NYOTA ya Mtanzania Mbwana Samatta imezidi kung’ara baada ya juzi kuifungia bao timu yake ya KRC Genk, ilipoibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya KV Oostende.
Samatta, ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, alifunga bao hilo dakika ya 77 sawa na jezi yake anayovaa katika timu hiyo, ikiwa ni dakika moja baada ya kuingia akitokea benchi akichukua nafasi ya Nikolaos Karelis.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba ya Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hilo ni bao lake la tatu tangu alipojiunga na miamba hiyo mapema mwaka huu.
Katika mchezo wa juzi, mabao mengine ya KRC Genk yalifungwa na Pozuelo, T. Buffel na N. Kebano.
No comments:
Post a Comment