mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Sunday, April 10, 2016

Ndanda Kosovo afariki dunia



MWANAMUZIKI maarufu nchini, Ndanda Kosovo `Kichaa’ amefariki dunia jana katika hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mwanamuziki mwingine kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Liva Hassan Sultan, alisema jana kuwa, Ndanda alifariki dunia jana asubuhi hospitalini hapo baada ya kulazwa kwa siku kadhaa kutokana na matatizo ya figo.
Sultan alisema kuwa Ndanda alilazwa kwa takribani siku tano kabla ya mauti kumkuta jana asubuhi na kwamba ameacha mjane na watoto wawili na msiba uko nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Alisema hii ni mara ya pili kwa Ndanda kulazwa hospitalini hapo kwani mara ya kwanza alilazwa wiki kadhaa zilizopita, lakini alitolewa baada ya kupata nafuu kabla ya kurudishwa tena siku zilizopita baada ya kuzidiwa.
Ndanda atakumbukwa kwa uhodari wake wa kutunga na kuimba, hasa kibao chao cha Wajelajela Original, ambacho alikiimba alipokuwa na kundi la FM Academia.
Kibao hicho waliimba baada ya kutoka lupango ambako waliswekwa baada ya kukamatwa na Idara ya Uhamiaji kutokana na kutokuwa na vibali va kuishi na kufanya kazi nchini.
Baadaye Ndanda alianzisha kundi lake la Stono Musica, ambalo hata hivyo hakudumu nalo sana kabla ya kwenda Marekani ambako alikaa kwa muda na kurejea nchini ambako alianzisha kundi lake la Watoto wa Tembo.

No comments:

Post a Comment