mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Friday, April 15, 2016

Ushindi Yanga, Azam waitesa Simba



KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja, amesema Ligi Kuu Tanzania Bara imezidi kuwa ngumu baada ya Yanga na Azam kushinda mechi za viporo, lakini amejipa moyo nafasi ya ubingwa bado ipo wazi.
Yanga juzi iliifunga Mwadui FC ya Shinyanga mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Azam FC iliifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 Uwanja wa Manungu, Turiani.
Azam imemaliza mechi zake za viporo, ambapo imecheza mechi 24 ikiwa na pointi 55 ikishika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga iliyocheza mechi 23 ikiwa na pointi 56.
Yanga itamaliza mechi yake ya viporo Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba ndiyo inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 24.
Kocha Mayanja alisema ushindi wa Yanga na Azam umezidisha ugumu kwenye ligi na sasa hawana budi kuongeza jitihada kushinda mechi zao.
“Hakuna kupumzika, lazima kichwa kiume kujua tutafanya vipi kuwa mabingwa, ligi imezidi kuwa ngumu,” alisema.
Taji la ubingwa wa ligi ndilo pekee lililobaki kwa Simba kulipigania baada ya kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Kombe la FA) mwanzoni mwa wiki hii.
Simba inatarajiwa kushuka dimbani Jumapili kuikaribisha Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mechi yenye ushindani wa hali ya juu kutokana na timu hiyo ya Mwanza kutoa upinzani mara kwa mara inapokutana na Simba.
“Mechi yetu na Coastal ni ngumu, na matokeo ya wapinzani wetu yamefanya iwe ngumu zaidi, kwani sasa ni lazima tushinde kama tunataka kuendelea kwenye mbio za ubingwa,” alisema Mayanja.

No comments:

Post a Comment