mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Wednesday, April 20, 2016

Azam yageukia kuinua filamu


Kutoka kushoto ni Muigizaji mahiri wa filamu Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’, Mkuu wa Masoko na mauzo wa Azam, Mrope Kiwanga, Msimamizi Uzalishaji wa kipindi cha Sinema Zetu Zamaradi Nzowa, Mhadhiri Msaidizi wa UDSM Issa Mbura na Meneja mipango Fatma Mohamed, wakikata keki ya uzinduzi wa project ya Kiwanda cha Filamu naTamthilia ya Tax1 itakayorushwa hewani kupitia channel 103 ya Sinema Zetu ya Azam TV ikiwa ni moja ya projekti mpya

KAMPUNI ya Azam Media kupitia chaneli yake ya sinema zetu imezindua mradi mpya wa Kiwanda cha Filamu, ambapo leo wanatarajia kufanya usaili kwa washiriki 200 ambao ni waigizaji chipukizi watakaoshiriki kwenye tamthiliya mpya ya Tax.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo jana Dar es Salaam, msimamizi mzalishaji wa Chaneli ya sinema zetu, Zamaradi Nzowa alisema Kiwanda cha Filamu ni mchakato wa kutafuta wasanii chipukizi kwa upande wa waigizaji na wapigapicha za video.
“Mradi huu ulianza tangu mwanzoni mwa Machi mwaka huu tulipowakaribisha wadau kuwa wanaweza kutumia kazi zao kupitia mitandao yetu ya kijamii na hatimaye tulipata washiriki 200, walituma kazi zao,” alisema.
Nzowa alisema lengo kuu la mradi huo ni kukuza na kuinua vipaji vya wasanii kutoka nchini ambao bado hawajapata fursa ya kuonesha kazi zao katika jamii. Alisema usaili huo utafanyika kuanzia leo kwenye fukwe za Coco, Dar es Salaam ambapo washiriki wataangaliwa vipaji vyao, na baadaye watachujwa na kubaki 20 ambao watashirikiana na wasanii wakongwe kwenye tamthilia hiyo itakayoanza kurushwa kuanzia Juni.
Aliwataja majaji katika usaili huo kuwa ni msanii Susan Humba ‘Natasha’ , na Mhadhiri msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Issa Mbura, ambao watafanya kazi ya kuchagua waigizaji bora chipukizi kisha baadaye kuwapa mafunzo kabla ya kuanza kuigiza. Naye Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Azam Media, Mgope Kiwanga aliwataka wale watakaopata nafasi hiyo kuchangamkia fursa na kuhimiza wale ambao hawatabahatika wasikate tamaa. “Hii ni fursa pekee kwa vijana wa Kitanzania kutumia nafasi hii kuonesha vipaji vyao,” alisema.

No comments:

Post a Comment