mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Sunday, April 10, 2016

Uchukuzi SC yatamba kutesa Mei Mosi


Wachezaji wa timu ya Uchukuzi SC ya wanawake wakivuta kamba wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wao uliopo jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam juzi. (Picha na Cosmas Mlekani).

TIMU ya Uchukuzi SC imetamba kufanya vizuri katika mashindano ya Mei Mosi yatakayofanyika mjini Dodoma kuanzia Aprili 16 mwaka huu.
Mwenyekiti wa timu hiyo inayoundwa na wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mohamed Ally alisema timu yake itafanya vizuri katika mashindano hayo.
Ally alisema kuwa kwa sasa wako katika mazoezi makali kujiandaa na mashindano hayo, ambayo yatafikia kilele chake Mei Mosi mjini Dodoma. Alisema Uchukuzi SC ina timu za soka, netiboli, kuvuta kamba, bao, karata, riadha, baiskeli na vishale.
Alisema kuwa wana uhakika timu yao kutamba katika mashindano hayo ya Mei Mosi kutokana na kufanya maandalizi kabambe chini ya makocha wazoefu.
Aliwataja baadhi ya makocha hao kuwa ni pamoja na Kenny Mwaisabula, Robert Damian, Kingsley Malwilo na Abunu Issa, ambao wameifanya timu yao ya soka kuwa tishio kwa timu zingine.
Alisema timu zao hizo zimekuwa zikicheza mechi kadhaa za majaribio ili kuwawezesha makocha kubaini makosa na kufanya marekebisho ya mwisho kabla timu hiyo haijaondoka kwenda Dodoma.
Naye Meneja wa Uchukuzi SC, Damiani alisema kuwa timu yao inatarajia kwenda Dodoma Aprili 14 tayari kwa mashindano hayo. Alisema timu ya soka na netiboli zimefanya majaribio kadhaa ili kujiweka fiti kwa mashindano hayo, ambayo wana uhakika wa kutwaa ubingwa.

No comments:

Post a Comment