mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Wednesday, April 20, 2016

Kocha Simba: Viporo vimetumaliza



KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja, amesema mapumziko ya wiki tatu kupisha mechi za viporo za Yanga na Azam ndiyo yamesababisha kikosi chake kucheza chini ya kiwango na kupoteza mechi mbili mfululizo.
Jumapili Simba ilifungwa bao 1-0 na Toto Africans katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kupunguza matumaini ya ubingwa ya klabu hiyo. Kutokana na matokeo hayo Simba imebaki na pointi 57 ikishika nafasi ya pili nyuma ya Yanga inayoongoza ikiwa na pointi 59.
Yanga inazidiwa mchezo mmoja na Simba. Pia wiki iliyopita, Simba ilifungwa mabao 2-1 na Coastal Union katika Robo Fainali ya Kombe la FA na kuondoa matumaini ya mashabiki angalau kupata uwakilishi katika michuano ya kimataifa mwakani.
Akizungumza na gazeti hili, Mayanja ambaye naye aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi dakika 31 siku ya mchezo wa Toto, alisema kukaa muda mrefu bila kucheza mechi ya ushindani kumechangia kufanya vibaya kwa Simba.
Hata hivyo kocha huyo anaamini bado Simba inayo nafasi ya kufanya vizuri na kutwaa ubingwa wa msimu huu kwa kushinda mechi zilizosalia. “Mashabiki wetu wana haki ya kuchukia kwa sababu tumewaangusha, hatukucheza vizuri na tulistahili kupata matokeo hayo, tulicheza kwa kujiamini sana.
“Hatukujua kama tulikosa mechi ya ushindani kwa muda wa wiki mbili na nusu kupisha mechi za viporo za Azam na Yanga, lakini hii siyo sababu ya sisi kupoteza matumaini ya ubingwa msimu huu,” alisema Mayanja. Kocha huyo raia wa Uganda alisema hali hiyo imemhuzunisha, kwani imemvurugia rekodi yake nzuri aliyoanza nayo tangu alipoichukua timu hiyo.

No comments:

Post a Comment