BEKI wa kushoto wa Simba, Mohamed Husseni ‘Tshabalala’ amesema timu yake inastahili kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kutokana na ushindani waliouonesha kwenye mechi zao.
Tshabalala amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba tangu ajiunge nayo msimu uliopita akitokea Kagera Sugar ya mkoani Kagera.
Akizungumza na gazeti hili, Tshabalala, alisema mapambano waliyoyaonesha kuanzia mwanzoni mwa msimu huu hadi sasa ni dhahiri wameonesha nia yao ya mafanikio wanayoyatafuta msimu huu, licha changamoto kubwa wanazokutana nazo kutoka kwa washindani wao kwenye ligi.
“Ukweli tumepania kuwa mabingwa msimu huu, ingawa ligi ni ngumu na ushindani ni mkubwa, lakini tutaendelea kupambana ili kufanikisha kile tulichokipanga na hilo linawezekana kutokana na ubora tuliokuwa nao hivi sasa,” alisema Tshabalala.
No comments:
Post a Comment