RAIS wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ravia Idarous Faina ametetea nafasi yake yaurais wa chama hicho kwa kupata asilimia 88.68 katika uchaguzi wa chama hicho uliofanyika jana visiwani Zanzibar.
Uchaguzi huo ulifanyika ukumbi wa Uwanja wa Gombani, Pemba, ambapo Ravia aliibuka kidedea kwa kupata kura 47 kati ya kura 53 zilizopigwa na kumshinda mpinzani wake Salum Bausi ambaye alipata kura sita.
Kwa upande wa Makamu wa Rais Pemba, nafasi hiyo imetetewa na Ali Mohammed Ali aliyemshinda Suweid Hamad Makame kwa kupata kura 46.
Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Suleiman Haji Hassan, alisema nafasi ya Makamu wa Rais Unguja imeenda kwa Mzee Zam Ali aliyepata 37.
Katika uchaguzi huo nafasi ya Makamu wa Rais Unguja ilikuwa na wagombea watatu, ambapo Mohammed Masoud alipata kura 11 na Ali Nassor Salum Mkweche alipata kura tano.
No comments:
Post a Comment