Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dodoma Bw. Mchenya John akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge (hawapo pichani) kabla ya Uchaguzi wa Viongozi wa TUGHE tawi la Bunge uliofanyika mapema wiki hii Mkoani Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi hiyo Bibi. Emma Lyimo.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Bunge Bw. Abdallah Hancha (wa kwanza kulia) akitoa neno la shukrani kwa wafanyakazi wenzie wa Ofisi ya Bunge kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa TUGHE uliofanyika mapema wiki hii Mkoani Dodoma. Walioambatana naye ni wajumbe wa Kamati Kuu ya TUGHE tawi la Bunge.
No comments:
Post a Comment