IKIWA ni siku tano kupita baada ya mabasi ya mwendo kasi kuanza kusafirisha abiria katika Jiji la Dar es Salaam, hali ya vituo vyake inatisha, anaandika Happiness Lidwino.
Baadhi ya vituo hivyo vinatoa harufu kali, vimeenea mikojo, kinyesi na takataka ngumu ambapo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na manispaa husika vimedai kutohusika na usafi wake.
Miongoni mwa vituo alivyotembelea mwandishi wa habari hii ni pamoja na Moroco (Kinondoni), Kinondoni B, Manyanya na Kimara Baruti ambapo vituo hivyo vimekuwa na hali inayotia shaka usalama wa abiria wanaotumia vituo hivyo kusubiri usafiri.
Gatson Makwembe, Msemaji wa Jiji alipoulizwa kuhusu ufuatiliaji wa usafi kwenye vituo hivyo baada ya hali kuwa mbaya, amedai jiji halihusiki.
“Mimi siwezi kuzungumzia suala hilo kwani sisi halituhusu labda uwatafute Dart au Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni,” amesema Makwembe.
Sebastian Mhowera, Ofisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni alipoulizwa, alidai kazi ya Manispaa ya Kinondoni ni kusimamia usafi wa barabarani pekee.
“Sisi kazi yetu ni kusimamia usafi barabarani ndani ya manspaa hii na sio uchafu uliopo ndani ya vituo vya mabasi ya UDA. Siwezi kuzungumzia uchafu uliopo kwenye nyumba ya jirani,” amesema.
Alipotafutwa William Gatambi, Msemaji wa Kampuni ya Dart inayosimamia UDA hakupatikana kujibu aliye na dhamana ya kufanya usafi kwenye vituo hivyo.
Hali ya wasiwasi inaendelea kutawala kwa wananchi kutokana na vituo hivyo kuwa na hali mbaya, kukosa ulinzi na hata kugeuka kuwa maeneo ya vibaka, mateja na watoto wa mitaani kupata hifadhi ya usingizi.
Kituo cha Kimara Baruti kimekuwa na mlundikano mkubwa wa watu, harufu mbaya inayotokana na kinyesi, mkojo huku mwingine ukiwa umefungwa kwenye chupa za maji na kutupwa hovyo. Uchafu wa kituo hicho unafanana na vituo vingine.
John Mgonja, mmoja wa abiria aliyekuwa akisubiri usafiri katika Kituo cha Moroco ameeleza kushangazwa na huduma mbovu za vituo hivyo.
“Kwanini vituo havina ulinzi, hakuna maji, sakafu chafu, taka ngumu kila mahali na harufu mbaya mpaka imekuwa kero.
“Sijui sisi tuna tatizo gani, hivi haya mambo yote hayakuwa kwenye mpango wao. Wao wanachojua ni kukusanya fedha kwa ajili ya nauli tu?” amehoji Mgonja.
Amesema, watu wanalazimika kufanya hivyo kwa kuwa, kama amebanwa na haja na vyoo vipo kwake anaona ni bora kikudhi haja yake kwanza mengine mbele kwa mbele.
“Sasa kama umefika hapa na umebanwa kwanini usijisaidie, lakini hata kama utaacha vyoo vichafu nani atakukamata? Hakuna mlinzi na hakuna usalama wowote,” amesema.

No comments:
Post a Comment