mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Sunday, May 21, 2017

TRUMP Adhihirisha Ubabe Wake Mbele ya Mfalme wa Saud Arabia..Azikataa Taratibu na Protoko Alizoandaliwa na Wenyeji Wake..!!!


Katika ziara itakayomoeleka Donald Trump katika mataifa kadhaa matano kuanzia Saud Arabia mpaka Brussels, Jerusalem ikiwamo imeonekana kupokelewa kwa mtazamo tofauti ukilinganisha na msimamo wake juuya uislamu na namna Saud Arabia ilivyompa heshima ya hali ya juu hasa wengi wakiilinganisha na ziara ya Obama aliyoifanya mara ya mwisho akiwa madarakani. 

Mambo yaliyoteka mijadala mitandaoni ni pamoja na 

Heshima Trump anayoonekana kuipata kutoka kwa taifa la Saud Arabia kuanzia kwenye mapokezi ambayo Obama hakuwahi kuyapata.

Kitendo cha Trump kumuweka mwanamke kama translater wa mazungumzo yao na mtazamo wa Arab kuhusu uhusika wa wanawake katika masuala nyeti katika jamii.

Swala la Melanie Trump kutokuvaa head scarf kama ilivyozoeleka kwa Hillary Clinton, Condoleezza Rice na Michelle Obama pamoja na staff wao waliokua wakivaa head scarfs kuenzi utamaduni wa Arab

Msisimko wa mji wa Riadh katika ziara hii ya Donald Trump ambapo wananchi wa Saudia wameonekana kuvutiwa na kumpokea Mr President kwa upendo bila kujali misimamo ya Donald Trump kuhusu Uislamu ambayo ndio dini ya Saudis

SERIKALI Yawatumia Mamilioni Wazazi wa Majeruhi wa Ajali ya Bus la Wanafunzi wa Lucky Vicent..!!!


Serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha,imetuma  Sh  44.9 milioni kwa wazazi wa majeruhi ya ajali ya Lucky Vicent wanaotibiwa hospitali ya Mercy iliyopo Marekani

Watoto wanaotibiwa Marekani ni Saidia Ismail, Wilson Tarimo na Doreen Mshana.

Akizungumza na waandishi  wa habari , Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo  amesema  kuna sababu ya kuelekeza nguvu kubwa kwa kuwasaidia majeruhi hao watatu walioponea chupuchupu kwenye ajali ya gari huko Karatu.

Pia alisema pesa hizo walizotuma zitaenda kusaidia familia zilizoondoka na majeruhi kwenda nchini Marekani na kwamba kila mzazi atapata Sh 11 milioni ,huku daktari aliyeondoka na majeruhi hao pamoja na muuguzi  watapata  Sh 5.5 milioni kila mmoja

"Tumetoa pesa hizo kwa familia zilizopo huko nchini Marekani ili ziweze kuwasaidia waliko huko ugenini," amesema Gambo

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa alisema fedha hizo zilizotolewa zinatokana na rambirambi zinazoendelea kuchangwa na wadau mbalimbali na ambako mpaka Mei 20 , Sh 67.99milioni  zilipatikana.

Amesema pamoja na kutoa Sh 44.72 milioni,fedha zilizobaki ofisini kwake ni Sh 23.27 milioni na akasema   fedha hizo zitaendelea kuwekwa huku timu ya wawazi wanne walioteuliwa na wafiwa wakiendelea kushirikiana na Serikali kuhakiki mapato na matumizi wa rambirambi hizo

"Kuna tuhuma nyingi ambazo zinadai rambirambi za wafiwa hazijawafikia wafiwa,taarifa hizo hazina ukweli,ofisi yangu imeratibu zoezi hilo kwa uaminifu wa hali ya juu na taarifa ya jumla imetolewa kwa umma juu ya mapato na matuzi yote," amesema Gambo

Alberto Msando Afunguka Kuhusu Video Iliyosambaa Akimshika Gigy Money Ikulu

Mwanasheria Alberto Msando amejitokeza na kuongelea kuhusu video iliyosambaa akimshika Gigy money sehemu za Kiuno, Amesema haya:

From @albertomsando - Nikikaa kimya nitakua mnafiki. Nimekosea. Kilichotokea hakikupaswa kutokea. I will be a man enough and say sorry kwa wote ambao nimewakwaza na kuwaangusha. Am so sorry. But the beauty of all this is we all are human. Kuna watu ambao wamekuwa wepesi kuhukumu. Siwalaumu. Ni sawa na ni haki yao. I made a stupid mistake. I take full responsibility. Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee. It could have been worse. And to all those who took time to text I appreciate. Thats friendship. #TheDon #Hennessy #TheClip

Kipindupindu chapiga kasi Yemen


Mlipuko wa Kipindupindu YemenHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMlipuko wa Kipindupindu Yemen
Shirika la Afya Dunia limeelezea mlipuko wa kipindupindu nchini Yemen ni kama tahadhari kwa sababu unasambaa haraka kuliko ilivyo tarajiwa.
Takriban watu 250 wamefariki dunia kwa ugonjwa huo mwezi uliopita.
Shirika la Save the Children limesema mamia ya watu wanaodhaniwa kuambukizwa ugonjwa huo wanaripotiwa kila siku na kwamba mlipuko huo karibuni utakuwa janga kubwa.
Ugonjwa huo ambao unasambaa kupitia uchafu katika chakula na maji, unaweza kudhibitiwa kirahisi, lakini mfumo wa afya nchini Yemen umevurugika kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya waasi wa Ki Houthi na majeshi ya serikali, ambayo yanaungwa mkono na muungano wa majeshi yanayoongozwa na Saud Arabia.

Thursday, March 16, 2017

Makonda ajitetea kuhusu Wema Sepetu, Gwajima


HATIMAYE Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametoa ufafanuzi kuhusiana na sababu za kuwatangaza hadharani watu waliohusishwa na dawa za kulevya wakiwamo Askofu Josephat Gwajima na mshindi wa taji la mrembo wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu.

Akizungumza katika hafla ya kutimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa huo kwenye viwanja vya Oysterbay jana, Makonda alisema uwazi katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni miongoni mwa sababu hizo, nyingine zikiwa ni kujiweka kwake mbali na vishawishi vya rushwa na pia kuwadhihirishia wananchi kuwa taarifa wanazotoa kuhusiana na vita hiyo zimekuwa zikifanyiwa kazi bila kusita.

Gwajima ambaye ni Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo jijini Dar es Salaam, pamoja na Wema ambaye pia ni msanii wa filamu, ni miongoni mwa watu maarufu kadhaa waliotajwa na Makonda katika orodha ya awali ya watuhumiwa 65 wa dawa za kulevya.

Wengine katika orodha hiyo ni pamoja na wanasiasa aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Iddi Azzan; baadhi ya wamiliki wa hoteli na klabu za usiku na pia wasanii wakiwamo Khalid Mohamed ‘TID’ na Chid Benz.

Watuhumiwa hao walitakiwa na Makonda kujisalimisha katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kwa mahojiano kabla ya hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa kwa baadhi yao.

Monday, November 28, 2016

LADY Jay Dee Arusha Jiwe Kigazani Baada ya Kauli ya Ruge Kuwa Walishamalizana


Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, alidai kuwa vituo vyake vinaweza kuanza kucheza kazi za Lady Jaydee iwapo akiwaruhusu wafanye hivyo.

Kupitia Instagram, Lady Jaydee ameijibu ofa hiyo kwa dongo lililowaendea wasanii waliowahi kumshirikisha kwenye nyimbo zao lakini kwa kuogopa kuingia matatani na kituo hicho chenye nguvu nchini, walifuta sauti yake.

“Kwahiyo wale mlio omba collabo sijui feat baadae mkaenda kufuta chorus zangu mtafanyaje ? Habariiiiiiiiiii zenu buaaaaaana  #SawaNaWao #TofautiNaHesabuZao,” aliandika Jide.

Ruge alitoa kauli hiyo Ijumaa iliyopita kwenye mahojiano na kipindi cha XXL.

“Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena [Lady Jaydee] kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,” alisema.

Ruge pia alisema ana muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee, japo amedai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko.’

Wiki kadhaa zilizopita Ruge na Joseph Kusaga walishinda kesi ya kuchafuliwa (defamation) iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Lady Jaydee na muimbaji huyo kuamriwa kuwaomba radhi.

“Tunashukuru walau tulishinda ile kesi lakini at least ilitengeneza mfano wa watu kuelewa kwamba tusipende kutuhumu vitu kama watu huna uhakika. Bahati nzuri pia hata katika hiyo kesi alisema mwenyewe hajawahi kusikia tunasema, aliambiwa na watu. Lakini ni mambo yashapita hayo.”

Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu 'Mzee wa Upako' Afunguka Kuhusu Sakata la Kuwatukana Majirani Zake


Siku tatu baada ya kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako, amejibu tuhuma hizo akisema anaishi kana kwamba hana jirani.“...Tunaishi kama majambazi tu, hujui jirani yako ni nani,” amesema.


Lusekelo amesema Yesu ambaye ni  mwana wa Mungu alikubali kudhalilishwa na baadaye kufa bila hatia hivyo na yeye alikubali kula kiapo katika nafasi ya utumishi wake.


Amesema magazeti wa  mitandao ya kijamii hayawezi kumshusha kwa kuwa hayakumpasha ila Mungu pekee.


Katika mahubiri yake yaliyohudhuriwa na waumini wengi kama ilivyo kwa Jumapili nyingine za karibuni kanisani kwake, Ubungo Kibangu, mchungaji huyo aliingia kwa mapokezi ya wimbo wa kuabudu uitwao ‘Angalia Bwana’ kabla ya waumini kuanza kumtunza kwa sadaka kama ilivyo kawaida ya ibada zake.


Katika mahubiri hayo alisema haiogopi jela, bali anaogopa kuvunja sheria za nchi na wala alipokamatwa na Polisi haikumtisha wala kumvunja moyo, kwani viongozi wa dini wamekula kiapo hadi kufa.


Aidha, alisema wapo waliosema kuwa Mzee wa Upako alikuwa anatukana, alidai kuwa matusi yake yote ni maandiko na anayetaka ufafanuzi wowote akipata nafasi amuulize yameandikwa katika vitabu gani li apate kuelewa.

Alisema mpumbavu sio tusi hayo ni maelezo na Yesu alitukanwa sana, na hata ushenzi si tusi lina maana pana ya kwamba huna hofu ya Mungu, mjinga ana dhambi ya mauti, inayomsubiri kwenda peponi.

Hata hivyo, aliwausia waumini wa kanisa hilo kuwa kamwe wasimtukane mtu kwa umbo ama rangi yake kwa kuwa hakupenda kuzaliwa hivyo na waishi hivyo kwa kutenda mema kwa kuwa ufalme wa Mungu watauona.

Alisema tangu kutokea kwa tukio amekuwa akipigiwa simu na watu ambao hakuwategemea huku waandishi wakimtaka kuzungumzia chochote wakiwamo waandishi wa habari ambao alisema walikuwamo ndani ya kanisa hilo jana.

Akifafanua kilichotokea siku hiyo, alieleza kuwa alitoka saa 11 alifajiri bila kufafanua alikuwa akitokea wapi, ndipo alipokutana na watu wawili akiwemo Mmasai na dada mmoja alipowauliza wanatokea wapi katika eneo hilo ambalo wakazi wengi wa huko hutoka na magari yao, ndipo ugomvi ulipoanzia.

“Hawa watu wa magazeti wanataka kuuza magazeti, barabara hiyo nimeijenga mimi hivyo nilikuwa na haki ya kuwauliza maana ni kibarabara... washenzi wakubwa wanaandika tu, halafu wanasema nimewatukana majirani kule hakuna jirani hajui wanaingia saa ngapi na wanatoka saa ngapi na hakuna hata habari za asubuhi. Kila mmoja anatumia gari lake,”alieleza Mzee wa Upako.


“Kwanza waliandika habari kwamba waumini hawatakuja kanisani badala yake wamejitokeza bila kukatishwa tamaa. Wakati mnajitokeza hapa mbele (kutoa sadaka), alipita mama mmoja amebeba mtoto, nilimwombea mwaka jana hapa kwamba atapata mtoto na leo amepata mtoto, sasa mbona magazeti yasiandike habari hizo?”


“Kwa nini wasiandike hayo mazuri ‘front page’ (ukurasa wa mbele)?, halafu mnaandika Mzee wa Upako matatani,matatani babu yako.”


“Najua na leo mmekuja mpo humu mnasubiri niseme, nasubiri mmalize kwanza nyinyi halafu na mimi ndiyo nitasema, baada ya mwezi mmoja najua mtakuwa mmemaliza,”alisema.