MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya Yanga, Paul Nonga, amesema taratibu ameanza kuzoea mfumo unaotumiwa na timu hiyo na siku si nyingi ataanza kuonesha makali yake ya kucheka na nyavu.
Nonga amekuwa katika wakati mgumu wa kugombea nafasi ya kucheza na washambuliaji wa kimataifa Amissi Tambwe raia wa Burundi na Mzimbabwe Donald Ngoma ambao wanafanya vizuri na kuwa chaguo la kwanza la kocha Hans van der Pluijm.
Akizungumza na gazeti hili Nonga, aliyeifungia timu hiyo mabao mawili yote akiyafunga kwenye mechi za Kombe la FA, alisema mwanzoni wakati anatua kwenye timu hiyo mfumo, ulikuwa ukimsumbua na kulazimika kutumia muda mwingi mazoezini ili kujifunza aweze kuendana na wenzake na anafuraha kuona ameanza kufanya vizuri na kupata nafasi japo akitokea benchi.
“Mwanzoni nilikuwa sichezi kabisa kutokana na kutouelewa vizuri mfumo ambao unatumiwa na mwalimu lakini nafurahi kuona kadri siku zinavyokwenda nimeanza kupata nafasi ya kucheza ingawa siyo kikosi cha kwanza lakini hizi dakika chache zinanitosha kuniwezesha kuzoeana na wenzangu na kufanya vizuri Yanga,” amesema Nonga.
Mshambuliaji huyo aliyewahi kutamba na klabu za Mbeya City na Mwadui FC, alisema kocha Pluijm amekuwa akimpa matumaini na kumtaka aongeze bidii ili aweze kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na uwezo wa upambanaji aliokuwa nao.
Alisema kitu kikubwa alichoambiwa kukifanyia kazi na Pluijm, ni kuzitumia vizuri nafasi anazozipata uwanjani akiweza kurekebisha hilo anaweza kuwa mshambuliaji mzuri na kuitwa hata timu ya taifa ya Tanzania Bara. Nonga ni mshambuliaji chaguo la tatu kwenye kikosi cha Yanga ambacho kina washambuliaji watano ambao ukiachana na Tmabwe na Ngoma wengine ni Malimi Busungu
No comments:
Post a Comment