mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira
Showing posts with label burudani. Show all posts
Showing posts with label burudani. Show all posts

Sunday, May 21, 2017

Alberto Msando Afunguka Kuhusu Video Iliyosambaa Akimshika Gigy Money Ikulu

Mwanasheria Alberto Msando amejitokeza na kuongelea kuhusu video iliyosambaa akimshika Gigy money sehemu za Kiuno, Amesema haya:

From @albertomsando - Nikikaa kimya nitakua mnafiki. Nimekosea. Kilichotokea hakikupaswa kutokea. I will be a man enough and say sorry kwa wote ambao nimewakwaza na kuwaangusha. Am so sorry. But the beauty of all this is we all are human. Kuna watu ambao wamekuwa wepesi kuhukumu. Siwalaumu. Ni sawa na ni haki yao. I made a stupid mistake. I take full responsibility. Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee. It could have been worse. And to all those who took time to text I appreciate. Thats friendship. #TheDon #Hennessy #TheClip

Monday, November 28, 2016

LADY Jay Dee Arusha Jiwe Kigazani Baada ya Kauli ya Ruge Kuwa Walishamalizana


Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, alidai kuwa vituo vyake vinaweza kuanza kucheza kazi za Lady Jaydee iwapo akiwaruhusu wafanye hivyo.

Kupitia Instagram, Lady Jaydee ameijibu ofa hiyo kwa dongo lililowaendea wasanii waliowahi kumshirikisha kwenye nyimbo zao lakini kwa kuogopa kuingia matatani na kituo hicho chenye nguvu nchini, walifuta sauti yake.

“Kwahiyo wale mlio omba collabo sijui feat baadae mkaenda kufuta chorus zangu mtafanyaje ? Habariiiiiiiiiii zenu buaaaaaana  #SawaNaWao #TofautiNaHesabuZao,” aliandika Jide.

Ruge alitoa kauli hiyo Ijumaa iliyopita kwenye mahojiano na kipindi cha XXL.

“Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena [Lady Jaydee] kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,” alisema.

Ruge pia alisema ana muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee, japo amedai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko.’

Wiki kadhaa zilizopita Ruge na Joseph Kusaga walishinda kesi ya kuchafuliwa (defamation) iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Lady Jaydee na muimbaji huyo kuamriwa kuwaomba radhi.

“Tunashukuru walau tulishinda ile kesi lakini at least ilitengeneza mfano wa watu kuelewa kwamba tusipende kutuhumu vitu kama watu huna uhakika. Bahati nzuri pia hata katika hiyo kesi alisema mwenyewe hajawahi kusikia tunasema, aliambiwa na watu. Lakini ni mambo yashapita hayo.”

Sunday, November 27, 2016

PICHA ya Aunty Ezekiel na Moses Iyobo Ikionyesha Ujauzito Yawa Gumzo Mtandaoni


Moja kati ya picha ambazo zimekuwa zikisambaa kwa kasi katika mtandao wa Instagram leo Jumamosi ya November 26 ni picha ya muigizaji Aunty Ezekiel pamoja na mpenzi wake Mose Iyobo.

Picha hiyo ambayo imepostiwa na baadhi ya watu ikiwemo Mose Iyobo mwenyewe inamuonesha Aunty Ezikiel akiwa mjamzito, kitu ambacho kimefanya baadhi ya mashabiki wao kutoa comment za pongezi.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mose Iyobo na Aunty Ezekiel wana mtoto wa kike anayejulikana kwa jina la Cookie hivyo kwa mujibu wa post ya Mose Iyobo inawezekana wakawa wanatarajia mtoto wa pili.

Saturday, November 26, 2016

Kajala Naye Amjibu Wema, Kamuweka Wazi Mpenzi Wake (Video)

Na Hamida Hassan, Ijumaa
DAR ES SALAAM: Gumzo kubwa ndani ya wiki iliyopita ilikuwa ni kuhusu msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu kujiweka kwa modo aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Mgimbu ‘Calisah’ lakini siku chache baadaye Kajala Masanja akamjibu baada ya kudaiwa kujiweka kwa msanii wa filamu anayefahamika kwa jina la Mutra.
Habari za Kajala kujiweka kwa Mutra zilivujishwa na mtu wa karibu wa mastaa hao aliyeomba hifadhi ya jina lake huku ikidaiwa kuwa wamekuwa wakiongozana sehemu mbalimbali.


“Penzi la Kajala na Mutra ndiyo habari ya mjini, wanatoka kwa siri lakini ukikaa nao karibu utajua tu kuwa wana uhusiano, fuatilieni mtaujua ukweli,” alidai mtoa habari huyo.
Baada ya habari hizi kulifikia Ijumaa, Mutra alitafutwa kupitia namba yake ya simu ambapo alipopatikana alisema: “Mh! Ni kweli ila hatupendi kuweka wazi, lakini angeulizwa yeye kwanza, hata hivyo nipigie baadae nitakujibu vizuri kwa sababu nipo lokesheni.”

Alipopigiwa baadaye alisema kuwa Kajala ni mtu wake wa karibu wanafanya kazi zao za filamu. Alipobanwa kuhusiana na awali kukiri, alisema:“Dah! Naomba nisamehe kwa kukujibu hivyo, nilikuwa lokesheni ndiyo maana nikateleza kukujibu vile.”
Baada ya Mutra, Ijumaa lilimsaka Kajala kwa kumtumia ujumbe wa WhatsApp ambapo mahojiano kwa ufupi yalikuwa hivi:

Ijumaa: Kajala mambo, unadaiwa kutoka kimapenzi na msanii mwenzako Mutra, mnadaiwa kuwa karibu muda wote na mara ya mwisho mlionekana pamoja kwenye sherehe ya Steve Nyerere.
Kajala: Ndio hivyo.
Ijumaa: Ndio hivyo ni shemeji kwa sasa au? Funguka basi?
Kajala: Kimyaa.



VIDEO: Diamond Akiri Kuandika Nyimbo Baada ya Kuumizwa na WEMA Sepetu na JACK Wolper

Watu walizungumza mambo mengi sana baada ya kusikia kuwa Harmonize na Jackline Wolper na uhusiano wa kimapenzi huku walio wengi wakiamini kuwa alikuwa akitafuta kiki tu.  Walioamini hivyo ni kutokana na uhusiano wa kimapenzi ambao uliwahi kuwapo kati ya Diamond Platnumz ambaye sasa ni bosi wa Harmonize na Wolper.

Katika mahojiano haya yaliyofanyika kipindi cha nyuma kati ya Zamaradi Mketema wa Clouds Tv na mwanamuziki Diamond Platnumz, Diamond alikiri kuwa aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wolper na pia aliandika wimbo wa Mawazo baada ya kuumizwa na msichana huyo.

Mbali na Wolper, Diamond amekiri kuwa aliwahi kuandika nyimbo nyingi kuhusu Wema Sepetu ambaye alikuwa ni mmoja wa watu aliowahi kuwapenda sana lakini wakamuumiza.

Swali ambalo limekuwa likiwatatiza wengi hadi leo, ni kwanini Diamond alimuacha Harmonize kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Wolper kama yeye alishawahi kutoka naye, tena akaishia kumuumiza?

Hapa chini ni video ya Diamond Platnumz na Zamradi Mketema walipofanya mahojiano kipindi cha nyuma.

Wednesday, November 16, 2016

Picha:Vera Sidika Aonyesha Nyumba yake na Gari Analomiliki ni ‘Kufuru’

Mrembo maarufu wa Kenya, Vera Sidika ameonyesha kuwa na yeye ni miongoni mwa mastaa wanaomiliki vitu vya thamani.

Kupitia mtandao wa Instagram, Vera ameuonyesha mjengo wa kifahari anaoumiliki pamoja na gari aina ya Range Rover na kuwaacha mashabiki mdomo wazi.



“I still remember the days I prayed for the things I have now. Just believe in the person you want to be and then work hard for it. Because the Limit to your abilities is where you set them. Have a productive week ahead. 👑QVB👑,” aliandika Vera kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao huo.

Hatua hiyo ya mrembo huyo kuonyesha mali zake hizo imeonekana ni kama amemkejeli hasimu wake Huddah Monroe.

“I wonder why Huddah sees Vera as a. Challenge??? The beef is real.. Am happy my queen is more matured than her =, ignoring her to the fullest,” amecomment mmoja wa mashabiki kwenye picha hiyo.

Monday, November 7, 2016

Dogo Janja Kijana Aliyefaulu Kwa Maksi za Juu Somo la Kuanguka na Kuinuka Katika Ubora wa Kiwango cha Juu

Msanii wa hop hop wa Kundi la Weusi, Nikki wa Pili amesema rapa kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja ndiye msanii wake bora 2016. nikki-na-dogo-janja

Rapa huyo amedai Dogo Janja aliwahi kuteleza na kuanguka lakini ameweza kufanikiwa kuinuka katika kiwango cha juu mno huku akiwa na nidhamu ya hali ya juu na kuweza kufuta makosa yake.

“Abdul Kachaa aka Dogo Janja kijana mdogo aliyefaulu kwa maksi za juu somo lililowashinda mamilioni ya watu, wasomi, wafanyabiashara, wanamichezo,” Aliandika Nikki wa Pili Instagram. “Watu wa rika zote somo la kuanguka na kuinuka katika ubora wa kiwango cha juu, nidhamu, kufuta makosa yote,”

Aliongeza, “Show zake sasa zinaacha history, brand yake iko na professional look, confidence iliyovuka mipaka, kwa umri wake na aliyo ya fanya 2016. Namtangaza kuwa msanii wangu bora 2016,”

Dogo Janja ni mmoja kati ya wasanii wa hip hop waliofanya vizuri katika tamasha la fiesta lililofanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.

Saturday, November 5, 2016

Master J: Mimi na Hermy B ni kati ya watayarishaji wa muziki tunaoishi maisha mazuri

Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna muziki pasipo kuwa na watayarishaji wa muziki – lakini wao ndio wamekuwa wakiongoza kuishi maisha ya chini zaidi.



Akiongea na kipindi cha Ladha 3600 ya EFM, mtayarishaji mkongwe wa muziki hapa nchini Master Jay amesema kuwa kwa Bongo ni maproducer wachache wenye maisha ya kwendana na hadhi yao.

“Kati ya maproducer wanaoishi maisha mazuri hapa mjini ni mimi na Hermy B,” amesema Jay.

Master ameongeza kuwa yeye alishtuka mapema ndio maana akaamua kuachana na kazi hiyo kutokana na kutoona faida na kazi hiyo wakati huo huo akiwa na familia inayomtegemea.

Dr. Cheni Aeleza Sababu za Kutojihusisha Tena na Filamu Nchini


Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini, Dr Cheni amesema hatatoa tena filamu nyingine kutokana na hali ya kibiashara ilivyo katika tasnia ya filamu hapa nchini

Dr. Cheni alisema hayo alipokuwa akizungumza na E News ya EATV ambapo alisema kuwa kazi zao hazina ulinzi na haiwafaidishi wasanii ndio maana huoni umuhimu wa kuendelea kutoa kazi hizo

Dr. Cheni alisema ukitoa leo filamu mpya baada ya siku moja utaikuta imesambaa nchi mzima ikiwa inauzwa tena kwa bei chee, alipoulizwa hadi lini ndo atatoa filamu, alisema kuwa hadi hapo Serikali itakapoingilia kutatua suala la kazi zao

"Siwezi kutoa tena filamu hadi Serikali itakapo hakikisha kuwa kazi zetu zipo salama, ukitoa filamu leo siku moja ya pili ya tatu unazikuta chini zinauzwa ambazo ni bandia, kilio chetu sisi bongo movie ni kazi zetu zinaibwa, namuomba Rais Magufuli aingilie kati suala hili kwani vijana wengi wamejiajiri kwenye bongo movie "alisema Dr Cheni

Wednesday, November 2, 2016

Alikiba Aanzisha Lebo yake Abby Skills na Jokate Wapata Shavu

Imekuwa ni kama fashion sasa kwa wasanii wa
Bongo Fleva kwa kila mmoja kutaka kuwa na
lebo yake, ukiachilia mbali wale ambao
walikwisha tangulia kwenye mambo hayo na
lebo zao zikafanya poa.

King Kiba ameitobolea siri Perfect255 kuwa
yuko katika maandalizi ya kurudi rasmi katika
suala hilo la kusimamia wasanii (Kuanzisha
Lebo) na tayari kuna wasanii ambao amekwisha
fanya nao mazungumzo na watakuwepo chini ya
lebo hiyo.

“Me record lebo ninayo muda mrefu, lakini
sikuifanya matangazo, lakini kuna wasanii ambao
nilikuwa nawamiliki nikapumzika, sasa hivi narudi
tena najipanga upya kama unavyomuona Abby
Skills anafanya kazi vizuri na bado ataendelea
kufanya kazi zingine, Abdu Kiba pia ametoa
ngoma hivi karibuni lakini haijafanya vizuri lakini
ngoma ijayo itakuwa ni ya mimi na yeye. Pia kuna
msanii mwingine ambaye watu hawajawahi
kumsikia, pia kuna wakina Jokate, kina Dalila na
wengine kibao tu ambao wapo chini ya Lebo
yangu.”

Jay Dee Atiwa Hatiani, Atakiwa Amuombe Radhi Ruge wa Clouds FM

Mahakama ya Wilaya Kinondoni imemtia hatiani mwanamuziki nyota wa kike nchini Judith Wambura (Lady Jay Dee) kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.Tokeo la picha la lady jaydee

Mahakama hiyo imemuamuru aombe radhi kupitia kwenye chombo cha habari chenye "coverage" pana nchini kote na ikiwezekana duniani.

Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashtakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga kwa kuuchafua uongozi wa kampuni hiyo na viongozi wake kupitia mitandao ya kijamii katika malumbano makali kati ya pande hizo mbili.

Mei 2013, Clouds Media Group na Ruge walimburuza Jay Dee mahakamani kwa kile walichodai kwamba alikuwa akiwatukana kwenye mitandao ya kijamii.

Tuesday, November 1, 2016

Mr Blue Asema Hahitaji Meneja Kwenye Muziki Wake

Msanii wa muziki wa kurap, Mr Blue amesema hahitaji kuwa na meneja wa kumsaidia katika kazi zake za muziki kwa kuwa tayari alishawahi kuwa na mameneja zaidi ya watatu ambao hawakumpatia mafanikio.
f1cbmr-Blue-ft-alikiba-mboga-saba

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mboga Sana’ amesema alikuwa hawezi kuishi kwenye tasnia ya muziki bila kuwa na meneja lakini kutokana na kuona mchango wao kwake haukuzaa matunda.

“Mimi nilikuwa siwezi kuendesha maisha yangu ya muziki bila kuwa na meneja na nilifanya kazi chini ya mameneja watatu lakini kwa sasa nimesema basi sihitaji meneja tena nahitaji ushauri wa wadau namna ya kuboresha kazi zangu,” Mr Blue alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.

Rapa huyo pamoja na AliKiba wameshiriki kusapoti ngoma ya Abby Skills inayokwenda kwa jina la Averina , ambapo Abby amewataka mashabiki kumuunga mkono ili arejee vyema kwenye game kama zamani.

Sunday, October 23, 2016

MTV Mama Awards 2016: Watanzania Waambulia Patupu, Nigeria na South Africa Wang'ara

Usiku wa Jumamosi ya October 22 2016 Johannesburg Afrika Kusini ndio siku ambayo zilitolewa rasmi tuzo za MTV Mama 2016 kwa wasanii waliofanya vizuri kwa mwaka 2016, mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee mkusanyiko wa matukio yote kwenye videos.

Ni kawaida kwa watu maarufu kupewa heshima ya kutoa tuzo kwa kumtangaza mshindi, mshindi wa Big Brother Africa 2014 Idriss Sultan kutokea Tanzania na msanii na mtangazaji wa TV kutoka Angola Weza Solange walipewa heshima ya kutoa tuzo ya kundi bora.

Msanii wa Bongofleva Alikiba kutoka Tanzania, Sauti Sol kutokea Kenya na mrembo Yemi Alade kutokea Nigeria ambaye pia alishinda tuzo ya msanii bora wa kike walikuwa ni miongoni wasanii waliopewa nafasi ya kuperform.

Wasanii kutoka Tanzania wanaounda kundi la Navy Kenzo Aika & Nahreel walikuwa ni baadhi ya watu maarufu waliopewa heshima ya kutoa tuzo za MTV Mama 2016.

Msanii wa Nigeria Wizkid alipopanda kwenye state kuchukua tuzo yake ya msanii bora wa kiume MTV Mama Awards 2016, tuzo ambayo ilikuwa inawaniwa pia na mtanzania Diamond Platnumz.

Jina la mtanzania Diamond Platnumz lilikuwa katika list ya wasanii watakaoperform katika tuzo za MTV Mama 2016, Diamond aliperform wimbo wa Kidogodogo aliowashirikisha P Squre wa Nigeria.

Baada ya baadhi ya wasanii kuperform Partorankig wa Nigeria, Sarkodie wa Ghana, Kored Bello, YCEE na Falz wa Nigeria walikuwa katika list ya wasanii watakaoperform katika tuzo hizo.

Zamu ya utolewaji wa tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana ilikuwa ya msanii wa South Africa DJ Maphorisa akiwa kawashirikisha Wizkid wa Nigeria na DJ Buckz ndio waliofanikiwa kushinda tuzo hiyo ya MTV Mama 2016.

Wizkid hakuishia kushinda tuzo mbili pekee katika usiku huo, lakini waandaaji walikuwa wamemuweka katika list ya wasanii walioperform pamoja na DJ Maphorisa na Emcee.

Msanii Yemi Alade kutoka Nigeria ambaye anafanya vizuri na hit songs zake kadhaa ndio alitangazwa mshindi wa tuzo ya msanii bora wa kike ya MTV Mama 2016.

Baada ya kushinda tuzo ya msanii bora wa kiume kwa mwaka 2016, Wizkid wa Nigeria allitangazwa pia kuwa mshindi wa tuzo ya msanii bora wa mwaka wa tuzo za MTV Mama 2016.




Tanzania safari hii hakuna msanii aliyefanikiwa kushinda tuzo hata moja ya MTV Mama 2016, kwa upande wa tuzo ya Best Breakthrough Act aliyokuwa anawania Rayvanny wa WCB ilichukuliwa na Tekno wa Nigeria wakati tuzo ya chaguo la wasikilizaji iliyokuwa inawaniwa na Yamoto Band ilichukuliwa na Jah Prayzah wa Zimbabwe.




Msanii kutoka United State of America USA Future ndio alikuwa msanii wa mwisho kutoa burudani na kuhitimisha sherehe za utoaji wa tuzo hizo za MTV Mama 2016 kutoka Johannesburg Afrika Kusini.

NAIJUA familia ya mboga saba? Wengine wanapenda kuwaita watoto wa kishua ama familia bora. Hii ikiwawakilisha watoto wanaozaliwa kwenye familia yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi, kiasi cha kutumia mlo mmoja ukiwa na mboga tofauti na zinazobadilishwa kila uchao. Ndio, kuna familia nyingine bhana mlo unakuwa na mboga moja na huwa ni hiyo hiyo deile mpaka inachosha.

wee
Ingawa kuna dhana kuwa watoto wa kishua huwa wavivu kujitafutia kwa sababu kila anachokotaka hukipata tu nyumbani, lakini ukweli sio wote. Kuna wengine wanaamua kuchakarika kutafuta maisha yao wenyewe, hata hawalingani na wale waliotokea familia za watu duni ambao walikatisha masomo ili kusaka noti wakiwa kwenye umri mdogo kabisa.

Mwanaspoti inakuletea baadhi ya mastaa wa kike waliozaliwa kwenye familia ya mboga saba, lakini wanakomaa kivyao vyao ile mbaya wakijichanganya na wenzao kusaka noto kwa jasho na damu.

VANESSA MDEE

Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988. Vanessa anatokea familia bora ya Sammy Mdee ambaye kwa sasa ni marehemu. Enzi za uhai wake, baba ya Mzee alikuwa mtu mzito kwenye nchi hii akiwa mume wa Sophia.

Akiwa na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. Vanessa Mdee alikulia miji ya New York , Paris, Nairobi na Arusha, lakini kwa sasa jamaa anatisha mbaya kwenye fani ya muziki akitamba ndani na nje ya Afrika.

JOKATE MWENGELO

Huyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku baba yake akifanya kazi serikalini.

Kumbuka Jokate alizaliwa Washington DC, Marekani ambapo wazazi wake walikua wakifanya kazi huko. Alipomaliza masomo ya juu ya Sekondari pale Loyola ndipo alipoanza kujichanganya kwa kuwania taji la Miss Tanzania mwaka 2006 na kushika nafasi ya 2 nyuma ya Wema Sepetu, kisha kuhamia kwenye fani ya muziki, utangazaji, mitindo na ubunifu na sasa akipiga fedha.

WEMA SEPETU

Wema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye familia ya kibalozi akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa marehemu Balozi Isaac Sepetu.

Wema alizaliwa mwaka 1988 katika hospitali ya St. Andrew ya Dar es Salaam na amesoma elimu yake ya awali mpaka sekondari kwenye Shule ya Academic International iliyopo Dar es Salaam kabla ya kwenda Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka Chuo Kikuu cha Limkokwing.

Alianzia shindano la urembo akitwaa mataji kadhaa ikiwamo la Miss Tanzania 2006 kisha kuhamia kwenye filamu na sasa anaendelea kukimbiza akimiliki kampuni yake na akizalisha bidhaa zenye jina lake. Achana kabisa, ila ukiamua kubisha we bisha tu.

Eddy Kenzo Awatolea Uvivu MTV Base, Adai Ameshinda ila Tuzo Akapewa Mwingine

Msanii wa Uganda Eddy Kenzo asema kuna namna inafanyika kuamua washindi wa MTV Mama na si upigaji wa kura maana kwenye kipengele change yeye ndo alikuwa na kura nyingi akifuatiwa na Mr. Flavour huku alieshinda Casper nyovest alikuwa na tatu kwa wingi wa kura...

Eddy KenZo Ameandika namnukuu
"Mimi Balozi wa mtandao wa Simu wa Airtel, Bahati Mbaya Mtandao wa Simu wa MTN ndo Wadhamini wa TuZo Za #mtvmama2016 na Mshindi ktk kipengele nilichotajwa Ni Balozi wa MTN (umeona eeeh) Eddy Kenzo akaendelea kutoboa "kumbuka nimetumbuiza ktk nchi 35 Na nchi 10 Kati ya Hizo nimetumbuiza nikiwa na nyomi la Kwenye Viwanja vya Mpira kuna nn mafanikio gani Zaidi ya hayo?
.
Walituambia tupige Kura Na Mashabk zangu walifanya hivyo Kwa kwenda kwenye mitandao ya MTV, Eddy Kenzo akasisitiza "Nenda Kwenye mtandao wao Na bonueza kipengele Cha #BestLiveAct Na ukajionee Mshindi nani, sina wivu mm (Kama Jux 🙈) Ila na lalamika kwasababu walituambia tupge Kura na mashabiki wakafanya maamuzi, nenda Kwenye page MTV ukaangalie walichosema Hata Kwenye emails, mm Eddy Kenzo ndo niliyepigiwa Kura Zaidi ya wote ktk kipengele Cha Best Live Act Na Msanii Ston Boy alikua wa Pili, Mr Flavour alikua wa TATU, Na Caspa Nyovest alikua wa Nne ktk Platforms zote MTV Base Africa, lakini mwisho wa cku mtu wa 4 ndo amepewa TuZo, jamani jamani Hata ingekua Wewe Povu lingekutoka tu, au mm ckuwaelewa waliposema tupige Kura Kwa Msanii unayempenda? Eddy Kenzo akamalizia Kwa kuwashukuru mashabiki zake Na Mwenyezi Mungu, imetafsiriwa Na MAKOROKOCHO @soudybrown .
Eheeeeeee nimejitahd kutafsiri Na ka dictionary Kangu ka kunyapia nyapia 🙈
.
Kwa anachokimaanisha Eddy Kenzo Ni kuwa wasanii Kama Navy Kenzo Hata wangefanya nn wasingepata TuZo kwasababu Ni mabalozi wa AIRTEL Tanzania, pia Bwana Diamond Platnumz asingeweza kupata TuZo kwasababu yeye Ni Balozi wa Vodacom, Ya Moto Band Na Ali KIBA nao wasiweza kupata TuZo kwasababu Ni mabalozi wa mtandao wa Simu wa @shilawadu Kazi kweli kweli #mtvmama2016 sio watu wa Spoti Spoti -

Joketi Kujenga Viwanja Vya Michezo

Mrembo, Jokate Mwegelo ameahidi kujenga viwanja vya michezo kwa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mahafali ya nane ya shule hiyo, Jokate alisema atajenga viwanja hivyo kupitia kampeni yake yake ya kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified.”

Amesema ameguswa na changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo na kuamua kusaidia kwa kupitia kampeni yake hiyo.

Tayari Jokate amekabidhi viwanja katika shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani

Wednesday, October 19, 2016

Babutale amezijibu shutuma za baadhi ya mashabiki nchini kuwa wasanii wa WCB wamekuwa wakinunua tuzo.

Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM, Tale alikuwa na maneno mafupi tu kuwajibu. “Kama ni rahisi na wao wakanunue,” alisema meneja huyo.

Jumamosi iliyopita Diamond na Harmonize walishinda tuzo za Afrimma zilizofanyika jijini Dallas, Marekani.

Alidai kuwa tuzo hizo ni za Tanzania nzima na imeonesha jinsi gani mashabiki wako nao pamoja. Amesisitiza kwa kuwaomba waendelee kuwapigia kura wasanii wote waliotajwa kwenye tuzo za MTV MAMA wakiwemo wasanii wake wa WCB, Diamond na Raymond.

Wengine ni Alikiba, Navy Kenzo, Yamoto Band na Vanessa Mdee.

Muuza sura kwenye video za Kibongo, Lulu Abass ‘Lulu Diva’ (pichani juu) na mwenzake Amber Lulu (pichani chini) hawana bifu lolote isipokuwa kuna watu wana mpango wa kuwagom-banisha.

Akichonga na Risasi Vibes, Lulu Diva alifunguka kuwa awali aliposikia kuwa Amber alimpaka matope kwenye ‘interview’ aliyofanya na redio fulani Bongo, alipaniki na kumtafuta ili amueleze kulikoni, lakini Amber alimwambia hakuna kitu kama hicho na kumtaka kuchunguza mwenyewe.

“Nilichunguza na kukuta kumbe si kweli, niligundua ni watu wasiopenda ushoga wetu ndiyo walikuwa wanajaribu kutukosanisha na si vinginevyo,” alisema Lulu Diva.

Monday, June 6, 2016

Video : Ommy Dimpoz Nae Kaamua Kutoboa Pua na Kusema Haya....


Kuna uwezekano mkubwa hii style mpya ya wasanii wa kiume kutoboa pua ikaenea kwa wasanii wengi zaidi. Ilianza kwa msanii Chid Benz ambae mara baada tu ya kuonekana katoboa pua ilikua gumzo sana sio tu magazetini hata mitandaoni huku wasanii wengi wakipingana na maamuzi yake.

Itakumbukwa pia kua Diamond Platnumz alifikia hatua hadi ya kumuimba Chid kua katoboa pua ila cha kushanaza mwaka huu nae Diamond katoboa pua. Ishu ya Diamond kutoboa pua ishasambaa sana ila mpya kwa sasa ni Ommy Dimpoz nae kutoboa pua!!!

Imenaswa video ikimwonyesha Ommy Dimpoz akiwaonyesha mashabiki wake kua nae katoboa pua, hadi akatoa heleni ya sikioni na kuiweka puani. Unaweza ona video hiyo hapa chini.....