Kuandaa: dakika 10
Mapishi: dakika 20
Mapishi: dakika 20
Mahitaji
- Nyama ya mbuzi ½ kilo
- Beef masala kijiko 1 cha chai
- Vitunguu maji 2 vikubwa
- Nyanya 2
- Mafuta kiasi
- Pilipili hoho
- Karoti 1
- Limao 1
- Pilipili mbuzi 1
- Soy sauce
Wapi kwa kupata bidhaa?
Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.
Maelekezo
- Safisha nyama weka pembeni ichuje maji. Andaa vitunguu maji menya kisha kata vipande vidogo
- Bandika sufuria jikoni. Weka mafuta ya kula. Mafuta yakipata moto, weka nyama. Kaanga hadi ianze kuwa ya kahawia, kisha weka vitunguu maji. Koroga kisha funika.
- Saga karoti, pilipili hoho na pilipili mbuzi kwa pamoja. Weka mchanganyiko kwenye nyama. Koroga kwa dakika 3. Nyama ikiwa inashika weka soy sauce kiasi kisha Koroga.
- Weka nyanya, ila ni vizuri ukizisaga kwanza. Weka chumvi, kamulia ndimu, kisha funika. Hakikisha nyama inakauka na hakuna mchuzi. Weka beef masala. Koroga mpaka iwe kavu. Kisha epua, jirambe
No comments:
Post a Comment