Hamisi Maduka Kaimu mwenyekiti wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alisistiza ulipaji wa fidia za Ardhi uzingatie uhalisia wa thamani ya eneo husika.
Abdallah Moto mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake kwa Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 kuhusu suala la kupewa kipaumbele utoaji wa hati miliki kwa wanavijiji.
Shakira Masudi mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alitaka Sera itambue wamiliki wa Ardhi wa maeneo wa muda mrefu katika kutoa Hati.
Mwl. Hadija Nyembo mkuu wa wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora.
Hanifa Selengu Mkuu wa wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la ukusanyaji wa maoni na kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kuiboresha. Zoezi hilo limeanza Mwaka huu wa 2016 ambapo linashirikisha kanda nane za Ardhi ambazo ni Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.
Na kwa sasa kamati maalumu ya kukusanya maoni ipo mkoani Tabora ikikusanya maoni ya wananchi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ardhi ili kupata sera iliyoridhiwa na wengi.
Katika sekta ya Ardhi Serikali ya Tanzania imekuwa ikitekeleza Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 kwa takribani miaka 20 hadi sasa, hata hivyo zimejitokeza changamoto nyingi ambazo zinalazimu kufanya mapitio ya sera hiyo.
Migogoro na malalamiko yanayotokana na ardhi ni changamoto zinazo chukua nafasi kubwa katika jamii yetu na imekuwa ikiigharimu kwa kiasi kikubwa katika kuitatua.
Kuongezeka kwa migogoro hii imekuwa ni changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi pamoja na watumiaji mbalimbali wa ardhi hususan wakulima na wafugaji, wawekezaji, wananchi, vijiji na hifadhi.
Hata hivyo, kuongezeka kwa mahitaji ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji hususan katika sekta za kilimo, madini, viwanda na wananchi kutonufaika na uwekezaji unaofanywa katika ardhi na hivyo kusababisha migogoro baina ya wananchi na wawekezaji.
Aidha kutokuwepo kwa mipango ya matumizi endelevu ya ardhi mijini na vijijini na hata sekta ya ardhi kuvamiwa na madalali ni changamoto iliyoifanya Serikali kuamua kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995.
Changamoto zote kwa pamoja, zimelazimika kufanyika kwa mapitio ya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kutoa mwelekeo mpya na usimamizi wa ardhi kwa manufaa ya watanzania wote.
Ardhi ni Sekta mama na hivyo basi Sera ya ardhi ni sera mama katika masuala yote ya maendeleo ikiwemo kilimo na mifugo, ambayo shughuli zake zinafanyika kwenye ardhi.
Na sasa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la ukusanyaji wa maoni na kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kuiboresha. Zoezi hilo limeanza Mwaka huu wa 2016 ambapo linashirikisha kanda nane za Ardhi ambazo ni Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment