mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Wednesday, November 16, 2016

Calisah Aachiwa Baada ya Kulala Polisi Kwa Tuhuma ya Kusambaza Video ya Utupu ya Wema Sepetu

Mode Calisah ameachiwa jioni hii baada ya siku ya jana kushikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kusambaza mitandaoni video ya utupu ya Wema Sepetu.

Akiongea na Bongo5 jioni kwa njia ya simu wakati akielekea nyumbani kwake, Calisah alisema ni kweli alikamatwa toka jana kutokana na tuhuma za kusamba video hizo mtandaoni.

“Kweli nilikamatwa toka jana lakini nimeachiwa,” alisema Calisah.

Pia model huyo amesema atatoa taarifa zaidi ya nini kinaendelea kuhusu suala hilo.

Babu wa Miaka 89 Ajichimbia Kaburi Canada

"Wajukuu watajua kwamba babu yao alishinda kaburi lake," anasema Bw Kickham

Mzee wa umri wa miaka 89 nchini Canada amegongwa vichwa vya habari nchini humo baada yake kujichimbia kaburi.

Mzee huyo bado yuko buheri wa afya.

"Huwa napenda kuchimba," Jimmy Kickham, kutoka kisiwa cha Prince Edward Island, aliambia CBC News.

Ameongeza kwamba anajivunia kukamilisha mradi huo wake wa kibinafsi.

Bw Kickham, ambaye anamiliki kazi ya ujenzi, amekuwa akichimba makaburi ya wengine pamoja na mitaro kwa zaidi ya miaka 60.

"Siku moja, niliamua kwamba nikifanikiwa kutimiza miaka 90 ningejichimbia kaburi langu."

Bado ana afya nzuri na atatimiza umri wa miaka 90 siku ya Alhamisi.

"Huwa napenda kuchimba. Ni moja ya mambo ambayo yamo kwenye mwili wake. Ni kazi tu. Pesa.

Nilikuwa nachimba kila walichotaka nichimbe, ninaweza," aliambia shirika la utangazaji la Canada.

 Afisa wa makaburi asijiliza Bw Kickham akifafanua ni kwa nini ameamua kuchimba kaburi lake
Bw Kichkam bado huwa anfanya kazi, akitumia trekta alilonunua miaka 45 iliyopita.

"Si jambo la ajabu kwangu kuchimba kaburi, ni kawaida. Nimeyachimba makaburi mengi, Mungu ndiye ajuaye," anasema.

Hata hivyo anaeleza kwamba ilichukua muda kwa familia yake kukubali mpango huo wake.

"Nilienda kwa padri kwanza na kisha kwa msimamizi wa mazishi na kupata vipimo, ingawa tayari nilijua vipimo kutokana na makaburi niliyoyachimba awali," anasema.

Anataka kuzikwa kitamaduni, ambapo sanduku la msonobari huwekwa kaburini mapema kabla ya maziko yenyewe.

Eric Gallant, mfanyakazi katika kanisa la St Alexis, Rollo Bay, anasema hajawahi kushuhuria kisa kama hicho awali.

"Kitu pekee ambacho sasa hakipo ni jeneza tu," anasema.

"Na mimi!" Bw Kickham aliongeza upesi.

Sunday, November 13, 2016

M'marekani ndio mshindi wa Tour of Rwanda

Ruggy Timothy ndiye aliyeshinda raundi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano ya mbio za kimataifa za baiskeli maarufu Tour of Rwanda yaliyoanza mjini Kigali
Image captionRuggy Timothy ndiye aliyeshinda raundi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano ya mbio za kimataifa za baiskeli maarufu Tour of Rwanda yaliyoanza mjini Kigali
Mmarekani Ruggy Timothy ndiye aliyeshinda raundi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano ya mbio za kimataifa za baiskeli maarufu Tour of Rwanda yaliyoanza mjini Kigali.

Msanii wa kizazi kipya anaepeperusha bendera ya Tanzania kwa kupitia songi lake jipya linalokwenda kwa jina la "I'M SORRY MAMA" mwanadada Chemical, amesema yeye ni bikira(hakuwahi kujigi jigi tangu azaliwe).

Chemical ameongea hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha D'WIKEND CHATSHOW kinachorushwa kupitia clouds tv. Chemical ameongeza, licha ya kuwa bikira hajawahi kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja(ulesbian).

Vilevile ameongezea, yeye hana gharama kabisa, kwasababu hatumii mavitu ya gharama kama wadada wa mjini(hapaki miwanja, haweki manywele ya bandia, na makororo mingine ya thamani) ambayo wadada wa mjini wamekuwa wakitumia.

Pichani msanii chemical akiwa na msanii mwezake wa bongo muvi bibie wema sepetu

Kundi la Kigaidi la ISIS Lapiga Marufuku Uvaaji was Chupi na Boxers Kwa Wanaume

Kile kikundi cha kigaidi kijulikanacho na kuogopwa kwa ukatili wa kutisha hili kuleta hofu kimeenda hatua zaidi mbele kwa kuweka sheria kali.

Wahuni hao Wamepiga marufuku uvaaji wa boxer na Chupi kwa wanaume kwasabab ni kimagharibi badala yake unatakiwa uvae bukta ndefu inayovuka magotini ama kitambaa unachojifunga kiunoni kama taulo. Na ukibainika kuvaa hivyo hatua kali itachukuliwa dhidi yako.

Wanajeshi wa Iraq na Kurd walishangaa kukuta mabandiko hayo yanayokataza uvaaji wa Chupi na Boxers walipoukomboa mji wa Hammam Al Allil kusini mwa Mosul dhidi yao.

Pia ISIS imepiga marufuku kunyoa ndevu, kusikiliza mziki na kuvaa jeans zilizobana.

Mbunge Godbless Lema Akipona Katika Hili Abadili Mbinu zake Katika Siasa

Siasa za kutengeneza matukio ya kujiongezea umaarufu zinaanza kumwendea vibaya Lema.

Idadi ya watu waliojitokeza mahakamani katika kesi ya Lema leo imekuwa ndogo sana ukilinganisha na uhamasishaji uliofanyika.

Picha zinazorushwa kutoka maeneo ya mahakama hazioneshi zile "nyomi" tulizozizoea pindi Lema anapopelekwa mahakamani.

Hata wanachama kindakindaki wanaofuatilia kesi hii kwenye mitandao kama Facebook wamekuwa wakimtaja Bananga pekee kama chanzo cha taarifa kutoka mahakamani.

Hata tukio linalopewa umaarufu la mwanamke anayedaiwa kuzimia linaripotiwa kwa picha inayoonesha watu wachache sana wakiwa na mama huyo.

Muda umefika Lema atathmini siasa zake zisije zikampa maumivu makali kuliko matokeo yaliyotarajiwa.

Monday, November 7, 2016

Dogo Janja Kijana Aliyefaulu Kwa Maksi za Juu Somo la Kuanguka na Kuinuka Katika Ubora wa Kiwango cha Juu

Msanii wa hop hop wa Kundi la Weusi, Nikki wa Pili amesema rapa kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja ndiye msanii wake bora 2016. nikki-na-dogo-janja

Rapa huyo amedai Dogo Janja aliwahi kuteleza na kuanguka lakini ameweza kufanikiwa kuinuka katika kiwango cha juu mno huku akiwa na nidhamu ya hali ya juu na kuweza kufuta makosa yake.

“Abdul Kachaa aka Dogo Janja kijana mdogo aliyefaulu kwa maksi za juu somo lililowashinda mamilioni ya watu, wasomi, wafanyabiashara, wanamichezo,” Aliandika Nikki wa Pili Instagram. “Watu wa rika zote somo la kuanguka na kuinuka katika ubora wa kiwango cha juu, nidhamu, kufuta makosa yote,”

Aliongeza, “Show zake sasa zinaacha history, brand yake iko na professional look, confidence iliyovuka mipaka, kwa umri wake na aliyo ya fanya 2016. Namtangaza kuwa msanii wangu bora 2016,”

Dogo Janja ni mmoja kati ya wasanii wa hip hop waliofanya vizuri katika tamasha la fiesta lililofanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.