mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Sunday, May 29, 2016

Benki ya Dunia yaionya Tanzania Kuhusu Kuitegemea China Kimisaada


Taarifa za hivi karibuni kutoka katika serikali ya China kuwa Tanzania itapewa kiasi kikubwa cha fedha cha dola bilioni 20 ambazo China imezitenga kwa ajili ya kuzisaidia nchi za Afrika kufanya mapinduzi ya kiuchumi, inaonyesha ushirikiano mkubwa uliopo kati ya nchi hizi mbili.

Benki ya Dunia imeonya kuwa, kuongezeka kwa ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na China kunaweza kuathiriwa na kushindwa kukua kwa Beijing.

China ni moja kati ya wabia wakubwa wa biashara na Tanzania na hutoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na pia imewekeza nchini. Mwaka 2014 inakaririwa kuwa thamani biashara ya Sino-Tanzania iliongezeka thamani hadi kufikia dola bilioni 2.6 kutoka kiwango kidogo kilichokuwepo mwaka 2000.

Katibu Mkuu katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Adelhelm Meru, alisema Tanzania inatumia nafasi ya mapinduzi ya viwanda China kwa kuhakikisha uwekezaji unafanyika kwenye vitu vitakavyoisaidia nchi.

Aidha aliendelea kueleza kuwa ifikapo mwaka 2020 sekta ya viwanda itakuwa inachangia asilimia 15 ya pato la taifa.



Katika ripoti ya uchumi nchini Tanzania yenye jina, The Road Less Travelled: Unleashing Public-Private Partnerships in Tanzania, Benki ya Dunia ilibaini kuwa kwa miaka ya hivi karibuni uchumi wa China umekuwa ukikua kwa kasi ndogo. Hili ni onyo kwa Tanzania ambayo ushirika wake na Beijing umekuwa ukizidi kila iitwapo leo.

Fedha za China katika miradi ya maendeleo ya Tanzania zimezidi kuongozeka kila baada ya mwaka ikiwa ni pamoja na dola bilioni 1.2, 2013/14-2014/15 kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar es Salaam. Ripoti ya iwekezaji wa China nchini Tanzania imeongezeka maradufu, unakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 60 kwa mwaka 2013

Kuyumba kwa uchumi wa China kuna weka katika mashaka uchumi wa Tanzania ambapo unategemea sana uwekezaji toka China. Benki ya Dunia ilieleza kuwa kuyumba kidogo kwa uchumi wa China kunaweza kutaiathiri tanzania moja kwa moja au vingine kupitia uwekezaji.

China imechaangia asilimia 10 ya bidhaa zote zinazotolewa nje ya nchi na ni nchi ya tatu kwa kuchukua bidhaa baada ya India na Afrika Kusini.

Chabzo: Swahili times

No comments:

Post a Comment