mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Wednesday, April 20, 2016

MLO WETU LEO

Viazi mviringo, maharage machanga na mayai

Chakula hiki ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma ambayo husaidia kuongea damu. Hii inatokana na kuwa maganda ya viazi yana kiwango kikubwa sana cha madini ya chuma, hivyo ni chakula murua kwa mtu anayehitaji kuongeza damu.

Mahitaji

  • Viazi 6
  • Maharage machanga fungu 2 (green beans)
  • Mayai 4
  • Pilipili hoho 1, ikatwe vipande vidogo
  • Chumvi
  • Vitunguu 2 (vidogo au wastani, kama kikubwa sana 1 kinatosha) kata vipande vidogo
  • Mafuta ya kula (nimetumia mafuta ya zaituni (olive oil))

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Chakula hiki kinaliwa na maganda yake. Ni muhimu sana maana yana virutubisho vingi vya chuma. Hiki ni chakula kizuri kwa wale wanaopenda kuongeza damu mwilini.Unaweza pia kupika viazi hivi kama chips lakini viazi visimenywe na ukapata virutubisho toka kwenye maganda ya viazi.
vviathi
  • Osha viazi. Weka kwenye sufuria, ongeza chumvi kiasi na ubandike jikoni. Acha vichemke vizuri hadi viive. Takribani dakika 15.
  • Kuna njia nyingi za kupika maharage mabichi, mie nimechemsha kawaida. Bandika sufuria jikoni, weka maji kisha acha yachemke.
  • Chukua kiasi cha maharage yanayotosha kula, kata ncha zake kwa kisu kisha weka kwenye sufuria yenye maji  yanayochemka kisha funika vizuri na mfuniko. Baada ya dakika 7 hadi 10 maharage yatakuwa yameiva. Toa na tenga kwenye sahani pembeni.
  • Weka kikaangio jikoni, ongeza mafuta ya kula, acha yapate moto. Weka kitunguu, kisha pilipili hoho.
  • Pasua mayai kwenye bakuli, weka chumvi kiasi. Koroga vizuri. Mwaga yai kwenye kikaango, acha liive vizuri, kisha geuza upande wa pili. Likiiva, toa na tenga kwenye sahani.

No comments:

Post a Comment