Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Salum Ally Hapi (wa pili kushoto) akimshukuru Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF James Mlowe mara baada ya kupokea msaada wa madawati 124 kwa ajili ya Shule ya Msingi Nakasangwe iliyopo Kata ya Wazo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Ofisa Elimu Msingi Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Salum Ally Hapi (kulia) akipokea msaada wa madawati 124 kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa mfuko wa pensheni wa LAPF, James Mlowe kwa ajili ya shule za Serikali Manispaa ya Kinondoni. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Ofisa Elimu Msingi Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni.
Mkuu wa Wilayaya Kinondoni, Salum Ally Hapi akizungumza katika hafla ya kupokea madawati 124 yaliyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF jijini Dar es Salaam juzi.
Kaimu Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Yesaya Mwakifulefule akizungumza katika hafla hiyo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Bw. James Mlowe akizungumza katika hafla hiyo.(P.T)
No comments:
Post a Comment