Tambi za hiliki na sukari
Kuandaa: dakika 5
Mapishi: dakika 8
Mapishi: dakika 8
i
Mahitaji
- Tambi 500g
- Sukari vijiko 2 vikubwa
- Hiliki 3
- Mafuta ya kupikia 1/4 lita
Wapi kwa kupata bidhaa?
Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.
Maelekezo
Chakula hiki utapika katika sehemu mbili, ya kwanza ni kukaanga na ya pili ni kuchemsha. Kisha utachanganya ili kupata mchanganyiko maridhawa wa mlo kamili. Ni vizuri kama utafanya vyote wakati mmoja, ila kama huna nafasi jikoni unaweza kuanza na kimoja kisha ukamalizia na kingine.- Anza kwa kumenya hiliki, kisha hifadhi maganda.
- Toa tambi kwenye packet, kisha gawa kwenye makundi mawili – kundi moja tambi za kukaanga na lingine za kuchemsha.
- Anza kuandaa kama ilivyoelezwa hapa chini. Ni vizuri kama utafanya hizi hatua kwa pamoja ili tambi zipate kuiva kwa muda mmoja.
- Bandika sufuria au kikaango cha mafuta jikoni, acha yachemke vizuri.
- Mafuta yakishachemka, ongeza fungu moja la tambi ulizotenga (Za kukaanga). Acha kwenye mafuta kwa muda kiasi hazi zianze kubadilika rangi. Ni vizuri kama hutoacha tambi zibadilike sana rangi kuwa za brown, maana zitaungua na kutokuwa na ladha nzuri.
- Epue tambi mapema kupata rangi ya wastani. Zitakuwa zimeiva vizuri tu.
- Bandika chungu au sufuria ya maji jikoni kwa ajili ya kuandaa tambi za kuchemsha.
- Weka maganda ya hiliki kwenye maji ya moto ili kuweka harufu nzuri kwenye tambi. Baada ya dakika kama 5 unaweza kuchuja maganda ya hiliki na kubaki na maji yenye harufu ya hiliki.
- Chukua kiasi cha tambi zilizosalia, weka kwenye maji ya moto, kisha ongeza sukari na hiliki.
- Subiria tambi zichemke kutokana na muda ulioshauriwa - dakika 5 hadi 7 - ili zisiwe na kiini kigumu ndani. Hapo tambi zako zitakua zimeiva.
- Changanya tambi za kukaanga na tambi za kuchemsha pamoja. Katika hatua hii unapata mchanganyiko wa rangi tofauti za tambi, harufu nzuri ya hiliki na utamu wa sukari unamalizia.
- Usisahau kutoa maoni kama ukishapika na kuonja ladha ya chakula hiki.
No comments:
Post a Comment