mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Friday, April 8, 2016

BMT yataka vyama vifanye uchaguzi


Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja
Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT), limetoa siku 14 kwa vyama na mashirikisho ya michezo nchini ambayo hayajafanya uchaguzi kufanya hivyo, ili kupata viongozi mbalimbali kulingana na katiba zao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja, klabu ambazo hazijafanya uchaguzi kutimiza hilo ili waongoze kwa demokrasia.
“Taarifa ya utekelezwaji iwasilishwe BMT haraka iwezekanavyo,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza kuwa agizo hilo ni kwa mujibu wa sheria ya BMT namba 12 ya 1967 na marekebisho yake ya 1971 iliyotoa jukumu la baraza kusimamia chaguzi za vyama na mashirikisho.
Hivi karibuni vyama hivyo vilipokutana na serikali na BMT vilitakiwa kusimamia katiba zao kwa kutekeleza suala hilo la uchaguzi na kuwa kitu kimoja katika kuendeleza michezo nchini.
Ni vyama vichache pekee vilivyofanya uchaguzi kuanzia mwaka jana ikiwemo Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Chama cha Darts Tanzania (TADA) na vingine ambavyo bado havijawekwa wazi.

No comments:

Post a Comment