mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Wednesday, April 20, 2016

Majimaji yazitangazia vita Simba, Yanga



TIMU ya Majimaji FC, imetamba kuzifunga Yanga na Simba itakapokutana nazo Uwanja wa Majimaji mjini Songea katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara hivi karibuni.
Majimaji, mabingwa wa zamani wa soka nchini ambayo waliporomoka na kupanda tena katika Ligi Kuu msimu huu, inahitaji pointi tatu ili kufikisha pointi 36, ambazo zitawaweka sehemu salama na kuepuka kushuka daraja, ambapo imebakisha michezo minne kabla ya ligi kumalizika.
Akizungumza na gazeti hili, Katibu Mkuu wa timu hiyo, John Mbano, alisema wana uhakika timu yao haitashuka daraja, kwani uwezekano wa kuzipata pointi hizo ni mkubwa kutokana na kuimarika kwa kikosi chao ambacho kipo nafasi ya tisa kati ya timu 16 kikiwa na pointi 33.
“Tunazisubiri kwa hamu kubwa Yanga na Simba kuja Ruvuma ili tulipe kisasi baada ya kutufunga idadi kubwa ya mabao kwenye mechi za mzunguko wa kwanza Uwanja wa Taifa,” alise

No comments:

Post a Comment