Sandwich ya kienye
Mapishi: dakika 7
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Mahitaji
- Mayai 2
- Kitunguu maji 1
- Nyanya 1 (zisimenywe, maana zinaliwa kama kachumbari)
- Kitunguu saumu 1 (Kimenywe na kupondwa)
- Pilipili hoho 2 (napenda zenye rangi tofauti ili kuleta rangi nzuri kwenye chakula)
- Chumvi
- Karoti 1 (Menya maganda)
- Pilipili manga ya unga
- Mkate (Unaweza pia kutumia mkate wa kutengeneza mwenyewe kama ulivyoelezwahapa)
Wapi kwa kupata bidhaa?
Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.
Maelekezo
Sandwich hii pia inaweza kuliwa kwa kuweka salad, au chochote kingine unachopendelea kula na mkate. Unaweza pia kutumia mkate wa kutengeneza mwenyewe kama ulivyoelezwa hapa. Ni vizuri kujaribu vitu tofauti ili ufahamu ladha tamu ya vyakula.- Anza kukaanga mayai – menya kitunguu kizima na karoti nusu, kata vipande vidogo kisha hifadhi kwenye chombo pembeni. Kata pilipili hoho, hifadhi pembeni. Kwenye chombo tofauti, pasua yai, koroga vizuri. Ongeza chumvi, pilipili manga na kitunguu saumu kwenye yai. Koroga pamoja vizuri, hifadhi pembeni.
- Bandika kikaango jikoni, weka mafuta. Acha yapate moto. Weka kitunguu. Koroga ili kiive na kulainika. Ongeza pilipili hoho na karoti kiasi. Acha ziive kidogo, takribani dakika 2 hadi 4. Mie huwa napenda pilipili hoho zisiive sana, maana zinakuwa na virutubisho zaidi na harufu nzuri.
- Mimina mchanganyiko wa yai kwenye kikaango. Acha lipate kuiva vizuri upande mmoja kisha geuze upande wa pili. Likiiva vizuri toa na hifadhi pembeni.
- Kata nyanya na nusu karoti kwenye vipande vidogo, kama unavyopendelea kachumbari yako iwe.
- Pasua mkate katikati. Panga yai, na nyanya katikati ya mkate. Kama una sauce, mimina ili uweze kuongeza ladha.
- Hiki ni chakula kamili, unaweza kunywa na kinywaji ukipendacho. Kinaenda vizuri pia na maji.
- Jirambe na ladha ya maisha.
MAPISHI YAPENDWAYO
No comments:
Post a Comment