mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Wednesday, November 2, 2016

Alikiba Aanzisha Lebo yake Abby Skills na Jokate Wapata Shavu

Imekuwa ni kama fashion sasa kwa wasanii wa
Bongo Fleva kwa kila mmoja kutaka kuwa na
lebo yake, ukiachilia mbali wale ambao
walikwisha tangulia kwenye mambo hayo na
lebo zao zikafanya poa.

King Kiba ameitobolea siri Perfect255 kuwa
yuko katika maandalizi ya kurudi rasmi katika
suala hilo la kusimamia wasanii (Kuanzisha
Lebo) na tayari kuna wasanii ambao amekwisha
fanya nao mazungumzo na watakuwepo chini ya
lebo hiyo.

“Me record lebo ninayo muda mrefu, lakini
sikuifanya matangazo, lakini kuna wasanii ambao
nilikuwa nawamiliki nikapumzika, sasa hivi narudi
tena najipanga upya kama unavyomuona Abby
Skills anafanya kazi vizuri na bado ataendelea
kufanya kazi zingine, Abdu Kiba pia ametoa
ngoma hivi karibuni lakini haijafanya vizuri lakini
ngoma ijayo itakuwa ni ya mimi na yeye. Pia kuna
msanii mwingine ambaye watu hawajawahi
kumsikia, pia kuna wakina Jokate, kina Dalila na
wengine kibao tu ambao wapo chini ya Lebo
yangu.”

No comments:

Post a Comment