mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira
Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

Monday, November 28, 2016

Lowassa Awajibu wanasiasa waliodai ni mgonjwa na atakufa


Aliyekuwa  mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewashukuru wananchi kwa kumpigia kura kwa wingi licha ya baadhi kumsema vibaya kwa kumwita mgonjwa na kwamba angekufa.


Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alitoa kauli hiyo mjini Mbinga mkoani Ruvuma ambako chama hicho kipo katika ziara ya kufanya mikutano ya ndani.


Akizungumza ndani ya vikao hivyo, Lowassa pasipo kutaja jina la mtu yeyote alisema: “Mwacheni Mungu aitwe Mungu, kwa sababu wote hata walionisema mabaya baadhi yao wameshatangulia mbele ya haki.”


Alisema kitendo cha wananchi kumpigia kura kwa wingi pamoja na kwamba alikuwa akizungumziwa vibaya juu ya afya yake, ni wazi kuwa walikubali kubeba lawama juu yake.


“Bila ujasiri na umoja wa dhati, hawa jamaa wataendelea kutupiku… lakini niwashukuru vile vile kwa kukubali kubeba lawama juu yangu, wapo waliosema huyu ni mgonjwa atakufa, bado mlinipigia kura nyingi ila Mungu ndiye hupanga yote,” alisema.


Pamoja na hayo, Lowassa aliwataka wanachama wa Chadema kuendelea kuwa na ujasiri na kudumisha umoja kwa kuendelea kujipanga kwa uchaguzi wa mwaka 2020.


Hii ni mara ya kwanza kwa Lowassa kuzungumza juu ya watu ambao walihoji kuhusu mwenendo wa afya yake wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.


Baadhi ya wanasiasa, hususani wale waliokuwa wakimpinga, walijaribu kuionyesha na hata kuiaminisha jamii kwamba mwanasiasa huyo ni mgonjwa na hafai kuongoza nchi.


Wapo ambao walidiriki kusema kwamba Ikulu si hospitali na wala hakuna gari la kubebea wagonjwa.


Miongoni mwa wapinzani wake ni baadhi ya wanasiasa wakubwa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwamo viongozi waliosikika katika majukwaa ya kampeni  mwaka jana wakiwashawishi wananchi kutomchagua Lowassa kwakuwa hata akipata urais hatotawala muda mrefu atakufa.


Wapo waliokwenda mbali na kusikika wakimwambia Lowassa Ikulu si wodi ya wagonjwa, hivyo hafai kupatiwa nafasi ya urais kulingana na afya aliyonayo.


Mikutano ambayo Lowassa ameitumia kuzungumzia suala hilo, inafanyika nchi nzima pamoja na kuwahusisha wajumbe wa ngazi mbalimbali za chama.


Uwepo wa Lowassa katika mikutano hiyo imesababisha watu wengi kukusanyika wakitaka kumuona.


Hata Lowassa anapokuwa anaondoka katika eneo hilo kuelekea mahali kupumzika, wananchi wamekuwa wakiunga msafara kwa kumfuata nyuma.


Mikutano hiyo inatajwa kuwa sehemu ya operesheni ya siku 40 inayofanyika nchi nzima iliyopewa jina la ‘Amsha Amsha

Saturday, November 26, 2016

KIMENUKA..Kura za Urais Kuhesabiwa Upya Marekani

Tume ya uchaguzi katika jimbo la Wisconsin nchini Marekani limepokea ombi la kurudiwa kuhesabu kura za uchaguzi uliopita ambapo mshindi alikuwa Donald Trump aliyeshinda kwa kura chache wiki mbili zilizopita.

Ombi la kurudiwa kuhesabu kura liliwasilishwa na mgombea wa urais kupitia chama cha  Green Party Jill Stein ambaye pia ametaka kura zirudiwe kuhesabiwa katika majimbo ya  Michigan na Pennsylvania.
Hata hivyo ikiwa Hillary Clinton atashinda jimbo hilo hakutabadilisha matokeo ya ushindi wa Trump kwani lina kura 10 pekee za wajumbe wa uchaguzi.
 Kamisheni hiyo imethibitisha kupokea maombi hayo na kuainisha kutoa maelekezo muda si mrefu.

CHADEMA Waibuka Mafichoni na Kulionya Jeshi la Polisi

NAIBU Katibu Mkuu (Bara) wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amelitaka Jeshi la Polisi kuacha kufuatilia mikutano yao ya ndani, inayoendelea sehemu mbalimbali nchini.

Mnyika alisema hayo mkoani Singida juzi akiwa kwenye moja ya mikutano ya ndani, iliyoandaliwa na Chadema kwa lengo la kuimarisha viongozi wake ngazi ya kata na wanachama ili waweze kuwafikia wananchi wa vijijini.

Naibu Katibu huyo alisema siyo jambo zuri polisi inapotumika vibaya kufuatilia mikutano ya Chadema, wakati ipo kikatiba na kuruhusiwa na serikali.

Kwa mujibu wa Mnyika, mkutano huo uliokutanisha wajumbe wa wilaya ya Ikungi, jimbo la Singida Mjini na Singida Kaskazini, ulikuwa na lengo la kuwapika viongozi wa kata ili wakaijenge Chadema imara maeneo ya vijijini.

Akizungumzia mikutano hiyo, Waziri Mkuu mstaafu wa serikali awamu ya tatu ambaye hivi sasa ni mjumbe kamati kuu ya Chadema, Fredrick Sumaye aliwataka viongozi hao wa kata kuhakikisha chama kinapata mafanikio ili hatimaye kiweze kushika dola.

Mbali ya Mnyika na Sumaye, viongozi wengine wa Chadema waliohudhuria walikuwa Mbunge Ester Matiko (Tarime Mjini), Susan Masele (Mwanza), Rose Kamili (Manyara), Jesca Kishoa (Singida) na wajumbe wengine watatu wa sekretarieti ya Chadema makao makuu.

Wednesday, November 16, 2016

Hillary Clinton: Nilitaka kujificha kabisa


Hillary Clinton alitunukiwa heshima na wakfu wa Children's Defense Fund katika Newseum mjini Washington DC
Image captionHillary Clinton alitunukiwa heshima na wakfu wa Children's Defense Fund katika Newseum mjini Washington DC
Mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameelezea masikitiko yake alipojitokeza hadharani mara ya kwanza tangu ashindwe kwenye uchaguzi wa rais nchini Marekani na Donald Trump wa chama cha Republican.
Bi Clinton, akihutubu mjini Washington DC amesema alikuwa hataki kutoka nyumbani tena.
Ameambia shirika la kuwasaidia watoto wasiojiweza kwamba uchaguzi huo umewafanya Wamarekani wengi kutafakari.
Bi Clinton aliongoza kwa wingi wa kura za kawaida lakini akashindwa kinyang'anyiro cha urais kupitia kura za wajumbe, ambazo ndizo huamua mshidni wa urais.
"Sasa, nitakiri kwamba kuja kwangu hapa halikuwa jambo rahisi," alisema alipokuwa akitunukiwa heshima na wakfu wa Children's Defense Fund.
"Kuna nyakati kadha wiki hiyo moja iliyopita ambapo nilitaka kujikunyata tu nikiwa na kitabu kizuri na nisiwahi kutoka nje ya nyumba tena."
Hillary ClintonImage copyrightGETTY IMAGES
Aliendelea: "Ninajua wengi wengu mmevunjwa moyo sana na matokeo ya uchaguzi. Hata mimi, pia, zaidi kushinda ninavyweza kueleza.
"Ninajua si jambo rahisi. Najua wiki moja iliyopita, watu wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo Marekani ni nchi ambayo tumekuwa tukiamini ndiyo.
"Migawanyiko iliyowekwa wazi na uchaguzi huu imekolea, lakini tafadhali nisikezi ninaposema hili.
"Marekani ni ya thamani. Watoto wetu ni wa thamani. Kuweni na imani katika nchi yetu, mpiganie maadili yetu na daima, msikate tamaa."
Grey line
Alipokuwa anatoa hotuba ya kukubali kushindwa wiki iliyopita, Bi Clinton alsiema Bw Trump anafaa kupewa fursa ya kuongoza.
Tangu wakati huo, amekuwa haonekani, ingawa siku moja alionekana akifanya matembezi porini.
Mfuasi wa ClintonImage copyrightFRANK FRANKLIN II / AP
Image captionBi Clinton alishinda ngome za Democratic California, Oregon, New York, New Jersey, Connecticut, Massachusetts, Maryland, Vermont, Delaware, Illinois, Rhode Island, Hawaii, Washington na District of Columbia, pamoja na New Mexico na Colorado.
Kwenye mawasiliano ya simu ambayo yalifichuliwa kwa wanahabari Marekani, alisikika akimlaumu mkurugenzi mkuu wa FBI James Comey, aliyetangaza kuanzishwa kwa uchunguzi mpya kuhusu kashfa yake ya barua pepe zikiwa zimesalia siku 11 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.
Baadaye uchaguzi ulipokuwa umekaribia kabisa, Bw Comey alisema hakukupatikana ushahidi mpya ambao ungebadilisha uamuzi wa awali wa FBI kwamba hakukuwa na ushahidi wa kumfungulia mashtaka.


Sunday, November 13, 2016

Mbunge Godbless Lema Akipona Katika Hili Abadili Mbinu zake Katika Siasa

Siasa za kutengeneza matukio ya kujiongezea umaarufu zinaanza kumwendea vibaya Lema.

Idadi ya watu waliojitokeza mahakamani katika kesi ya Lema leo imekuwa ndogo sana ukilinganisha na uhamasishaji uliofanyika.

Picha zinazorushwa kutoka maeneo ya mahakama hazioneshi zile "nyomi" tulizozizoea pindi Lema anapopelekwa mahakamani.

Hata wanachama kindakindaki wanaofuatilia kesi hii kwenye mitandao kama Facebook wamekuwa wakimtaja Bananga pekee kama chanzo cha taarifa kutoka mahakamani.

Hata tukio linalopewa umaarufu la mwanamke anayedaiwa kuzimia linaripotiwa kwa picha inayoonesha watu wachache sana wakiwa na mama huyo.

Muda umefika Lema atathmini siasa zake zisije zikampa maumivu makali kuliko matokeo yaliyotarajiwa.

Monday, November 7, 2016

Wanawake waliosubiri miaka 96 kumpigia kura mwanamke


Wanawake waliopiga kura kwa njia ya postaImage copyrightI WAITED FOR 96 YEARS
Image captionWanawake hawa, wote wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 96, walipiga kura kwa njia ya posta na kupashana habari
Tarehe 8 Novemba, mamilioni ya wanawake wa kimarekani watafanya kile ambacho hawakupata fursa ya kukifanya kabla - kumpigia kura mwanamke aliyeteuliwa kama mgombea mkuu wa chama kuwa rais wa Marekani.
Kwa baadhi yao hii kikomo cha miaka 96 ya kusubiri.
Yeyote aliyezaliwa kabla ya tarehe 18 Augusti 1920 nchini Marekani alianza maisha katika nchi ambayo haikumruhusu wanawake kupiga kura.
Hao ni pamoja na Estelle Schultz, mwenye umri wa miaka 98, aliyekuwa akifanya kazi kwenye viwanda viwili katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia na mwalimu wa muda mrefu,ambaye alipelekwa kwenye kituo cha kupigia kura kama mtoto na mama yake kushuhudia namna kura zinavyopigwa.
Estelle ana matatizo makubwa ya moyo na yuko chini ya uangalizi wa hospitali. Lakini anasema: "nimeamua kwamba ningependa kuishi muda mrefu wa kutosha kuweza kushudia kuchaguliwa kwa mwanamke wetu wa kwanza rais ."
Sarah Benor alituma ujumbe kwa niaba ya bibi yakeImage copyrightSARAH BENOR
Image captionNinatuma hii kwa ombi la bibi yangu mwenye umri wa miaka 98, ambaye hatumii kompyuta ,' aliandika Sarah
Mwezi Oktoba, alipokuwa akipiga kura yake ya awali kwa njia ya posta, alisema kuwa alibaini ni kiwango gani hali hiyo "ilivyo muathiri" , na akamuomba mjukuu wake wa kike Sarah kutuma picha yake hii kwenye Facebook
Picha hii ilipendwa na mamia ya watu kwa ishara ya ''like'', suala lililoibua shauku ya sara na familia yake kutafuta taarifa zinazofanana na ya bibi yao.
Waliwapata wengine wengi, na wavuti " Nilisubiri miaka 96 " ulianzishwa, na kujaa kauli kutoka kwa wafuasi wa Hillary Clinton waliozaliwa kabla wanawake kuwa na haki ya kupiga kura.
Baadhi ni watu wazima wa kutosha kiasi cha kukumbuka wakati wanawake walipopewa fursa ya kupiga kura, mara baada ya kuidhinishwa kwa marekebisho ya 19 ya katiba ya Marekani.
''Jerry''EmmettImage copyrightAP
Image captionMfuasi wa Democrat mwenye umri wa miaka 102 "Jerry" Emmett pia ni mchangiaji wa tovuti
"nakumbuka nikimsindikiza mama yangu tukiwa kwenye farasi kuelekea kwenye kituo cha kupigia kura katika uchaguzi wa kwanza ambapo wanawake waliruhusiwa kupiga kura. Hatimae baada ya muda mrefu nilikuwa na haki ya kupiga kura ,"aliandika Juliet Bernstein mwenye umri wa miaka 103 kutoka Massachusetts, ambaye alizaliwa mwaka 1913, na kupaya shahada ya kwanza kwa kutiwa hamasa na mama yake.
Mama yangu alikuwa miongoni mwa wanawake wa kwanza kukata nywele zao kuwa fupi na kubadilisha mtindo wa sketi ndefu zilizokuwa zikiburuzwa kwenye matope na kuvaa magauni mafupi ," alisema Beatrice Lumpkin, mwenye miaka 98, kutoka Chicago.
"yote ni juu ya haki zetu , wakianza na haki yao ya kupiga kura. Nilipokuwa mtu mzima kiasi cha kuelewa ni vipi wapigania haki ya kupiga kura nilijivunia sana''
Baadhi ya wachangiaji wa mtandao huo wanasema wanayo furaha kuwa na fursa ya kumpigia kura mwanamke kama raia katika kipindi cha uhai wao - kitu ambacho wengi hawakudhani kingewezekana.

Trump: Wasomali wanaeneza itikadi kali Marekani


Mgombea wa urasi nchini Marekani Donald Trump asema jamii ya Wasomali nchini Marekani inaenneza itikadi kali
Image captionMgombea wa urasi nchini Marekani Donald Trump asema jamii ya Wasomali nchini Marekani inaenneza itikadi kali
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump ameishambulia jamii ya Wasomali wanaoishi katika jimbo la Minnesota nchini Marekani ,akiwalaumu kwa kueneza maoni yenye itikadi kali nchini humo.
Alitumia mfano wa kisa cha shambulio la kisu lililotekelezwa na mhamiaji raia wa Somalia mnamo mwezi Septemba katika mji wa St.Cloud ,akisema kuwa wakaazi wa Minnesota wameteseka vya kutosha.
Bwana Trump ambaye alikuwa katika ziara ya kampeni kabla ya uchaguzi wa Jumanne amesema kuwa iwapo atakuwa rais atahakikisha kuwa wakaazi wa maeneo wanashauriwa kabla ya wakimbizi kupelekwa ili kuishi.
Hivi ndivyo alivyosema Trump:
"Viongozi wetu wana ujinga kiasi gani? Wana Ujinga kiasi gani kuruhusu mambo kama haya kutokea? Hapa Minnesota mumekabiliwa na matatizo chungu nzima kutokana na ukaguzi mbovu wa wakimbizi, huku idadi kubwa ya Wasomali wakiingia katika jimbo hili bila wakaazi kufahamishwa,bila usaidizi wenu ama hata ruhusa.
Huku wengine wakijiunga na kundi la wapiganaji wa Islamic State na kueneza maono yao ya itikadi kali katika kila pembe ya nchi pamoja na dunia nzima kwa jumla.
Kwa kweli ni vigumu kuamini na kila mtu anasoma kuhusu mikasa inayotokea Minnesota...Mumeona kisa cha shambulio la kisu katika eneo la St Cloud.
Serikali ya Trump haitasajili wakimbizi bila usaidizi wa jamii ya eno hili.Hilo ndilo wanaweza kuwafanyia kwa sababu mumeteseka vya kutosha."
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Jumanne 8 Novemba, 2016.

Saturday, November 5, 2016

Tundu Lissu Akataa Kujisalimisha Mahakamani Bila Barua ya Wito

Siku moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuagiza Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akamatwe kwa kushindwa kuhudhuria kortini, mbunge huyo amedai hana taarifa hizo hivyo hawezi kujisalimisha popote.

Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, alidai atajisalimisha tu kwenye vyombo vya dola au kwenda mahakamni ikiwa atapelekewa barua aliyoandikiwa na mahakama na kutiwa saini na kugongwa muhuri na hakimu.

“Kaka, mimi siwezi kufanyia kazi za magazeti katika masuala ya kisheria, nipo hapa ninaendelea na shughuli zangu kama kawaida na kama mnavyoniona niko katika kuwawakilisha wananchi wa jimbo langu,” alieleza Lissu.

Mwanasheria huyo mkuu wa Chadema alitoa maelezo hayo jana alipohojiwa kuhusiana na habari zilizoandikwa na vyombo vya habari, kwamba Mahakama ya Kisutu juzi iliagiza mbunge huyo akamatwe baada ya kushindwa kuhudhuria katika kesi inayomkabili.

Mbali ya mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa kwa Lissu, pia iliagiza iandaliwe hati ya kuitwa mahakamani kwa wadhamini wake ili wajieleze kwa nini wasilipe fungu la dhamana walilotia saini ambalo ni Sh10 milioni.

Kwa mujibu wa Hakimu Mkazi wa Kisutu, Thomas Simba, Lissu amekuwa hahudhuri kortini kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili pamoja na wahariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa na mchapaji wa magazeti, Ismail Mehboob.

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14 mwaka huu, Dar es Salaam, Lissu na wenzake walikula njama za kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti la Mawio lenye kichwa cha habari: “Machafuko yaja Zanzibar”.

Juzi, siku ambayo kesi hiyo ilipangwa kutajwa tena, Lissu hakuwapo mahakamani kutokana na kile mdhamini wake Robert Katula alichodai kuwa mshtakiwa huyo anaendesha kesi ya uchaguzi Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Mwanza hivyo asingeweza kuhudhuria.

Kutokana na maelezo hayo wakili wa upande wa Jamhuri, Patrick Mwita aliomba mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa mshtakiwa jambo ambalo Hakimu Simba alikubali pamoja na wito kwa wadhamini kufika mahakamani Novemba 21, mwaka huu.

Alipoulizwa kuhusu hatua hiyo, Lissu alisema kuwa wito wa kwenda mahakamani ni lazima barua iwe imeandikwa na kugongwa muhuri na kutiwa saini ya hakimu wa mahakama na siyo kusikia na kwenda bila ya kuwepo kwa wito kamili.

Wednesday, March 16, 2016

CCM NYAMAGANA KUMSAFIRISHA KWA NDEGE MSANII ALIETEMBEA KWA MIGUU KUTOKA JIJINI MWANZA HADI DAR.


Rafael Shilatu ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana (Kulia) akizungumza katika hafla ya kumpongeza msanii Rich4D.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG.
Chama cha Mapinduzi CCM kimekubali kumsafirisha kwa ndege Mwanamuziki Chipukizi Richard Stanford maarufu kwa jina la Rich4D, alietembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es Salaam ili kumpongeza Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuwajumuisha Wasanii katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Raphael Shilatu, alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, katika hafla ya kumpongeza msanii huyo kwa matembezi yake baada ya kurejea Jijini Mwanza.
“Kwanza nimpongeze kwa matembezi yake ambayo ni ya kizalendo kabisa. Lakini niseme kwamba atakapopata fursa ya kwenda kuonana na Mhe.Rais, tutamsafirisha kwa ndege kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar na kumrudisha pia”. Alisema Shilatu huku akimuomba Katibu Mkuu Mhandisi John Kijazi kumsaidia msanii huo ili aweze kuonana na Mhe.Rais Dkt.Magufuli.
Januari 16 mwaka huu Msanii Rich4D alianza matembezi yake kutoka Jijini Mwanza na kupita katika Mikoa Minane sawa na kilomita 1,200 hadi kufika Jijini Dar Februari 10, hii ikiwa ni siku 26 mfululizo za matembezi hayo ambayo mbali na kumpongeza Rais Dkt.Magufuli, pia yalilenga kuwasilisha kilio cha wasanii chipukizi wa Mikoani ambao wamekuwa wakikosa fursa mbalimbali ikilinganishwa na wasanii wakubwa walioko Jijini Dar.
“Kila Mkoa na Wilaya nilizopita nilipokelewa na
viongozi mbalimbali wakiwemo Maafisa Utamaduni na baada ya kufika Dar
nilipokelewa na Viongozi wa Serikali akiwemo aliekuwa Katibu Mkuu
Ombeni Sefue ambae aliniahidi kuonana na Mhe.Rais kabla mwezi wa mwili haujaisha kwani nilishindwa kuonana na rais baada ya kuambiwa yuko katika majukumu mengine ya Kitaifa”.
Alitanabaisha Rich4D na kumuomba Katibu Mkuu mpya Mhandisi John Kijazi kuhakikisha ahadi aliyoiacha Sefue inatimia.
Msanii Rich4D akionyesha Vibali alivyokuwa navyo kabla ya kuanza matembezi yake.
                    Bonyeza HAPA Kutazama Picha za Mapokezi.

VIONGOZI WA CHADEMA ARUSHA WARUDI CCM BAADA YA UTEUZI WA KATIBU MKUU


Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha wameanza
kurudisha kadi za chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
mara tu baada ya uteuzi wa Katibu Mkuu mpya wa Chama.

Viongozi hao wa CHADEMA Arusha wametoa madai kadhaa ambayo yamewafanya kufikia uamuzi huo kwa nyakati tofauti.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Olumuriaki Ndugu Godfrey Kitomari na wanachama wanachama wa
chadema 97 wa Kata ya Sombetini wamerudi CCM kwa sababu zifuatazo;-

1. Kuridhishwa na kasi ya Mhe Dkt Magufuli.
2. Kuchukizwa na Mbowe kukiuza chama na kuiacha agenda ya kukemea ufisadi kama ilivyokuwa mwanzo na badala yake kuwatetea.
3. Uteuzi wa Katibu Mkuu asiye na uwezo lakini mwenye rekodi mbaya kwenye jamii.
[​IMG]
Pichani: Ndugu Kitomari akiveshwa Kofia ya CCM kwenye Mkutano wa hadhara wa kukaribishwa CCM.
[​IMG]
Wananchi wa Kata ya Sombetini wakishuhudia tukio la Mwenyekiti huyo wa Mtaa kujiunga na CCM.
[​IMG]
WanaCCM wakimlaki Ndugu Kitomari mara baada ya kujiunga na Chama hicho.
Katika tukio jingine; 
Mwenyekiti wa BAVICHA Kata ya Mjini Kati Ndugu Ally Kaole (pichani) naye
amejiuzulu nafasi yake hiyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi – CCM.

Kaole ametoa sababu za uamuzi wake huo kuwa ni;-
1.
Uteuzi wa Katibu asiyekijua Chama lakini asiyejua falsafa za Uongozi na
Utawala, amesema uteuzi huo unalenga kuua Chama hicho. Ndugu Ally
amedai kuwa Katibu Mkuu mpya wa CHADEMA na yule aliyestaafu hawafanani
hata chembe, ni sawa na kufananisha Kifo na Usingizi.

2.
Amesikitishwa na Mwenyekiti wa Chama kutetea majipu tena hadharani,
akisema hatua hiyo imeondoa uhalali wa yeye kuwepo katika chama hicho
ambacho aliamini kuwa kinachukizwa na majipu na kwamba kilikuwa kinaomba
ridhaa ili kuyashughulikia.

[​IMG]
Pichani: Ndugu Ally Kaole (aliyekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Arusha.