Sauce ya ndizi mzuzu na viazi vitamu
Kuandaa: dakika 5
Mapishi: dakika 10
Mapishi: dakika 10
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mahitaji
Mahitaji- Ndizi mzuzu 2
- Kiazi kitamu 1
- Mafuta ya kula (yanayotosha kukaanga, hapa nimetumia mafuta ya zaituni au olive oil)
- Chumvi
- Pilipili hoho 2
- Karoti
- Kitunguu maji 1
- Kitunguu saumu 1
- Maggi cubes (hivi ni viungo vyenye ladha mbalimbali)
Wapi kwa kupata bidhaa?
Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.
Maelekezo
Chakula hiki niliandaa kwa kukaanga, lakini pia unaweza kuoka hizi ndizi halafu ukazipika kwenye mboga za majani. Ili kuzingatia afya, hakikisha unatumia mafuta mazuri ya kupikia. Mafuta mazuri hutokana na mimea, mfano olive oil, au mafuta ya viumbe wa baharaini, mfano mafuta ya samaki wa maji baridi.- Menya ndizi na viazi. Kata vipande vya wastani na uweke pembeni vizuri.(Kwenye hatua hii, mie nililoweka viazi na ndizi kiasi kwenye mchanganyiko wa kitunguu saumu, limao na chumvi. Ni vijimambo vya kuongeza ladha, lakini si lazima sana)
- Bandika kikaangio au sufuria. Weka mafuta ya kula na acha yapate moto. Weka ndizi na viazi. Usirundike chakula ili kipate kuiva vizuri. Itachukua takribani dakika 5 hadi 7 hadi kuiva. Vikiiva weka kwenye paper towel au tishu ili mafuta yajichuje. Rudia hatua hii hadi umalize viazi na ndizi zote.
- Menya kisha kata kitunguu, karoti na pilipili hoho kwenye vipande vidogo. Menya kitunguu saumu (au kama una cha unga utaweka moja kwa moja) kisha saga ili kiwe laini.
- Bandika sufuria tofauti jikoni. Weka mafuta. Yakichemka, weka kitunguu saumu. Kisha weka kitunguu maji. Koroga hadi kilainike na kipate kubadilika rangi. Weka pilipili hoho na karoti. Ongeza chumvi. Koroga kisha funika na mfuniko mboga zipate kuiva na mvuke wake.
- Weka magi cube na viungo vyovyote unavyopendelea. Kisha koroga. Mie kwenye hii hatua niliongeza pia supu ya kuku kidogo ili kuleta ladha tamu kwenye mboga hii.
- Mboga ikiiva, weka ndizi na viazi kwenye mboga. Changanya vizuri. Acha zikae dakika 3 hadi 5 ili zipate kuingia ladha ya viungo na supu vizuri. Kisha epua.
- Tenga na ujirambe na chakula kitamu hiki.
- Unaweza kula ndizi hizi kama chakula kitamu tu, lakini pia unaweza kula na kitu kingine cha kusindikizia.
- Jirambe na ladha ya chakula kitamu.
No comments:
Post a Comment