Wanafunzi wakisikiliza semina
Bi Fatma Amiry akitoa semina ya jinsia katika ukumbi wa chuo cha uandishi wa habar
Watanzania kote nchini wametakiwa kuachana na mifumo ya kizamani ya kubagua wanawake na kuwaona wanaume ndio watu muhimu badala yake wafate usawa wa kijinsia na kuona watu wote ni sawa.
Hayo yamesemwa na Bi. Fatma Amiry ambaye ni Afisa ustawi wa jamii mkoani Arusha katika semina ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia na maambukizi ya Ukimwi iliyofanyika katika ukummbi wa chuo cha Uandishi wa Habari na utangazaji Arusha (AJTC).
Ameeleza kuwa jamii nyingi za kitanzania bado zinamitazamo hasi kuhusiana na suala la usawa wa kijinsia kutokana na mila na destuuri walizojiwekea ambazo zinaleta migogoro na usnyanyasaji wa kijinsia.
Bi Fatma amesema jamii inatakiwa ibadilike kulingana na wakati uliopo ili kuweza kuleta usawa huo katika jamii ikiwa ni pamoja na wanawake kurithi mali,kupewa elimu na kutokudharauliwa
“Ni wakati wa mabadiliko katika jamii zetu, maisha ya zamani ni tofauti na sasa hivyo nawaomba watanzania wenzangu waache kunyanyasa jinsia tofauti ili kuweza kutimiza malengo ya haki sawa kwa wote”Alisema Bi. Fatma Amiry
Licha ya hayo pia amewashauri vijana na jamii kwa ujumla kupima afya na kuwa waaminifu kwa wapenzi wao ili kuweza kupunguza kasi ya maambukizi ya virus vya Ukimwi
Kwa upande wake mkufunzi wa chuo hicho Bw. Lucas Modaha amesema vijana na wanandoa wajiheshimu na kulinda utu ili kuepuka maambukizi mapya ya VVU
No comments:
Post a Comment