mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Wednesday, November 2, 2016

Huduma Ya Kwanza Kwa Mtu Aliyekula Au Kunywa Sumu

Mtu anaweza kula au kulishwa sumu katika mazingira mbalimbali. Kuna watu wengine huamua kujaribu kukatisha maisha yao kwa kunywa sumu kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha. Lakini vyovyote iwavyo katika maisha yako au ya ndugu, jamaa na rafiki kukatisha maisha kwa kula au kunywa sumu sio suluhisho la kukimbia matatizo ya maisha bali ni kuingia kwenye matatizo makubwa mno kwani huko roho itakapokwenda ni MAJUTO MAKUU!

Endapo itatokea mtu amekunywa sumu au amekula chakula chenye sumu muwahishe hospitali au kituo cha afya haraka kama utaona hali hizi: kuwa na kichefuchefu, kutapika au kuharisha, damu kwenye kinyesi, kukosa mkojo, mate kuwa machache mdomoni na yenye mnato au macho kuingia ndani.

Wakati unafanya harakati za kumpeleka kwenye kituo cha afya, mpe tiba mojawapo ya hizi: Pia ukiona sumu sio kali sana maana mara nyingine tunaweza kula chakula lakini baada ya muda fulani tunasikia matumbo yanauma au tunaharisha,

Tumia tiba hizi:
Changanya siki aina ya 'Apple cider vinegar' kijiko cha chai (15ml) kwenye maji ya moto au vuguvugu kiasi cha kikombe kimoja (230ml) kisha mpe anywe. Rudia kila baada ya masaa 2 - 3.
Saga mkaa kisha chukua kiasi cha unga wa mkaa (500mg - 1g) changanya kwenye maji kikombe kimoja (230ml) mpe anywe. Rudia kila baada ya masaa 2- 3.

Kwa tumbo linalouma kutokana na sumu au chakula chenye sumu alichokula mtu anywe chai iliki au peppermint ili kutuliza tumbo. peppermint au iliki ni viungo vya vyakula vinavyopatikana sokoni au suppermarket. Apple cider vinegar ina matumizi mengi sana katika maisha yetu ya kila siku hivyo ni bidhaa muhimu kuwa nayo nyumbani kwako!

Jay Dee Atiwa Hatiani, Atakiwa Amuombe Radhi Ruge wa Clouds FM

Mahakama ya Wilaya Kinondoni imemtia hatiani mwanamuziki nyota wa kike nchini Judith Wambura (Lady Jay Dee) kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.Tokeo la picha la lady jaydee

Mahakama hiyo imemuamuru aombe radhi kupitia kwenye chombo cha habari chenye "coverage" pana nchini kote na ikiwezekana duniani.

Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashtakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga kwa kuuchafua uongozi wa kampuni hiyo na viongozi wake kupitia mitandao ya kijamii katika malumbano makali kati ya pande hizo mbili.

Mei 2013, Clouds Media Group na Ruge walimburuza Jay Dee mahakamani kwa kile walichodai kwamba alikuwa akiwatukana kwenye mitandao ya kijamii.

Bondia Mashali Aliponzwa na Tsh.1000

Rafiki wa karibu wa marehemu Thomas Mashali aliyejitambulisha kwa jina la Ally amesimulia mkasa mzima wa kifo cha rafiki yake huyo.

Tokeo la picha la thomas mashali

Ally alisimulia mkasa wa rafiki yake huyo akiwa msibani maeneo ya Tandale jijini Dar es salaam, ambapo amedai kuwa juzi usiku alipata taarifa za kushambuliwa kwa Mashali na watu wasifahamika maeneo ya Kimara jijini humo.

“Ilikuwa usiku nimekaa nyumbani Manzese Madizini akaja dereva bodaboda anaitwa Yusuf Kidevu akaniambia babaako wanampiga huko Kimara wanamuua kama vipi nenda.”

“Nikahisi ni uongo kwasababu wakati mwingine wanazusha tu, mara kidogo akaja mtu wa pili akasema babaako anakufa huko Kimara, kwasababu alikuwa ni mtu wa pili kuniambia nikaona bora niende.”

“Nikaenda hadi Kimara, kufika pale nikakuta wameshampiga wamemuumiza askari wanampakia kwenye gari. Nikalifata gari hadi Sinza, akapata kitanda akalazwa nikaenda kumsalimia lakini saui ilikuwa inatoka kwa mbali hadi usogeze sikio ndio unaweza kumsikia.”

“Nikamuuliza imekuwaje, akasema kuna dereva bodaboda alimkodi lakini walivyofika Kimara akampa hela kidogo wakaanza kuzozana ndio mkasa ulipoanzia.”

“Alimpa shilingi 2000 lakini dereva bodaboda alikuwa anataka shilingi 3000, akaanza kumtukana Mashali akaona anadharauliwa akampiga ngumi yule dereba bodaboda akaanguka chini, baada ya hapo akaanza kupiga kelele za mwizi wakaja watu wengine watatu wakataka kumpiga akapambana nao akawapiga.”

“Baada ya kuona wote hawamuwezi wote wakaanza kupiga kelele za kumuita mwizi, wakaongezeka watu wengine wakaanza kumshambulia.”

Mwili wa Thomas Mashali unatarajiwa kuzikwa Jumatano jijini Dar es salaam.

Tuesday, November 1, 2016

Magufuli: Huwa Nawasiliana na Rais Kenyatta, Hatuna Bifu Kama Watu Wanavyozani

Baada ya mwaka mzima tangu kuchaguliwa, rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kwanza ya kiserikali nchini Kenya.

Kulikuwepo uvumi kuwa huenda kuna tofauti kali ya rais huyo na mwenzake wa Kenya hasa baada ya rais Magufuli kukosa kuhudhuria mkutano mkuu wa kibiashara ulioandaliwa jijini Nairobi.
Ziara hiyo ya siku mbili inanuiwa kudhihirisha nia safi kati ya Kenya na Tanzania pamoja na kuimarisha biashara.

Mr Blue Asema Hahitaji Meneja Kwenye Muziki Wake

Msanii wa muziki wa kurap, Mr Blue amesema hahitaji kuwa na meneja wa kumsaidia katika kazi zake za muziki kwa kuwa tayari alishawahi kuwa na mameneja zaidi ya watatu ambao hawakumpatia mafanikio.
f1cbmr-Blue-ft-alikiba-mboga-saba

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mboga Sana’ amesema alikuwa hawezi kuishi kwenye tasnia ya muziki bila kuwa na meneja lakini kutokana na kuona mchango wao kwake haukuzaa matunda.

“Mimi nilikuwa siwezi kuendesha maisha yangu ya muziki bila kuwa na meneja na nilifanya kazi chini ya mameneja watatu lakini kwa sasa nimesema basi sihitaji meneja tena nahitaji ushauri wa wadau namna ya kuboresha kazi zangu,” Mr Blue alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.

Rapa huyo pamoja na AliKiba wameshiriki kusapoti ngoma ya Abby Skills inayokwenda kwa jina la Averina , ambapo Abby amewataka mashabiki kumuunga mkono ili arejee vyema kwenye game kama zamani.

Mwaka Mmoja wa Magufuli Kama Rais "Kamwe Huwezi Kuleta Mabadiliko ya Kimsingi Bila ya Kuwa na Kiwango Fulani cha Uwendawazimu"

Ndugu zangu,
Juzi hapa kwenye siku yake ya kuzaliwa, Rais wa Awamu ya Tano, Dr John Pombe Magufuli yumkini aliacha kula keki yake ya kusheherekea siku yake hiyo na kuamua kuwa kazini.
Zikatujia taarifa kubwa mbili; utenguzi wa uteuzi wa DCI na ziara ya kushtukiza wizara ya Maliasili na Utalii.

Nataka niwe mkweli kwa nafsi yangu, kuwa hata kama tungekuwa, kama nchi, na utaratibu wa kuwa na Rais wa kipindi cha mwaka mmoja, basi, huyu tuliye naye sasa, John Pombe Magufuli, angekuwa amemaliza muda wake wa mwaka mmoja akiwa ameacha alama nyuma yake, alama za kudumu muda mrefu.

Ukweli nchi yetu imeanza kubadilika na fikra za watu wake pia zimeanza kubadilika. Maana, ilifika mahali, kuna walioacha kazi kwenye NGO- Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kwenda kufanya kazi Serikalini ikiwamo kwenye Halmashauri zetu wakitamka wazi kuwa kwenye NGO kazi nyingi, wanarudi Serikalini na kwenye Halmashauri kupumzika na kula posho za safari na nyinginezo.
Nchi haiwezi kusonga mbele ikiwa na watu wenye mitazamo kama hiyo. Ni lazima kuwe na nidhamu ya utendaji kazi na kuheshimu sheria, kanuni na taratibu. Na wenye kukiuka hayo, ni lazima wajue kuna adhabu yenye kuendana na matendo yao maovu. Ndiyo siri kubwa ya nchi za wenzetu zilizoendelea.


Nilipata kuandika hapa, kuwa inavyoonekana; Magufuli Ana Uwezo Wa Kumwona Bata Na Sungura Kwa Wakati Mmoja..! ( Novemba 30, 2015)
Hii ni dhana kongwe ya kimtazamo iliyojengeka kifalsafa. Ni uwezo wa mwanadamu katika taswira moja kuwaona viumbe wawili wenye kufanana. Hivyo, inahusu uwezo kuliona jambo hilo hilo katika sura tofauti.

Ndio, kuna kuona kikiwa na kuona kama. Kuliangalia jambo kwa mtazamo tofauti.
Mwanafalsafa Thomas Kuhn yeye anazungumzia dhana ya ' Paradigm Shift'. Ni ile hali ya uwepo wa mapinduzi ya kifikra na ya kisayansi yenye kupelekea mabadiliko ya kimsingi katika jambo lile lile tulilokuwa na mazoea nalo.

Captain Thomas Sankara, kiongozi mwanapinduzi aliyeuawa wa Burkina Faso, katika wakati wake, alizungumzia umuhimu wa kuwa na ujasiri wa kuyapa mgongo mazoea ya kale.
Sankara aliacha hiba njema ya kuenziwa ndani ya nchi yake, Afrika na duniani. Mwanamapinduzi huyu alikuja kuawa kwa kupigwa risasi na wapinga mapinduzi na maendeleo ya Burkina Faso.
Sankara alipata kukaririwa akisema: “Ningependa kuacha nyuma yangu, imani ya kuwa, kama tunaimarisha kiwango fulani cha uangalifu na oganaizesheni, basi, tunastahili ushindi.

Kamwe huwezi kuleta mabadiliko ya kimsingi bila ya kuwa na kiwango fulani cha uwendawazimu. Hali hii inatokana na kutoshinikizwa na taratibu zilizozoeleka, kuwa na ujasiri wa kuzipa mgongo kanuni za kizamani, ujasiri wa kuanzisha mustakabali. Ni wendawazimu wa jana waliotuwezesha kuyafanya tuyafanyao leo. Ninataka kuwa mmoja wa wendawazimu hao.” (Hayati, Kapteni Thomas Sankara)

Yumkini tunachokishuhudia kwenye nchi yetu ni Magufuli's paradigm shift'. Hali ya kuwa na mabadiliko ya msingi.
Na hii ya Magufuli paradigm shift inaweza kuibadili nchi kwa haraka, maana kila mmoja atalazimika kubadilika.
Maggid,
Iringa

‘Makonda’ Feki Awatapeli Wachina Mil 22.8

Dar es Salaam. Raia wa China wametapeliwa fedha taslimu Sh 22.8 milioni wakidai kuwa sauti waliyoisikia kwenye simu ya kiganjani iliyotumiwa na tapeli ilifanana na ya  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema jana ofisini kwake kuwa Oktoba Mosi, mwaka huu mfanyakazi wa Kampuni ya Group Six ambaye  ni raia wa China, Marco Li (24) alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Makonda.

Sirro alisema tapeli huyo alimtaka raia huyo atoe Dola 3,500 za Marekani kwa ajili ya msaada wa kumsomesha mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Manilla kilichopo nchini Ufilipino.

“Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Jensen Hung (39) alikubali ombi la mkuu wa mkoa huyo feki na kumtuma msaidizi wake, Marco Li aende ofisini kwake kwa ajili ya kujiridhisha,” alisema Sirro.