mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Monday, April 4, 2016

HEKTA 5000 ZA ARDHI YA KIJIJI CHA LUHANGA WILAYANI MBARALI ZARUDISHWA KWA WANANCHI KUTOKA WAWEKEZAJI

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala akizungumza na wananchi wa kijiji cha Luhanga Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya kwa lengo la kutoa tamko la serikali juu ya ulejeshwaji wa ardhi ya wananchi hao hekta 5000 ambazo zilichukuliwa na wawekezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala akisisitiza jambo katika Mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu huyo wa Mkoa kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Luhanga (Hawapo Pichani)Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya .
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Luhanga Mbarali Mkoani Mbeya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu huyo wa mkoa(Hayupo Pichani) kwa lengo la kulejeshewa ardhi yao iliyochukuliwa na wawekezaji .
Mkutano ukiendelea katika kijiji cha Luhanga Mbarali kati ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Wananchi wa kijiji hicho ambao walikuwa katika mgogoro mkubwa wa ardhi na wawekezaji.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mbeya Guram Shekifu akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala mara baada ya kumaliza mgogoro huo.
Wananchi wakifuatilia Mkutano.
Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali Mbeya wakichukua kumbukumbu za Mkutano huo.
 
SERIKALI Mkoni Mbeya, imezirejesha hekta 5000 za ardhi ya kijiji cha Luhanga Wilayani Mbarali, zilizokuwa zimetolewa kwa wakulima zaidi ya 200 wa chama cha Luhanga (Luhanga AMCOS), huku ikiuagiza uongozi wa halmashauri kuwachukulia hatua watendaji wote walihusika na mchakato wa ugawaji wa ardhi hiyo.
Akikabidhi ardhi hiyo leo, kwa wananchi wa Kata ya Luhanga, Wilayani humo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala, alisema serikali imefikia uamuzi huo baada ya kubaini kwamba zoezi hilo lilifanyika kinyume  na sheria na kanuni za ardhi za vijiji zinavyoelekeza.
Amesema, sheria  mama namba 5 ya ardhi ya mwaka 1999, imebainisha kwamba halmashauri ya kijiji haina mamlaka ya kugawa ardhi zaidi ya ekali 20 au 50 lakini wao wamegawa ardhi zaidi ya hekta 5000.
Mkuu huyo ameongeza kuwa mbali na zoezi hilo kughubikwa na ukiukwaji wa sheria lakini pia, wawekezaji hao wameonekana ni wababaishaji  kutokana na kushindwa kutimiza ahadi za maendeleo walizokuwa wamezitoa kwa wananchi wa eneo hilo.
 Aidha, Makala, aliwatahadharisha wananchi hao, kujiepusha na walaghai wa ardhi na kuacha kugawa ardhi ovyo kwani rasilimali hiyo haiongezeki ukilinganisha na mahitaji ya watu, ambao kila siku wanaongezeka idadi.
 
Amesema serikali inaweza kufanya uparesheni ya kuwataka vijana wafanye kazi lakini kama wananchi au viongozi wanauza ardhi zoezi hilo haliwezi kufanikiwa . 
 
Amesema mkoa wa mbeya unajulikana kwa kuongoza kwa migogoro ya ardhi hususani wilaya ya mbarali hivyo yeye kama mkuu wa mkoa  atahakikisha anashughulika vyema na suala hilo.
 
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka jamii za wafugaji wa kimasai kuhakikisha wanaachana na tabia ya kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo badala yake wawalitihishe katika elimu ambayo ndio mkombozi kwao.

Sunday, April 3, 2016

SAKATA la Mabosi wa NHC na EWURA Kulipwa Mshahara wa Milioni 36 Lachukua Sura Mpya Baada ya Wenyewe Kukana

Mabosi  wa mashirika mawili ya Serikali nchini, wanaodaiwa kulipwa mshahara wa Sh milioni 36, wamekanusha madai hayo, huku wakielezea kushangazwa na taarifa hizo wakati hata nusu ya fedha hizo, hawapati.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu alisema  halipwi mshahara huo.

Akijibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo kuhusu taarifa ya utekelezaji na utendaji wa shirika hilo kwa mwaka 2014/15, Mchechu alisema shirika hilo pamoja na kutekeleza majukumu yake, bado lina changamoto za uhaba wa fedha.

“Katika ujenzi wa nyumba zetu, Serikali haigharamii masuala ya miundombinu kama vile maji, umeme, barabara hilo ni jukumu letu na linatugharimu fedha nyingi. 

“Sasa nashangaa wako watu wanasema mimi nalipwa mshahara mkubwa, sielewi wametoa wapi huo mshahara kwa sababu silipwi mshahara huo, mimi nalipwa chini ya huo walioutaja,” alisema Mchechu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura),Felix Ngamlagosi aliiambia kamati hiyo kwamba mamlaka hiyo ina changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa watumishi na maslahi duni. 

Alisema wakati maslahi ya wafanyakazi ni duni, ameshangaa kusikia vyombo vya habari vikisema yeye ni miongoni mwa wakurugenzi wanaolipwa Sh milioni 36 kwa mwezi.

“Jamani hapa tunazungumzia maslahi duni ya watumishi wetu, nashangaa kusikia naambiwa nalipwa milioni 36, mshahara wangu haufiki hata nusu ya hizo fedha,” alisema Ngamlagosi.

 Nyumba nafuu 
Awali wajumbe wa kamati hiyo baada ya kupitia taarifa hiyo ya NHC, waliiomba Serikali kuharakisha kuwepo kwa sera ya nyumba ili kurahisishia mashirika yanayohusika na masuala ya ujenzi wa nyumba kujenga nyumba za bei nafuu kwa wananchi.

“Yapo malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba NHC mnauza nyumba kwa bei kubwa, huku mkitoa matangazo kuwa nyumba hizo ni bei nafuu,” alihoji mjumbe wa Kamati hiyo, Mbunge wa Ushetu, Elias Kwandikwa. 

Akijibu hoja hiyo, Mchechu alisema nyumba zinazojengwa na NHC zinauzwa kuanzia Sh milioni 30 hadi 250 kwa fedha taslimu na kwamba mnunuzi atatakiwa kulipa kodi.

Aliongeza kuwa kama mnunuzi hatakuwa na fedha taslimu, benki washirika wanatoa mikopo kwa ajili ya ununuzi wa nyumba hizo, ila wanunuzi watatakiwa kulipa riba za benki husika. 

Baada ya majibu hayo, wajumbe hao walitaka Serikali iangalie jinsi ya kupunguza mzigo kwa shirika hili na ikiwezekana waondolewe kodi ya uingizaji vifaa vya ujenzi ili kusaidia nyumba hizo kuuzwa kwa bei nafuu, kwa lengo la kuwanufaisha wananchi hasa wale wa kima cha chini.

Akizungumzia hoja hizo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula alisema shirika hilo, linapaswa kuwasiliana na watendaji katika maeneo husika ya ujenzi wa nyumba hizo, ili wawasaidie kubeba gharama ndogondogo.

“Serikali na wizara zinafanya kazi kwa ushirikiano na NHC, na hili la gharama za miundombinu, kila halmashauri nchini ambayo ujenzi wa nyumba hizo unafanywa, inaweza kuangalia jinsi ya kusaidia gharama za miundombinu, ili nyumba hizo ziuzwe kwa bei nafuu zaidi kwa wananchi,” alisema Mabula.

Hali si shwari kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) baada ya wafanyabiashara wa mataifa yanayotumia Bandari ya Dar es Salaam kutafuta sehemu nyingine kiasi cha kusababisha kiwango cha mizigo kupungua kwa asilimia 50.

Bandari hiyo, ambayo ni maarufu kwa usafirishaji wa mizigo inayokwenda na kutoka nchi za Malawi, Congo, Uganda, Burundi na Rwanda, imekumbwa na kadhia hiyo baada ya wafanyabiashara wa nchi hizo kuamua kutumia bandari nyingine za Beira, Msumbiji na Durban ya Afrika Kusini.

Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Hebel Mhanga alisema hali ya biashara kwa sasa si nzuri kwa kuwa mtiririko wa shehena za mizigo umepungua ikilinganishwa na miaka iliyopita.

“Miaka yote shehena ya mizigo bandarini ilikuwa ikiongezeka kwa kati ya asilimia 10 mpaka 11, lakini sasa imeshuka mpaka kufikia asilimia 50,” alisema Mhanga kwenye semnina ya wahariri iliyofanyika ofisi za bandari hiyo jana.

Mhanga alitoa mfano wa shehena iliyokuwa ikisafirishwa na wafanyabiashara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), kuwa imepungua kwa asilimia 50 huku mizigo ya wafanyabiashara wa Zambia ikipungua kwa asilimia 46.

Alitaja sababu zilizochangia kuporomoka kwa biashara hiyo kuwa ni pamoja na wafanyabiashara hao kuanza kukatwa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Alisema tangu sheria ya ulipaji wa VAT ilipopitishwa mwaka jana, wasafirishaji wote wanaotumia bandari hata wale ambao mizigo yao inasafirishwa kwenda nchi jirani, wanalazimika kulipia kodi hiyo.

Sababu nyingine ni utaratibu wa himaya moja ya forodha kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Alisema baada ya kuona mfumo huo unafaa, Tanzania iliamua kuutumia kwa nchi nyingine ambazo hazipo katika jumuiya hiyo.

Alisema katika utaratibu huo, nchi zote zinakuwa na mwakilishi katika ofisi za TPA na masuala ya kodi na mizigo yote inalipiwa ushuru nchini kabla ya kusafirishwa kwenda nchi zao.

“Hili limekuwa mwiba kwa wenzetu wa DRC, kwani nchini mwao mfumo wa ukusanyaji kodi unatoa mianya ya ukwepaji, kwa hiyo kwa kutumia njia hii ni wazi kuwa kila mzigo utalipiwa hapa nchini kabla haujasafirishwa, jambo wanaloona linalowaongezea gharama za uendeshaji,” alisema.

Mhanga alisema kutokana na hali hiyo, kwa sasa wafanyabiashara hao wameamua kutumia bandari za nchi nyingine kupitisha mizigo yao, akizitaja kuwa ni Durban na Beira.

Sababu nyingine aliyoitaja ni kushuka kwa thamani ya Randi dhidi ya Dola ya Marekani, kitu alichosema kinawafanya wasafirishaji kuona kwamba wakipitishia mizigo yao Dar es Salaam wanatumia fedha nyingi kuliko Durban.

“Ulipaji wetu unawalazimisha wafanyabiashara watumie Dola wakati wao wanatumia Randi ya Afrika Kusini na sasa imeshuka, hivyo njia rahisi kwao ni kutumia Bandari ya Durban kwa kuwa watapunguza gharama za usafirishaji,” alisema.

Alisema sababu ya nne ni kukamilika kwa ujenzi wa njia ya reli kutoka Malawi hadi Beira.

Alisema usafirishaji mizigo kwa njia ya reli ni nafuu kwa kuwa unapunguza gharama kwa asilimia 30 na pia hutumia siku chache hivyo wafanyabiashara wengi sasa wanatumia bandari ya Beira badala ya Dar es Salaam. 

 “Kutofanya vizuri kwa reli yetu ni kikwazo kikubwa kwa biashara ya bandari. Mfano hadi Desemba 2015, jumla ya tani 14.8 zilipita bandari yetu, lakini ni asilimia 0.01 pekee ndiyo iliyosafirishwa kwa njia ya reli na asilimia 99.9 ilisafirishwa kwa barabara,” alisema meneja huyo.

Meneja huyo alisema ili kunusuru hali hiyo, busara inahitajika zaidi, ikiwa ni pamoja na kupitia upya sheria hiyo ya VAT.

Alisema kwa upande wao wameshafanya maboresho ili kuvutia wawekezaji kuja nchini, ikiwa ni pamoja na kuimarisha matumizi ya teknolojia tofauti na awali.

Alisema kwa sasa wamezindua mfumo mpya unaojulikana kama ‘Habour View’ unaosaidia kupokea taarifa zote za meli, mizigo na ulipaji hivyo mteja anaweza kulipia kwa njia za benki na simu.

Alisema wamefupisha muda wa kushusha mzigo katika meli hadi kufika siku mbili tofauti na awali ilipokuwa inachukua siku sita.

Alisema kwa upande wa shehena ya magari, mwaka 2010 uwezo ulikuwa ni kushusha magari 200 lakini kwa sasa wana uwezo wa kushusha magari 700.

Awali, Mkurugenzi wa Masoko wa TPA, Fransisca Muhindi alishauri Serikali kuwekeza katika kutangaza bandari hiyo ili kuinusuru.

“Wenzetu hawalali, wanafanya biashara ya ‘door to door market’(nyumba kwa nyumba), wanawekeza kiasi kikubwa. Ni bahati mbaya sana sisi hatuwekezi. Kuna usemi unasema wekeza shilingi ili upate shilingi,” 

Hali si Nzuri Bandari ya Dar es Salaam.....Mizigo Yapungua Kwa Asilimia 50

Rais Magufuli Atoa shilingi Milioni 10 nyumbani kwao Geita leo Kuchangia Upanuzi wa Kanisa

Rais Magufuli ametoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa kanisa la bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita kwa ajili kuchagia upanuzi wa kanisa hilo ambapo fedha hizo zimekabidhiwa na kaimu mnikulu Ngusa Samike katika misa ya pili ya ibada ya Jumapili ya pili ya Pasaka, iliyofanyika kanisani hapo leo tarehe 03 April, 2016.

Kabla ya misa hiyo ya pili Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa pamoja na Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga na Mkewe Mama Ida Odinga, walisali misa ya kwanza ambapo Rais Magufuli aliahidi kuchangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya upanuzi wa kanisa hilo ambao unaendelea.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema katika misa hiyo Paroko wa Parokia ya Chato, Padre Henry Mulinganisa alieleza kuwa kanisa hilo linatarajia kuadhimisha miaka 50  tangu kuanzishwa kwake baadaye mwaka huu, na kwamba maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na upanuzi wa kanisa ambao unachangiwa na waumini wenyewe.

Padre Mulinganisa amemshukuru Rais Magufuli kwa mchango huo na amemuahidi kuwa utatumika vizuri ili uendeleze upanuzi wa kanisa hilo pamoja na michango ya waumini wengine.

GARI Lateketea Kwa Moto Pamoja na Dereva Akiwa Ndani..

KUNA GARI IMEPATA AJALI MAENEO YA MBEZI BEACH AFRICANA GARI NO T598BEL TOYOTA LANDCRUISER DEREVA KAUNGUA HAJAFAHAMIKA HATA KWA SURA,SAMBAZA UJUMBE HUU GROUP TOFAUTI ILI WENYE NDUGU WAMFAHAMU,GARI LIPO POLISI KAWE.

Friday, April 1, 2016

TUZINGATIE USAWA WA KIJINSIA KATIKA JAMII

Wanafunzi wakisikiliza semina

 Bi Fatma Amiry akitoa semina ya jinsia katika ukumbi wa chuo cha uandishi wa habar

Watanzania kote nchini wametakiwa kuachana na mifumo ya kizamani ya kubagua wanawake na kuwaona wanaume ndio watu muhimu badala yake wafate usawa wa kijinsia na kuona watu wote ni sawa.

Hayo yamesemwa na  Bi. Fatma Amiry ambaye ni Afisa ustawi wa jamii mkoani Arusha  katika semina  ya  kupinga unyanyasaji  wa kijinsia na maambukizi ya Ukimwi iliyofanyika katika ukummbi wa chuo cha Uandishi wa Habari na utangazaji  Arusha (AJTC).

Ameeleza kuwa  jamii  nyingi  za kitanzania bado zinamitazamo  hasi kuhusiana na suala la usawa  wa kijinsia  kutokana na mila na destuuri walizojiwekea  ambazo  zinaleta migogoro na usnyanyasaji wa kijinsia.

Bi Fatma amesema  jamii inatakiwa ibadilike kulingana na wakati uliopo ili kuweza kuleta usawa huo katika jamii ikiwa ni pamoja na wanawake kurithi mali,kupewa elimu na kutokudharauliwa
“Ni wakati wa mabadiliko katika jamii zetu, maisha ya zamani ni tofauti na sasa hivyo nawaomba watanzania wenzangu waache kunyanyasa jinsia tofauti ili kuweza kutimiza malengo ya haki sawa kwa wote”Alisema Bi. Fatma Amiry

Licha ya hayo pia amewashauri vijana na jamii kwa ujumla  kupima afya  na kuwa  waaminifu kwa wapenzi wao  ili kuweza kupunguza kasi ya maambukizi  ya  virus vya  Ukimwi
Kwa upande wake mkufunzi wa chuo hicho Bw. Lucas Modaha amesema  vijana na wanandoa wajiheshimu na kulinda utu ili kuepuka maambukizi mapya ya VVU