mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Monday, May 9, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA JENGO LA KITEGAUCHUMI LA MFUKO WA PENSHENI PPF JIJINI ARUSHA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akikata utepe kuzindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016. Wa pili (kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama, (kushoto) ni Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro (wa kwanza kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Ramadhan Kijjah, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango. Picha zote na Mafoto Blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la uzinduai wa Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.
Jengo hilo lililozinduliwa leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akihutubia wakazi wa arusha na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati alipozindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.
Sehemu ya wadau kutoka NSSF waliohudhuria uzinduzi huo wa wenzao wa PPF.
Sehemu ya wadau wakimsikiliza Mhe. Rais Dkt. Magufuli.....
Baadhi ya wafanyakazi wa PPF Kanda yas Arusha wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
Sehemu ya wananchi wa Jiji la Arusha wakimsikiliza Mhe. Rais Dkt. Magufuli.....
Wananchi wakimshangilia Mhe Rais wakati akihutubia.....
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mhe Rais.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni PPF na Wakurugenzi wa Mfuko wa huo wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
Baadhi ya viongozi na wadau wa Mfuko huo na Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro (kushoto) wakimsikiliza Mhe Rais.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PPF, Ramadhan Kijjah, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na baadhi ya Wadau wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
Wakifurahia baada ya uzinduzi huo....
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Meneja wa PPF Kanda ya Arusha, Onesmo Ruhasha, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
Viongozi wakiwa meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa
Wadau wakiimba wimbo wa Taifa
Wadau wakiimba wimbo wa Taifa

Kipaumbele chetu ni kuboresha reli ya TAZARA- Balozi Kijazi

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI, ENG. JOHN WILLIAM KIJAZI AFUNGUA MKUTANO  WA WATAALAM KUTOKA NCHI YA CHINA, TANZANIA NA ZAMBIA WA KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA UTENDAJI WA SHIRIKA LA RELI LA TANZANIA NA ZAMBIA (TAZARA) KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA MWL. JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leonard Chamuriho (kulia), akimkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi kwenye Jengo la Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere, wakati alipofika kufungua Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA).
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi (kushoto), akisalimiana na ujumbe kutoka Nchini China ambao wanahudhuria  Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere. Kushoto kwake ni Balozi wa China Nchini Dkt. LU Youqing.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi (kulia), akisalimiana na ujumbe kutoka Nchini Zambia ambao wanahudhuria  Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leornard Chamuriho (kulia), akitoa hotuba yake kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere.
 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi, akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku nne unaozikutanisha Nchi Tatu China, Tanzania na Zambia kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi (wa nne kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
SERIKALI  imesema iko tayari kuboresha reli ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA) ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi kwani ni jambo la msingi na itashirikiana na nchi za Zambia na China ili kufanikisha azma hiyo. 

Akizungumza  leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu Kiongozi,  Balozi  John Kijazi wakati akizindua kikao kazi kilicho shirikisha nchi tatu ambazo ni  Tanzania, Zambia na China kuhusu maboresho ya kiutendaji ya reli ya TAZARA.

“Kipaumbele chetu ni kuboresha reli ya TAZARA ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi, kikao hiki kitajadili kwa kina changamoto mbalimbali zinazoikabili reli hii, pamoja na fursa zilizopo na namna ya kutatua changamoto hizo ili kufufua uchumi wetu kupitia reli ya TAZARA” amesema Balozi Kijazi.

Balozi Kijazi amesema kwa muda sasa reli hii imekua ikifanya kazi bila ufanisi kutokana na sababu mbalimbali licha ya kuwa kiwango cha mizigo kutoka bandari ya Dar es salaam kimeongezeka kutoka tani milioni  6 mwaka 2006 hadi kufikia tani milioni 15 mwaka 2015, reli ya TAZARA imeshindwa kuwa na uwezo  wa kusaidia kusafirisha mizigo hiyo, ambapo mwaka kila mwaka uwezo wake unashuka kutoka kusafirisha mizigo tani 601,229 mwaka 2005/2006 hadi tani 87,860 kwa mawaka 2014/2015.

Vile vile, licha ya kuwa nchi za Zambia  na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimeongeza uzalishaji wa shaba  bado TAZARA haikuwa na uwezo wa kuhudumia ama kusafirisha shaba hiyo, utendaji huu wa kiwango cha chini lazima ubadilike. 

Aidha, Serikali imesema ina ya dhati ya kuibadilisha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati, na yenye viwanda, kwa kujua kuwa uanzishwaji mzuri wa mtandao wa miundombinu hasa reli, barabara, usafiri wa anga, usafiri wa majini ni chanzo muhimu ya kutimiza azma hiyo.

Kwa upande wake, Katibu wa Baraza la Mawaziri la Zambia Dkt. Rowland Msiska amesema kuna haja kubwa ya kuboresha reli ya TAZARA kwa kuwa reli hiyo ina msaada mkubwa kiuchumi si tu kwa nchi za Tanzania, Zambia na China bali hata nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya  Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.

Aidha, amesema kuna faida nyingi za kuboresha reli ya TAZARA ikiwemo ya gharama nafuu. Usafirishaji mizigo kwa njia ya reli ni wa gharama nafuu kuliko barabara kwani inagharimu senti 5 kwa tani moja kwa umbali wa kilometa moja, huku gharama za usafirishaji kwa barabara ikiwa ni senti 12 kwa tani moja kwa umbali wa kilometa moja.

Naye, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Biashara ya China, Bwana. Liu Junfeng amesema Serikali yake  itaendelea kushirikiana na nchi za Tanzania na Zambia ili kuboresha utendaji wa reli hiyo, huku akisisitiza uhusiano wa nchi hizi tatu umeendelea kuimarika  na unazalisha fursa nyingine za ushirikiano.

Reli ya TAZARA ilijengwa mwaka 1970 hadi 1976 kwa msaada wa Jamhuri ya watu wa China kama zawadi kwa mataifa ya Tanzania na Zambia, kwa lengo la kusaidiza kuongeza njia za usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment