mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Monday, April 18, 2016

Chanzo cha kuua michezo Zanzibar chabainika


MKURUGENZI wa Idara ya Michezo na Utamaduni Zanzibar, Hassan Tawakal Khairalwa amesema kuwa kukosekana kwa mfumo mzuri wa usimamizi wa michezo mashuleni ndio chanzo kikuu cha kuua michezo ya elimu ya bila ya malipo.
Kauli hiyo aliitoa katika shule ya Sekondari ya Haile Selasi alipozungumza na walimu wakuu kuhusu suala zima la michezo mashuleni.
Alisema kuwa vugu vugu la michezo ya elimu bila ya malipo limeonekana kufa siku hadi siku kutokana na kutokuwepo kwa usimamizi mzuri jambo ambalo kama walimu ni lazima lisimamiwe.
Aidha alisema kuwa kuna baadhi ya shule zimekuwa zikipuuza suala la michezo huku wakiwataka wanafunzi kushiriki michezo hiyo wakati wa mashindano pekee pasipo na kufanya mazoezi.
“Kuna shule zina michezo lakini haiwafanyishi wanafunzi mazoezi na wengine huwaambia subirini katika mashindano tukacheze tufungwe turudi, alisema.
Alisema kuwa walimu hao hufanya vitendo hivyo kwa makusudi kwa madai kuwa kushiriki michezo kunawaondoshea ufahamu wanafunzi jambo ambalo sio la kweli.

No comments:

Post a Comment