mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Wednesday, May 4, 2016

Taasisi ya Misaada ya Kijamii ya Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangalla Yajitolea Kumsomesha Getrude Clement


Kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa kizazi cha miaka ijayo, Taasisi ya Misaada ya Kijamii ya Hamisi Kigwangalla iliyoanzishwa na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla imejitolea kumlipia ada Getrude Clement kwa masomo yake ya kidato cha tano na sita. Uamuzi huo wa kumsomesha Getrude umekuja baada ya jana kukaribishwa kuongea kwenye kikao cha wabunge...

Polisi Yaua Majambazi Wanne Katika Mapango ya Amboni Tanga


Watu wanne wameuawa katika mapambano na polisi yaliyotokea kwenye mapango ya Amboni mjini Tamga, eneo ambalo polisi mmoja aliuawa Februari mwaka jana katika tukio lililohusishwa na ugaidi. Katika tukio hilo la Februari mwaka jana, polisi walilazimika kuomba msaada wa askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) kukabiliana na watu waliokuwa wamejificha kwenye mapango hayo na kupiga kambi hapo hadi walipokisambaratisha...

WANAMGAMBO WA KIISLAM WATISHIA KUWAUA MATEKA 3 UFILIPINO


Rais wa Ufilipino, Benigno Aquino katika kambi ya jeshi la anga, Angeles city, Pampanga DIsemba 21,2015.
Rais wa Ufilipino, Benigno Aquino katika kambi ya jeshi la anga, Angeles city, Pampanga DIsemba 21,2015.
Na RFI
Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Abu Sayyaf limerusha hewani Jumanne hii video inayowaonyesha mateka watatu, kutoka Canada, Norway na Ufilipino, na kutishia kuwaua, wiki mmoja baada ya kumua raia moja wa Canada aliyetekwa nyara pamoja nao.
Katika video hiyo, iliyorushwa Jumanne hii kwenye YouTube,mateka hao watatu tatu, kutoka Canada Robert Hall, Norway Kjartan Sekkingstad, na Ufilipino Marites Flor, rafiki wa Bw Hall, wametoa wito kwa serikali za Canada na Ufilipino, wakiomba "kutekeleza madai ya kundi hilo", shirika maalum katika ufuatiliaji wa vyombo vya habari vya jihadi SITE, limearifu.
Mateka hao wameonekana wakikaa chini, nyuma ya shamba la linaloonekana kuwa la nazi, chini ya ulinzi wa watu sita wenye silaha wakisimama nyuma yao.
Mateka kutoka Canada, Robert Hall, anasema watekaji nyara wamemuamuru kuomba serikali ya Canada na "kutekeleza" mahitaji yao, bila kuyabainisha.
Mateka kutoka Norway, Kjartan Sekkingstad, amesisitiza kwamba kama "madai hayo hayatotekelezwa, tutauawa siku chache kama rafiki yetu John."
Mmoja wa watekaji nyara ameonya serikali ya Ufilipino naupata "somo" katika mauaji ya John Ridsdel na kuepukakuchelewa katika mazungumzo hayo.
Kundi hili wanamgambo wa Kiislamu la Abu Sayyaf lilitangaza wiki iliyopita kuwa lilimuua mateka kutoka Canada John Ridsdel, baada ya kumalizika kwa muda uliyotolewa Aprili 25, kwa kutoa fidia ili aweze kuachiliwa huru.
Mateka hawa watatu walitekwa nyara mwishoni mwa mwezi Septemba pamoja na John Ridsdel, walipokuwa katika mgahawa kusini mwa Ufilipino.
Rais Ufilipino Benigno Aquino aliahidi mwishoni mwa mwezi Aprili kuanzisha mashambulizi ya kijeshi kwa lengo la "kutokomeza shughuli za kihalifu" za kundi la Abu Sayyaf na kuonya kuwa serikali haitojadiliana na shirika inalolichukulia kama la kigaidi.
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau pia ametupilia mbali mazungumzo yoyote na watekaji nyara.
Bw Aquino alisema kuwa mateka wanashikiliwa katika kisiwa cha Jolo, ngome kuu ya jadiya kundi la Abu Sayyaf, zaidi ya kilomita elfu kusini mwa Manila.

MAMAKE TUPAC SHAKUR AAGA DU!


Afeni Shakur
Mama yake aliyekuwa mwanamuziki wa mtindo wa Rap Tupac Shakur ,Afeni Shakur amefariki akiwa na umri wa miaka 69.
Kaunti ya California imethibitisha kifo chake kupitia ujumbe wa Twitter.Hakuna maelezo zaidi yaliotolewa.
Alice Faye Williams,alibadilisha jina lake na kuitwa Shakur akiwa mtu mzima alipokuwa mwanaharakati wa kisiasa na kujiunga na vuguvugu la Black Panther.
Alikuwa na mimba ya Tupac mwaka 1971 alipokamatwa na kufungwa jela pamoja na wanachama wengine wa vuguvugu hilo na kukabiliwa na mashtaka ya njama ambayo baadaye yalitupiliwa mbali.
Shakur alikuwa kigezo kizuri cha muziki wa mwanawe na alisimamia muziko wake baada ya kifo chake.
Tupac Shakur
Tupac Shakur alifariki mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 25,baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika gari moja.
Mauaji yake bado hayajapata ufafanuzi.

Tuesday, May 3, 2016

LAPF YAKABIDHI MADAWATI YA SHILINGI MILIONI KUMI KWA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI


JAMES1
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Salum Ally Hapi (wa pili kushoto) akimshukuru Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF James Mlowe mara baada ya kupokea msaada wa madawati 124 kwa ajili ya Shule ya Msingi Nakasangwe iliyopo Kata ya Wazo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.  Kulia ni Ofisa Elimu Msingi Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni.
JAMES2
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Salum Ally Hapi (kulia) akipokea msaada wa madawati 124 kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa mfuko wa pensheni wa LAPF, James Mlowe kwa ajili ya shule za Serikali Manispaa ya Kinondoni. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Ofisa Elimu Msingi  Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni. 
JAMES3
Mkuu wa Wilayaya Kinondoni, Salum  Ally Hapi akizungumza katika hafla ya kupokea madawati 124 yaliyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF jijini Dar es Salaam juzi.
JAMES4
Kaimu Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa  LAPF Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Yesaya Mwakifulefule akizungumza katika hafla hiyo.
JAMES5
Meneja Masoko na Mawasiliano wa  Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Bw. James Mlowe akizungumza katika hafla hiyo.(P.T)

Monday, May 2, 2016

WAMBURA-SITAKUBALI RASILIMALI ZA TAIFA HILI ZICHEZEWE.


a1Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(wa pili kushoto) akipata msaada wakati akiteremka toka katika kiwanja cha shirika la utangazaji Tanzania(TBC) kulipojengwa nyumba za watumishi wa shirika hilo ambazo hazijaisha kwa zaidi ya miaka 20 sasa na kutoa maagizo ya kumalizia nyumba hizo au kuwapa Halmashauri ya Kisarawe ili wajenge Hostel za wanafunzi.(Picha na Daudi Manongi-WHUSM)
a2Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola akitoa mrejesho kuhusu nyumba za shirika hilo zilizo kisarawe mkoani Pwani ikiwemo kukamilisha upatikanaji wa hati  wa eneo hilo na kuliendeleza ili watumishi wa TBC wa kisarawe walitumie kwa makazi.
a3Kaimu mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi.Nahya Mansour(wa kwanza kushoto) akimskiliza Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(hayupo pichani) wakati akitoa maagizo juu ya nyumba za Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) zilizopo eneo la kimani Kisarawe mkoa wa  Pwani.wengine pichani ni Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Kisarawe Bi.Mwanamvua Mrindoko(wa pili kushoto).
a4Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola wakati alipofanya ziara katika nyumba za shirika hilo zilizopo kisarawe mkoani Pwani.
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura ametoa wito kwa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kutunza Rasilimali za Taifa kwa kuwa ni pesa inayotoka na jasho la mlipa Kodi na ingeweza kutumika kwa kazi nyingine kuliko uharibifu unaofanyika katika kiwanja cha Shirika hilo kilicho eneo la kimani ambako zimejengwa nyumba za wafanyakazi wa shirika hilo waliopo kisarawe mkoa wa Pwani.
Mhe.Wambura alisema hayo wakati alipotembelea eneo la shirika hilo ili kupata mrejesho wa maagizo aliyotoa wakati alipofanya ziara ya kwanza katika eneo hilo Aprili 2011 mwaka huu na kuipatia siku saba Idara ya Miradi ya shirika hilo ikishirikiana na Halmashauri ya kisarawe kufanikisha upatikanaji wa hati miliki ya eneo hilo la makazi ya wafanyakazi wa shirika hilo.
“Taratibu za Kisarawe za upatikanaji wa hati zimekamilika na sasa wamepeleka ile Rasimu kwa kamishna wa hati kanda ya mashariki ,na maelezo tumeyaskia kwamba kulikuwa na kupishana katika uaandaaji wa hati ndo maana ikachelewa lakini kwa sasa hivi bado tunaitaji kulinda rasilimali za Taifa.Tunaitaji kuzuia uharibifu”,Alisema Mhe Wambura.
Aidha Mhe Wambura ametoa maagizo kwa shirika hilo kuangalia uwezekano wa kuendeleza makazi hayo kwa kuwa mpaka sasa imepita miaka 20 eneo hilo halijaendelezwa na shirika hilo au kufanyiwa uwekezaji wowote au wakabidhi eneo hilo kwa halmashauri ya kisarawe ili wajenge hostel za wanafunzi na kuongeza kwamba yeye hatakubali eneo hilo lipotee kwa uharibifu kwa wananchi  kubomoa nondo na kuuza kama vyuma chakavu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola alimwahidi waziri huyo kuwa watahakikisha kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 suala hilo linashughulikiwa  na kudai kwamba mara nyingi wanaweka pesa ya ukarabati lakini inakatwa lakini wataanza ukarabati kwa awamu kwa mikoa ya Arusha na Mwanza na makao makuu kwa hiyo hata izi za kisarawe zitakarabatiwa mara moja.

Haya Hapa Matokeo ya Simba na Azam Yaliyofanya Mashabiki wa Yanga Waendelee Kuchekelea Kileleni...



Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo Mei 1 2016 kwa mchezo kati ya Simba dhidi ya Azam FC kuchezwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huu ni mchezo wa 26 kwa vilabu vyote na ulikuwa mchezo muhimu kwa kila klabu hili kujiweka pazuri katika nafasi ya kuwania ubingwa.

Azam FC kabla ya mchezo dhidi ya Simba kumalizika kwa sare ya 0-0 walikuwa na point 58 wakiwa nafasi ya pili ya Ligi, wakati Simba walikuwa nafasi ya tatu wakiwa na point 57 wakiongozwa na Yanga ambao wapo kileleni wakiwa na point 65 na michezo 26. Sare ya mchezo huu ilikuwa ni furaha kwa Yanga ambao wameongeza tofauti ya point kwa Azam FC na Simba.

Kwa idadi ya mechi Simba na Azam FC huu ulikuwa ni mchezo muhimu kwao kuhakikisha wanapata point tatu ili kuweza kupunguza tofauti yao ya point na Yanga wanaoongoza Ligi wakiwa na tofauti ya point sita na Azam FC anayefuatia, umuhimu wa mchezo kwa pande zote mbili ndio ulifanya mchezo kuwa na tension kubwa kitu ambacho kilifanya wachezaji wa pande zote kukosa magoli ya wazi wakati mwingine.