe wa Yanga akizawadiwa pia Sh. Milioni 5.7.

Thabani Michael Kamusoko ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Kigeni, akiwaangusha Mzimbabwe mwenzake anayecheza naye Yanga SC, Donald Ngoma na kipa Muivory Coast wa Simba, Vincent Agban hivyo kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7 pia.

Mholanzi Hans van der Pluijm ameshinda tuzo ya Kocha Bora na kuzawadiwa Sh. Milioni 8, akiwaangusha Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar na Salum Mayanga wa Prisons.
Tshabalala ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi akiwaangusha Farid Mussa wa Azam na Shizza Kichuya wa Mtibwa Sugar na kuzawadiwa Sh. Milioni 4.

Ibrahim Hajib wa Simba ameshinda tuzo ya Bao Bora la Msimu na kuzawadiwa Sh. Milioni 3 akimuangusha Tambwe wa Yanga, wakati Mtibwa Sugar imezibwaga JKT Ruvu na Mgambo Shooting katika tuzo ya Timu yenye Nidhamu na kuzawadiwa Sh. Milioni 17.2.
Ngole Mwangole ameshinda tuzo ya Refa Bora na kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7 baada ya kuwaangusha Anthony Kayombo na Rajab Mrope.

Timu ya Mtibwa Sugar imeteuliwa kuwa timu yenye nidhamu Ligi Kuu Bara katika msimu uliopita wa 2015/16.

Rais Magufuli Aibua Ufisadi Mwingine wa Mabilioni ya Shilingi Ndani ya Jeshi la Polisi


Rais Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vilinafanya jeshi hilo kukosa heshima katika jamii huku akisema kuwa ana taarifa za jeshi hilo kuingia katika makubaliano ya kifisadi ya mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kununua sare za jeshi hilo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akiwaapisha makamishna wa Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo na kuongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba mabilioni hayo yalitolewa kwa siku moja lakini hadi leo hakuna hata sare moja ya iliyonuuliwa.

Ameshangazwa na jeshi hilo kutoa kiasi cha fedha kinachokadiriwa kuwa kati ya shilingi bilioni 40 hadi 60 kwa ajili ya sare za polisi ambazo hadi leo hakuna hata moja iliyonunuliwa na wakati huohuo jeshi hilo likikosa shilingi bilioni 4 tu za kukomboa magari yao zaidi ya 70 yanayoshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) huko bandarini.

Aidha, Rais Magufuli ameagiza uchunguzi ufanyike na wahusika wafikishwe mbele ya haki ila angalau hata nusu ya fedha hizo ziweze kurudishwa zikalipie magari ya polisi yaweze kutoka bandarini maramoja.

Amelitaka pia Jeshi la Polisi kuachana na utaratibu wa kuwa na watumishi ambao ni raia wa kawaida na badala yake polisi wenyewe ndio washike nafasi hizo kulingana na taaluma husika na kushangazwa na taarifa kuwa  Mhasibu Mkuu wa Polisi aliyetumbuliwa hivi karibuni kwa tuhuma za ubadhirifu alikuwa raia wa kawaida na sio polisi

Baada ya Kufunga Goli Kwenye Mchezo wa Europa League Samatta Afunguka


Mtanzania Mbwana Samatta aliweka rekodi ya kufunga katika michuano ya Europa League baada ya timu yake ya Genk kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 mbele ya Budućnost ya Montenegro.

Clouds FM kupitia kipindi chake cha michezo cha Sports Extra kilifanya mahojiano maalu na Samatta kutaka kujua mambo mbalimbali. Mtandao huu ukaona haitakuwa vibaya kama utakuletea kile alichokisema nyota huyo hasa kama ulikosa kusikiliza show ya Sports Extra.

sportsextra: Mbwana Samatta unajisikiaje kuwa Mtanzania wa kwanza kufunga goli katika michuano ya Europa League?

Samatta: Nimejisikia vizuri kwasababu ndiyo kitu ambacho kila siku nakipigania kuweza kufanikiwa, mshambuliaji unaweza kufunga magoli, nimejisikia vizuri na inanipa morali zaidi ya kuendelea kujituma.

sportsextra: Ulianza katika kikosi cha kwanza mbele ya Nikola Karelis mshambuliaji wa kutumainiwa wa Genk, hii inamaanisha kuwa mwalimu Peter Maes anakuamini sana kuliko mshambuliaji huyo anayehusishwa na kujiunga na klabu ya Nottingham Forest ya nchini England?

Samatta: Nafikiri sasahivi mwalimu ananiamini na anapenda kunitumia, ni kitu ambacho kwakweli ni kizuri kwangu mwenyewe binafsi lakini pia nafikiri yeye kwake anaona namsaada mkubwa kwenye timu yake nikiwa naanza kwenye kikosi cha kwanza. Nafikiri ni jambo la kusubiri muda utakapofika kilakitu kitakuwa wazi lakini kwa sasahivi nafikiri mwalimu anapenda kunitumia zaidi.

sportsextra: Watu wengi walikuwa wanajaribu kujiuliza kuwa Mbwana yupo wapi wakati wa likizo yako baada ya kusimama kwa Ligi Kuu ya soka nchini Ubelgiji. Watu wanataka kujua ulikuwa wapi Mbwana wakati wa mapumziko?

Samatta: Likizo nilikuwa Tanzania japo likizo ilikuwa fupi lakini nilikuwa nyumbani nimepumzika ilikuwa ni kipindi cha mwezi wa Ramadhani kwahiyo nilikuwa kwenye mfungo. Ilikuwa haina sababu ya kuonekana kwasababu ilikuwa ni kipindi cha mapumziko.

Ukifata program ya mazoezi kutoka kwenye timu, ilikuwa ni muda wa kupumzika kwa wiki moja halafu wiki nyingine unatakiwa ufanye mazoezi wewe mwenyewe binafsi. Lakini kwa bahati mbaya mimi sikupata muda wa kupumzika kwasababu wakati likizo inaanza mimi nilitakiwa nijiunge na timu ya taifa kwa ajili ya mechi dhidi ya Misri na baada ya hapo niliendelea na program ambayo nilipewa mimi binafsi.

Mchezaji anapopewa likizo anatakiwa apumzike kabisa kwasababu ni kipindi ambacho mwili wake unatakiwa ujirudi na kutengeneza nguvu mpya. Haina maana kwamba ukipewa likizo basi ujifue na kujiweka nondo hapana, muda wa mapumziko ni kipindi ambacho anatakiwa apumzike kama amepewa program basi afanye lakini asijichoshe.

sportsextra: Mbwana nafasi ya timu yako ya Genk sasa unaionaje katika michuano ya Europa League baada ya jana kupata ushindi mbele ya klabu ya Budućnost?

Samatta: Nafikiri bado tunakibarua kwasababu ni mechi ya kwanza na tumeshinda kwa goli 2-0, mpinzani sasahivi kichwani kwake anajua kwamba amefungwa goli mbili na anahitaji kurudisha na kupata ushindi akiwa nyumbani, kwahiyo kibarua bado kipo siwezi kusema moja kwa moja kwamba tutakata tiketi ya kucheza kwenye makundi lakini nafikiri tuna timu nzuri na tunaweza kufika huko kwa hiyo kila kitu ni wakati.

MAGUFULI 'Ilifika Mahali Kuna Wafanyakazi Weekend zao Walikuwa Wakizifanyia Dubai na Kurudi Jumapili".


Mh Rais amewafikishia salaam wale wote wenye tafsiri hasi juu ya hali ya uchumi inayojitokeza sasa ya kufungwa na kugeuzwa kwa mahoteli kuwa hosteli kama mtikisiko wa kiuchumi kwamba fikra na mitizamo yao si sahihi.

Mh. Magufuli amesema na hapa namnukuu, "Hii ni tafsiri kwamba wapangaji wa nyumba hizi walikuwa ni wafanyakazi serikalini".

Mh Rais ameongeza na kusema kwamba, "Ilifika mahali kuna wafanyakazi weekend zao walikuwa wakizifanyia Dubai na kurudi Jumapili".

Mh. Rais nimemnukuu akisisitiza kwamba, "Hapo nyuma nchi hii kuna watu walikuwa wao wanaenjoy huku wengine wakiwa watizamaji, hii hapana lazima tu-enjoy wote".