mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Friday, April 22, 2016

MLO WETU LEO

Samaki wa kupaka

Haya ni mapishi mahsusi ya kuamsha vionjo vyako vya ulimi. Ladha ya nazi kwenye huyu samaki ni murua kabisa kuliwa kama mlo kamili nyumbani. Hii mboga inayofaa kuliwa na vitu tofauti, lakini mahsusi kwa wali wa nazi. Unaweza pia kula kwa vitafunwa mbalimbali kama chapati au maandazi. Kama kweli unapenda kujinoga na misosi ya ukweli, basi jaribu haya mapishi na kujiramba vizuri, hutojutia nafsi yako.

Mahitaji

  • Samaki 2
  • Nazi 1
  • Vitunguu maji 1
  • Karoti 2
  • Vitunguu swaumu 1
  • Hiliki 1
  • Pilipili mbichi 1 (kama ni mpenzi wa pilipili, siyo lazima)
  • Nyanya 3
  • Ndimu 1
  • Chumvi Kijiko 1 kikubwa
  • Bizari
  • Foil paper
  • Vibanio vya kuchomea samaki

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mie napendelea kula samaki mzima mzima bila kumkata. Huwa nahisi raha sababu naweza kumtafuna mwenyewe bila ya kuwa na kiambato kingine zaidi. Katika mapishi haya, utaelewa umuhimu wa kumla samaki mzima, maana hakuna utakachobakisha. Angalia tu usije kukwamwa na miba, maana utamu ukizidi unaweza kushangaa umemeza hadi miba ya samaki.
  • Andaa viungo vyako vyote, kisha saga nyanya, vitunguu maji, karoti, hiliki,vitunguu swaumu kwa pamoja.
  • Kuna nazi yako na uchuje tui zito.
  • Osha samaki kisha mchovye kwenye viungo.  Nyunyizia pilipili juu yake (hii si lazima kwa wale wasiokula pilipili). Ongeza chumvi na umkamulie ndimu.  Kisha acha samaki wako wakae kwa dakika kama 10 ili viungo vipate kuingia.
  • Rudia hivyo kwa idadi ya samaki ulionao.
  • Funga samaki kwenye foil. Banika au choma Samaki wako kwenye jiko la mkaa ( kama BBQ) au oven. Unaweza kuchoma kwa njia yeyote lakini nashauri kutumia jiko la mkaa pamoja na waya wa kuchomea. Weka moto mdogo sana kisha mbanike ili aweze kuiva kwa joto kiasi. Unaweza kumgeuza geuza ili aweze kuiva vizuri pande zote.
  • Anza kupika tui la nazi kwa kubandika chungu au sufuria jikoni. Koroga tui huku ukiwa unaongeza viungo ulivyosaga hapo awali - nyanya, vitunguu maji, vitunguu swaumu, hiliki, na karoti. Kisha ongeza ndimu na chumvi. Angalia usizidishe chumvi maana samaki ana chumvi pia. Usiache kukoroga ili kufanya tui kuwa laini kwa matokeo mazuri zaidi. Koroga mchanganyiko wa tui hadi likauke na kuwa kitu kimoja na viungo vyake.
  • Kama umetumia jiko la mkaa - Samaki akishaiva, mtoe kwenye foil, kisha chukua kibanio cha kukaangia samaki muweke na uanze kumnyunyuzia rojo juu yake.  Mgeuze na kuongeza rojo ya tui juu yake. Changanya vizuri hadi rojo liingie vizuri. Fanya hivi kisha muweke samaki kwenye moto mdogo ili kuhakikisha kuwa samaki, viungo na rojo vinaungana vizuri. Ukimaliza tenga samaki kwenye sahani tofauti.
  • Kama umetumia oven - Samaki akishaiva, mtoe kwenye foil, Chukua chombo (mfano sahani) kisha nyunyuzia rojo juu yake. Muweke samaki juu ya hiyo rojo na uendelee kuongeza rojo ya tui juu ya samaki wako. Changanya vizuri hadi rojo liingie vizuri. Ukishamaliza unaweza kumuweka samaki kwenye moto modogo ili kuhakikisha kuwa samaki na rojo vinaungana vizuri. Ukimaliza tenga samaki kwenye sahani tofauti.
  • Rudia hii hatua hiyo kwa samaki wote waliobaki.
  • Ukimaliza mboga yako iko tayari kuliwa. Ni vizuri ikiliwa ikiwa bado ya moto kwa kuleta ladha nzuri.
Unaweza kula mboga hii na wali, ugali, maandazi, chapati, au ukachanganya na mboga za majani.
Jirambee na ladha ya maisha..! Enjoy samaki wa kupaka.

Thursday, April 21, 2016

Diwani na Mwenyekiti Chadema Nusura Watwangane laivu Bila Gloves



Diwani wa Kata ya Isyesye, Ibrahimu Mwampwani (Chadema) na Mwenyekiti wa Mtaa wa Manga Veta, Godlove Haule (Chadema) nusura watwangane makonde mbele ya wananchi baada ya kutuhumiana kula rushwa kutoka kwa mwenye jengo la ghorofa linalodaiwa kujengwa juu ya mkondo wa maji na kusababisha mafuriko jijini Mbeya.

Sakata hilo lilitokea baada ya viongozi hao kukutana mbele ya jengo hilo wa kiwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri na wananchi wakijadiliana jinsi yakukabiliana natatizo la mafuriko yanayotokea mara kwa mara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha .

Akizungumziatukiohilo, John Steven mkazi wa Isyesye alisema kuwa walifika katika eneo hilo kwalengo la kupata suluhisho la mafuriko na ubovu wa miundombinu ya barabara kwani limekuwa nitatizo kubwa katika eneo hilo ambapo asilimia kubwa ya wananchi wanaokaa eneo hilo wameyafungia ndani magari yao kutokana na kushindwa kupita.

 “Hawa ni viongozi wetu na ndiyo wanashughulikia suala hili lakini cha kushangaza inaonyesha baadhi yao wanamaslahi binafsi hadi wanafikia hatua kama hii yakurushiana maneno na kutaka kupigana wakati tunaoumia ni sisi wananchi wa kawaida kutokana na mafuriko,” alisema

Haule alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema kuwa ni kweli walitaka kurushiana makonde kutoka na na baadhi ya viongozi wa kisiasa wamekuwa wakifanya kazi kwa maslahi yao kwani tatizo la jengo hilo la ghorofani la muda mrefu lakini hakuna hatua inayochukuliwa.

Kwa upande wake Mwampwani alipoulizwa kuhusiana natukio hilo alisema kuwa ni kweli hali hiyo ilikuwepo ni baada ya kuambiwa na mwenyekiti huyo kuwa inawezekana atakuwa amechukua rushwa kwa mmilikiwa jengo hilo.

WANAFUNI WAKIWA MAKINI KUANDIKA WANACHOFUNDISHWA JUU YA SEMINA YA UJASIRIAMALI

Semina ya ujasiriamali imeendelea katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha  huku mada mbalimbali zikiwasilishwa na wakufunzi wa chuo hicho.

Muwasilisha  mada wa kwanza Bwana Thomas Majaliwa Ishengoma amesema biashara nyingi zinashindwa kudumu kutokana na ukosefu wa elimu muhimu katika biashara sanjari na kufanya biashara moja huku akiwashauri wajasiriamali na wanaohitaji kuwa wajasiriamali kuwa na mazoea ya kujaribu biashara zote.

Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Thomas Majaliwa Ishengoma akiwasilisha mada isemayo Ujasiriamali  katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Aidha amesema ili biashara idumu mjasiriamali anapaswa kufanya mambo ambayo yatainua biashara yake ikiwa ni pamoja na kutengeneza bidhaa yenye thamani kwa wateja sanjari na kuwa na nguvu ya kifedha.

Kwa upande wake mtoa mada wa pili Bwana Elifuraha Samboto ameelezea mambo muhimu ya mkakati wa kimasoko kuwa ni katika kuwalipa na kuwajali wafanyakazi, na kufanya utafiti wa kibiashara na kuwajali wateja.
Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Elifuraha Samboto akiwasilisha mada ya isemayo mkakati wa kukuza soko la biashara katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Hata hivyo amesema kuwa mjasiriamali ili aweze kuendelea na kufikia malengo yake anapaswa kuepukana na uvivu, wivu, Chuki, pamoja na hasira .

Naye mtoa mada wa tatu Bwana Elihuruma Chao ameelezea kanuni muhimu za mjasiriamali kuwa ni lazima aipende kazi anayofanya, uwezo wa kusimamia kazi, kuthubutu kufanya kile ambacho amekusudia pamoja na kuwa na nidhamu katika biashara anayoifanya.

Makamu mkuu  wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Elihuruma chao akiwasilisha mada ya isemayo maadili ya biashara katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Aidha amesema ili mjasiriamali aendelee mbele lazima afuate maadili ya biashara ambayo ni kuheshimu hadhi ya kila mfanyakazi, kuwa mwaminifu katika kutoa ahadi za kweli kwa wateja wake na kuendeleza mahusiano mazuri  kwa wateja wake.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakisikiliza pamoja na kuandi kakile kinachowasilishwa  na wakufunzi wa chuo hicho katika semina ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Semina ya ujasiriamali imeanza siku ya Jumatatu ambapo mpaka sasa mada tisa zimekwisha wasilishwa  na inatarajia kufikia kikomo hapo kesho.

Wednesday, April 20, 2016

Dk Msolla ataja kilichoiua Azam


Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Dk Mshindo Msolla

KOCHA wa zamani wa timu ya soka ya taifa, ‘Taifa Stars’, Dk Mshindo Msolla amesema maandalizi ya zimamoto ndiyo yaliyoiondosha Azam kwenye michuano ya kimataifa juzi.
Azam iliyokuwa ikishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC), juzi ilitupwa nje ya michuano hiyo baada ya kufungwa mabao 3-0 na Esperance ya Tunisia katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili iliyochezwa mjini Tunis.
Matokeo hayo yanaifanya Azam itolewe kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya kushinda mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyofanyika Dar es Salaam Aprili 10, mwaka huu. Akizungumza jana, Dk Msolla alisema Azam haikuwa na maandalizi ya kutosha, ilicheza mechi chache za ligi ndipo ikaenda kucheza na Esperance wakati wapinzani wao walijiandaa muda mrefu.
“Maandalizi ya zimamoto yaliiponza Azam, wenzetu walijiandaa muda mrefu na walijua kwamba wanacheza na walijua kwamba wanacheza na timu iliyowafunga mechi ya kwanza,” alisema. Dk Msolla alisema kingine kilichoiponza Azam ni kukosekana umakini kwa wachezaji wa timu hiyo, jambo ambalo lilifanya kufungwa mabao mepesi. “Timu haikuwa na mawasiliano, ikafungwa mabao mepesi, wachezaji walimuacha Bocco (John) peke yake muda mrefu, hivyo mabeki wa Esperance walipenya wanavyotaka,” alisema.
Naye Grace Mkojera anaripoti kuwa nahodha msaidizi wa Azam FC, Himid Mao, amewataka mashabiki wao kutokata tamaa baada ya kutolewa na Esperance ya Tunisia.
Kwa mujibu wa tovuti ya Azam FC, Mao aliyeingia dakika ya 79 katika mchezo huo kuchukua nafasi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’, alisema kwa sasa nguvu zao zote wanahamishia katika Ligi Kuu soka Tanzania Bara na Kombe la FA, akiwaahidi kuwa watapambana kuchukua makombe yote hayo.
“Matokeo yamewasikitisha watu wengi hasa sisi wachezaji, lakini wanatakiwa wajue Azam FC ni timu changa sana na kwa sasa tunapiga hatua kubwa, lakini hii haitufanyi tuvimbe vichwa kwani bado tuna deni. “Hivyo nafikiri inabidi tufanye kitu kikubwa zaidi kuweza kusogea na wao mashabiki waendelee kutupa sapoti, bado ligi ipo, FA ipo tutajitahidi kuweza kuchukua makombe yote hayo. “Mchezo ulikuwa mgumu, ulikuwa mzuri dakika 45 za kipindi cha kwanza, tuliweza kuikabili presha ya ugenini na hatukuweza kuruhusu bao, kipindi cha pili naona wenzetu walirudi na nguvu zaidi, tulizuia wakapata mabao kutokana na labda makosa yetu ya kiuchezaji wakaweza kushinda,” alisema.
Mao alisema ni hatua kubwa wamefikia mpaka sasa hadi kutolewa hasa kutokana na ukubwa wa wapinzani wao waliokuwa wakipambana nao.
“Unajua mpira ni mchezo wa makosa na katika mpira unajifunza kila siku iwe unacheza mechi au unafanya mazoezi, ukiiangalia Esperance ipo kwenye nafasi za juu Afrika (nafasi ya tatu), ni timu nzuri ni timu bora, sisi kufika hapa na namna tulivyocheza na hatua kubwa sana tumefika, lakini ni changamoto kwetu inabidi tuchukue kitu ambacho kitatusaidia kufanikiwa katika mashindano yanayokuja mbele,” alisema.
Azam FC iliyopanda Ligi Kuu miaka minane iliyopita, msimu huu ilikuwa ikishiriki kwa mara ya nne michuano ya Afrika hadi inafika raundi hiyo ilifanikiwa kuwatoa Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 7-3.

Haya Ndio Madhara Sita ya Kutoa Mimba Kwa Mwanamke.....



Kutoa mimba ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.

Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba.

Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?

Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu isipokuepo ndio basi tena.

Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…

Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi mimba. Vifo hivyo vimekua vikisababishwa na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%, mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.

Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka hii ya karibuni wanawake wengi ambao wanalia kutopata watoto wana historia za kutoa mimba miaka iliyopita, na wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa maamuzi yao. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba kutoka.

Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko wa uzazi una utando maalumu amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi. Lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija husika tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..

Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya mda husika akibeba mimba nyingine. Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu  na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili maisha yao yote.

Kansa ya mlango wa uzazi
Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.

Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…

Mwisho
kumbuka kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimba...maumivu ya kukosa mtoto ni makali sana kuliko aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Hawa wanaozaa sasa hivi unawaona malaya ipo siku utawakumbuka utakapo ambiwa na daktari kwamba labda itokee miujiza ndo utazaa.Kama hutaki mimba tumia njia za uzazi wa mpango kwani kuendelea kutoa mimba kutakupa adhabu ya kukosa mtoto ambayo adhabu hiyo utaitumikia maisha yako yote..

Wastara Afunguka, Asema kuvunjika kwa ndoa yake na mbunge Sadifa kumempa Amani



Msanii wa filamu Wastara Juma amefunguka na kuzungumzia kuvunjika kwa ndoa yake na Mbunge wa Donge kupitia CCM Sadifa Khamis Juma ambayo imeduku kwa kakribani miezi 3.

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Wastara amesema mahusiano ya mapenzi ni kama mtu anavyoishi na rafiki yake, mkizinguana maachana.

“Binafsi kwa sababu ni muda mchache naumia kuwakarahisha mashabiki wangu kwa sababu hawamchukulii Wastara katika stori hizo au katika muonekano huo,” alisema Wastara. Lakini kwa upande wangu naona ni bora zaidi nilivyotoka mapema kwa sababu pengine ingeniathiri nikashindwa kufanya kazi zangu na kulea wanangu,”

Wastara alisema hawezi kuzungumzia chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake kwa kuwa yale ni maisha yake ya ndani.

Pia Wastara amesema bado umri wake unamruhusu kuingia tena kwenye mahusiano, ukifika wakati amempata mtu sahihi ataolewa tena.

SIMANZI: Msanii Bongo Muvi Afariki Dunia Akijifungua Hospitalini



Ni simanzi! Nyota ya msanii Leila Gabriel ‘Lissa’ ambayo ndiyo kwanza ilikuwa imeanza kuchomoza kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, ilizimika ghafla mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya msanii huyo kupoteza maisha muda mfupi baada ya kujifungua kwenye Hospitali ya St. Benard, Kariakoo jijini Dar es Salaam.