mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Monday, April 18, 2016

Azam leo ni leo



AZAM leo ipo Tunis, Tunisia kumenyana na Esperance ya huko katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Wawakilishi hao wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kushinda mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.
Mechi hiyo ya leo inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Olympique de Rades mjini Tunis na kocha wa timu hiyo Stewart Hall alisema timu yake iko vizuri kwa mechi hiyo.
“Timu iko vizuri, tunatarajia mchezo utakuwa mgumu hasa kwa vile tumeshinda mechi ya kwanza nyumbani hivyo tumejiandaa na kila mmoja anafahamu wajibu wake”.
Kocha Hall alifafanua kuwa wanacheza na timu bora Afrika, hivyo uwezekano mkubwa wa wapinzani wao kubadilika kwao ni mkubwa.
“Timu kubwa hizi zina mbinu nyingi kwenye mechi, unaweza kuwakuta wamebadilika kabisa mechi ijayo, lakini yote hayo tumejipanga kukabiliana nayo,” alisema.
Ikiiondosha Esperance kwenye mechi hiyo, Azam itaingia hatua ya 16 bora ambapo itacheza na timu itakayotoka kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa kabla ya kufuzu hatua ya makundi, endapo itashinda.
Pambano hilo la Azam FC linatarajia kuanza saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Mechi nyingine zitakazochezwa leo ni kati ya Stade Gabesien itakayocheza na Zanaco, Sagrada Esperanca dhidi ya Vita Club Mokanda, Medeama na El Ahly Shandy, SC Villa itacheza na Fath Union Sport, Misr Makkassa itacheza na CS Constantinois, Enppi itacheza na Mounana na Kawkab Marrakech itamenyana na Mouloudia Club D’oran.

No comments:

Post a Comment