mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Tuesday, May 31, 2016

Amboni Tanga: Watu 8 Wauawa kwa Kufichua vitendo vya Kihalifu



Watu kadhaa wa kijiji cha Mikocheni karibu na mapango ya Amboni mkoani Tanga wameuawa usiku wa kuamkia leo.

Inasemekana watu waliouawa wanadaiwa kufichua vitendo vya uhalifu kijijini hapo na kwamba miili ya watu hao waliouawa imepelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoani humo.

Chanzo : Radio One.

Mya Take : Ulinzi shirikishi unaweka rehani maisha ya raia wema.

Majambazi Yauwa na Wananchi Baada ya Kumpora Mfanyabiashara Sh Laki Tano


Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa na mwingine mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kujihusisha na ujambazi jijini Dar es Salaam.Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema tukio hilo lilitokea Mei 28 mwaka huu baada ya polisi kupata taarifa kuwa maeneo ya Mburahati kuna majambazi watatu, ambao walikuwa wanafukuzwa na kundi la bodaboda huku wakifyatua risasi.Sirro alisema katika ufuatiliaji askari walifika katika eneo hilo na kukuta jambazi mmoja akishambuliwa na wananchi baada ya silaha aliyokuwa akiitumia kuishiwa risasi.
Jambazi huyo alikutwa na silaha moja, bastola LLA yenye namba 649440. Alisema majambazi wengine wawili, walikimbia wakiwa na bodaboda yenye namba za usajili MC 444 BFY.
Polisi waliwakimbiza wakishirikiana na madereva bodaboda hadi kufika katika eneo la Kisukuru, ambako majambazi hao walianguka na kuangusha bastola yao aina ya Chinese Star, ndipo wananchi walianza kuwashambulia kwa mawe na fimbo.
Aliongeza kuwa majambazi hao, walishambuliwa baada ya muda mfupi walifariki dunia huku mwingine alifanikiwa kukimbia na begi dogo jeusi lililokuwa na fedha.Sirro alisema awali majambazi hao, walikuwa watatu wakiwa kwenye pikipiki maeneo ya Buguruni, ambapo walifanya tukio la uporaji wa Sh 500,000 mali ya Mushi Bakari, aliyekuwa na gari namba T 786 CZI Toyota IST ambaye walimjeruhi mkono wa kulia.

Diamond Platnumz Aonyesha Hadharani Bastola Yake


The CEO of Wasafi Records, Diamond Platnumz, has now joined the list of celebrities who are believed to be walking around with guns.
Well this comes days after he shared a photo on his gram posing with a gun in what looks like a photo studio.
This has left many wondering whether he is a licensed gun holders or he was just posing with it for fun and giggles.

Kilio cha Maisha Magumu: Je, Tulikuwa Tunategemea Vipato Haramu?


Kuna kilio cha maisha magumu kila kona. Utasikia wakina mama,wafanyakazi, vijana hata wazee wanadai kipindi hiki cha awamu ya tano pesa imekuwa ngumu sana!.

Ninajiuliza:
1:Serikali inatueleza Inazuia ufisadi, kubana matumizi yasio ya lazima, matokeo yake wananchi wanalia eti maisha yamekuwa magumu maana yake nini?

2:Makusanyo ya Kodi ya kuwahudumia wananchi yameongezeka sana lkn kilio kila kona, tatizo nini?

3:Je Maisha bora mtaani kipindi kilichopita yalikuwa matokeo ya wizi,ufisadi,matumizi mabaya ya pesa za umma na ukwepaji kodi?

4: Nasikia hotel zinakoswa wateja na taasisi nyingi zinazorota kutokana na kubana matumizi kwa serikali. Najiuliza hivi hawa jamaa walianzisha hizo taasisi/kumbi/hotel walikiwa na market strategy ya kutegemea wateja wawe serikali tu au?

5: je, unadhani nini kinakosekana ili kikiwepo Mafisadi waendelee kutumbuliwa,wakwepa kodi walipe, Gharama za maisha zishuke, Serikali iwe na pesa za kutosha, n.k na maisha ya wananchi yawe saaafi kwa matajiri na maskini kihalali? nini kinakosekana.

Najaribu kuwaza....

Siri Nne za Shilole Kupenda ‘Vitoto’


MSANII nyota wa Muziki wa Kizazi Kipya, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole, baada ya kusemwa kwa muda mrefu, hatimaye amefunguka na kutoa sababu nne za yeye kupenda kutoka na wanaume wanaotajwa kuwa ni wadogo kwake kiumri.

Akizungumza na Ijumaa, nyota huyo ambaye pia hufahamika kama Shishi Baby, alisema maneno ya watu juu ya jambo hilo siyo sahihi, kwani historia ya maisha aliyopitia ndiyo inayomfanya aonekane mkubwa, wakati yeye ni binti mdogo aliyezaa mapema.

Aidha, mkali huyo wa kibao cha Paka la Baa, alisema yeye hivi sasa ana umri wa miaka 30, ‘size’ kabisa kwa wanaume anaotoka nao kimapenzi, kwani hata hao nao, siyo watoto ‘kihiiivyo’ kama maneno ya watu yanavyosema.
Sababu nyingine ni;
.
1: KUOGOPA KUZEESHWA
“Mimi ni kijana kutembea na wazee siwezi, naweza kujikuta nimezeeshwa bure kitu ambacho sikitaki hata kukisikia, kwani naamini bado nina uhitaji kama kijana.
“Angalia wasichana wengi wadogo wanaotoka kimapenzi na wazee hujikuta nao wanakuwa na mambo ya kizee, unadhani atafanya nini wakati ameshakubali kuzeeshwa?”

2: HATAKI KUBURUZWA
“Mimi napenda kuchakarika ndiyo maana sipendi kabisa penzi la wazee ambao ukiwa tegemezi kwao wanakuburuza. Wanawake wengi wanaotoka na wazee huwategemea kwa sababu ya uvivu wao wa kutafuta, kwangu mimi kazi tu!

3: ANASAKA PENZI LA KWELI
“Wasichana wengi wa mjini wamekuwa wakijiingiza kwa wazee lakini hawana mapenzi nao ya kweli, wanakwenda kuchuna pesa kisha wana viserengeti, mimi mwenzao nafuata penzi kwa hao vijana, wanajua kupenda na kwa sababu hobi yangu ni wao siwezi kuwa na wazee kwa kweli.”

4: VIJANA WANA NGUVU, WANAVUTIA
“Na uweke pia hii, kwamba vijana wana nguvu, damu changa na wanavutia, siwezi kutoka na wazee hawana mvuto.”
Baada ya kutaja sababu zake hizo, Shilole alihoji ni yupi mwenye afadhali kati yake na wasichana wenzake wanaotoka na wazee lakini wakiwa wavivu kutafuta?

Baadhi ya Wabunge Wapongeza Wenzao Kusimamishwa


Baadhi ya wabunge wa chama tawala wamepongeza uamuzi wa bunge wa kuwasimamisha wabunge 7 wa upinzani kwa kutofuata sheria za bunge kwa kutaka kushinikiza kujadiliwa kwa hoja ambayo ilikuwa imeshatolewa maamuzi kuhusu bunge kurushwa live.

Baadhi ya wabunge hao ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambaye ameupongeza uamuzi wa Bunge na kusema kwamba ni lazima ifike sehemu adhabu itawale bungeni. Wabunge 7 waliosimamishwa wamepewa kitu wanachostahili kwa kuvunja kanuni.

Mbunge wa Geita vijijini Joseph Kasheku Msukuma amesema kwamba adhabu hiyo ni sawa kwa wabunge hao ili iwe fundisho kwa wabunge wapya.

Kwa upande wake Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga amesema kwamba kusimamishwa huko kutajenga heshima ya Bunge na kuwa fundisho kwa wengine.

Aidha Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu na Ester Bulaya vikao vya mkutano wa tatu na wanne, Godbless Lema, Zitto Kabwe, Paulin Gekul, na Halima Mdee vikao vyote vya mkutano wa tatu na John Heche vikao 10 vya mkutano unaoendelea sasa.

Mwalimu Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumkuwadia Mwanafunzi Wake



Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyaigabo iliyopo Kijiji cha Musati wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara anatuhumiwa kumkuwadia kijana anayemuuzia duka kwa kumpelekea mwanafunzi na kusababisha apate ujauzito.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’hazi alisema mwalimu huyo, Agness Matiko amekamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma hizo.

Ng’hanzi alisema binti huyo mwenye umri wa miaka 16 alimaliza darasa la saba mwaka jana kwenye shule anayofundisha mwalimu huyo.

Alisema mwalimu huyo alikuwa akimtoa darasani mwanafunzi na kumpeleka nyumbani kwake na kumkutanisha na kijana wake huyo kwa ajili ya kufanya naye ngono.

Binti huyo alikuwa anasoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Ikorongo kabla ya kufukuzwa baada ya kubainika kuwa na mimba ya miezi sita.

“Mwaka jana nikiwa darasa la saba mwalimu alinipeleka nyumbani kwake ili nikamsaidie kukamua ng’ombe maziwa, siku ya pili wakati wa mapumziko alinichukua nikamuoshee vyombo tulimkuta huyo kijana baadaye mwalimu alinisihi nibaki naye ndani,” alidai.

Alidai licha ya kukataa kufanya naye ngono, lakini mwalimu alimwambia: “Mimi ni mwalimu wako, kama lingekuwa jambo baya nisingekushauri, hivyo wewe kubali, akatufungia kwa nje. Huyo kijana akanipeleka chumbani kwake akanilaza kitandani na kuniingilia.”

Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo baadaye mwalimu huyo alikwenda kufungua mlango na kumchukua na kumpeleka darasani na huo ukawa mwendelezo wa kumkutanisha na kijana huyo.

Alidai kila mara alimpeleka nyumbani kwake na kuwakutanisha huku akimwambia anataka waoane.

“Baada ya kubainika nina ujauzito walimtorosha huyo kijana na kudai kuwa walimfukuza kwa madai aliwatia hasara dukani,” alidai.

Akizungumza baada ya kupata dhamana, licha ya kukiri kukamatwa kwa tuhuma hizo, mwalimu Matiko alisema hajawahi kumfanyia ukuwadi mwanafunzi huyo.

Alisema kijana aliyekuwa akiishi kwake walimpata kijijini hapa akiwa anatafuta kazi. “Ndipo tulimpatia kazi ya kuuza duka tangu Aprili hadi Oktoba 2015 nilipomfukuza kwa kunisababishia hasara na alisema kwao ni Mabatini mkoani Mwanza,” alisema.

Baba wa binti huyo, Marwa Nchama (53) alisema baada ya kubaini ana mimba alifuatilia na kubaini mwanaye alikuwa akifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na kijana huyo.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Turuka Samwel alikana kulifahamu tukio hilo likiwamo suala la walimu kuwafanyisha kazi wanafunzi majumbani mwao.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Maftah Ally, alisema watumishi wanaohusishwa na tuhuma za kuwapa mimba wanafunzi licha ya kufikishwa mahakamani, watawachukulia hatua za kinidhamu.

Majambazi Yauwa na Wananchi Baada ya Kumpora Mfanyabiashara Sh Laki Tano


Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa na mwingine mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kujihusisha na ujambazi jijini Dar es Salaam.Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema tukio hilo lilitokea Mei 28 mwaka huu baada ya polisi kupata taarifa kuwa maeneo ya Mburahati kuna majambazi watatu, ambao walikuwa wanafukuzwa na kundi la bodaboda huku wakifyatua risasi.Sirro alisema katika ufuatiliaji askari walifika katika eneo hilo na kukuta jambazi mmoja akishambuliwa na wananchi baada ya silaha aliyokuwa akiitumia kuishiwa risasi.
Jambazi huyo alikutwa na silaha moja, bastola LLA yenye namba 649440. Alisema majambazi wengine wawili, walikimbia wakiwa na bodaboda yenye namba za usajili MC 444 BFY.
Polisi waliwakimbiza wakishirikiana na madereva bodaboda hadi kufika katika eneo la Kisukuru, ambako majambazi hao walianguka na kuangusha bastola yao aina ya Chinese Star, ndipo wananchi walianza kuwashambulia kwa mawe na fimbo.
Aliongeza kuwa majambazi hao, walishambuliwa baada ya muda mfupi walifariki dunia huku mwingine alifanikiwa kukimbia na begi dogo jeusi lililokuwa na fedha.Sirro alisema awali majambazi hao, walikuwa watatu wakiwa kwenye pikipiki maeneo ya Buguruni, ambapo walifanya tukio la uporaji wa Sh 500,000 mali ya Mushi Bakari, aliyekuwa na gari namba T 786 CZI Toyota IST ambaye walimjeruhi mkono wa kulia.

Msamaha wa Jakaya Kwa Baadhi ya Watuhumiwa wa Ufisadi wa EPA Waleta Utata


Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete hakutumia ibara ya 45 ya Katiba kutoa msamaha kwa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), wanaoelezwa kuamriwa kurejesha fedha walizochukua.Aidha, alisema pale ambapo kuna makosa, Rais anaweza kumsamehe mtu ambaye tayari amehukumiwa au kupewa adhabu kwa kutumia ibara hiyo.Alisema, “Mimi kwa taarifa nilizonazo Mheshimiwa Rais mstaafu hakutumia kifungu hicho,” Dk Mwakyembe alisema bila kueleza kifungu kilichotumiwa.Alisema hivyo jana bungeni mjini hapa, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF) aliyetaka kujua endapo Rais aliyepita alitumia madaraka yake vibaya, alikosea au alikuwa sahihi kuruhusu baadhi ya watuhumiwa walipe fedha walizodaiwa kuzifanyia ubadhirifu kupitia akaunti ya EPA (Hawakutajwa).Pia, mbunge huyo katika swali lake la pili la nyongeza alitaka kujua ni lini watafikishwa mahakamani akieleza kuwa msamaha waliopewa haukuwa wa kikatiba na kwamba wanastahili kushitakiwa.Katika swali lake la msingi, Haji alitaka kujua iwapo Rais ana mamlaka ya kisheria kutoa msamaha kwa watuhumiwa wa uhalifu wa aina yoyote ambayo mashauri yake yapo katika vyombo vya dola kwenye hatua za uchunguzi, upelelezi au mahakamani.

Msichana wa Kazi za Ndani Afikishwa Mahakani Kwa Kuua Mtoto Mchanga


NAIROBI, KENYA: Msichana wa kazi za ndani mwenye miaka 20 afikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya mtoto mchanga wa miezi nane.

Wolper adai amefilisiwa na Mkongo , amejikuta hana gari wala sehemu ya kulala



Msanii wa filamu, Jacqueline Wolper baada ya kukiri kwamba anatoka kimapenzi na Harmonize, amefunguka na kueleza madai ya kufilisiwa na Mkongo ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani.

Akiongea katika promo ya kipindi kipya cha Take One ambacho kinatarajiwa kuruka Jumanne hii, Wolper amedai yeye ndiye aliyetendwa na Mkongo ambaye alikuwa mpenzi wake, kwani wakati anaanza naye mahusiano alikuwa ana gari na nyumba lakini baadae akijikuta hana hata sehemu yakulala.

Muigizaji huyo ambaye amekuwa akionyesha uwezo mkubwa katika filamu zake, amedai alikuwa anajilipia nyumba kwa dola, lakini ulifikia wakati akafilisika na kuanza kulala hoteli.

Wolper amedai mahusiano hayo yalimsababishia kugombana na baadhi ya watu wake wa karibu ambao walikuwa wakimshauri vizuri, lakini yeye alikuwa akiwaaona kama wanamfitini.

Muigizaji huyo ambaye amewahi kutamba na filamu yake Tom Boy, kwa sasa anatoka kimapenzi na hit maker wa wimbo ‘Bado’, Harmonize kutoka WCB.

Monday, May 30, 2016

PISHI LA LEO WALI WA KAROTI


MAPISHI YA WALI WA KAROTI

Mahitaji

Kitunguu maji
karoti
siagi( Butter) inasaidia kuweka harufu nzuri katika chakula chako




Huo ni muonekano halisi wa kitunguu kilichokatwa na karoti iliyokwaruzwa


Weka siagi yako katika sufuria kisha weka vitunguu kaanga kidogo





Kisha weka karoti pia kaanga ziiive kiasi 




Huu ndio muonekano wa karoti imeshaiva





Kisha weka wali wako ndani ya mchanganyiko wa wali uliokwisha iva



Hakikisha unachanganya safi kabisa mapaka karoti na wali vinachanganyika safi




Kisha tengeneza shape nzuri ya wali na weka katika sahani



Wali huu unaweza kula na mboga yeyote ile na utakua umewashangaza wageni kwa ubora na ladha ya chakula ulichowaandalia furahia weekend na familia yako hujachelewa.

Mbunge Amtaja Kikwete Sakata la EPA


Mbunge wa Konde Khatibu Said Haji (Cuf), jana aliibua sakata la Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) bungeni akimtaja Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kwamba alikiuka Katiba kwa kutoa msamaha kwa watu waliotuhumiwa. Hata hivyo, Serikali kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria Dk Harrion Mwakyembe ilikanusha madai hayo na kusema Rais alikuwa sahihi kwa kuwa viko vifungu ambavyo vinampa nafasi...

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI MBALI MBALI LINDI VIJIJINI


 Mwenge wa Uhuru ukiwasili kwenye uwanja wa mpira wa Mchinga I,wilaya ya Lindi vijijini ambapo ulizindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika Majimbo mawili wa wilaya hiyo, jimbo la Mchinga na jimbo la Mtama.
 Viongozi mbali mbali wakiwa wamesimama tayari kuupokea Mwenge wa Uhuru katika wilaya ya Lindi Vijijini
 Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Bw. George Jackson kitaifa akizindua mradi wa maji katika shule ya msingi Mchinga I.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda wakiwaongoza waongoza Mwenge wa Uhuru kitaifa kupita juu ya daraja lililofunguliwa rasmi na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Daraja hili linawaunganisha wakazi wa Mchinga II na Mchinga I.
 Wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata ya Mnonela wakihushuhudia Mwenge wa Uhuru kwa kuushika ulipowasili shuleni hapo jimbo la Mtama , Lindi Vijijini.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) , mkimbiza Mwenge Kitaifa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda wakiwa wamekalia moja ya madawati 50 yaliokabidhiwa kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi  Mnolela.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa heshima kwa Mwenge wa Uhuru kwenye viwanja vya shule ya msingi Madangwa.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Madangwa waliojitokeza kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru ambapo aliwaambia kuwa utekelezaji wa yale aliyoahidi umeanza na kuwahakikishia wananchi wa jimbo lake ahadi zake zitakamilika mapema zaidi.

Tamko la ACT Wazalendo Baada ya Wabunge wa Upinzani Kufungiwa


Baada ya Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge ambapo wabunge Easther Bulaya na Tundu Lissu wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano  wa nne.

Wabunge Pauline Geku, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema wamepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatohudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu. Makosa hayo waliyafanya mkutano wa pili mwezi January.

Baada ya adhabu hiyo kwa wabunge, ACT Wazalendo wametoa tamko lao ambapo wameyazungumza haya……

’Chama cha  ACT Wazalendo kimesikitishwa na kitendo cha ugandamizaji wa demokrasia kilichofanywa na wabunge wa CCM kwa kuwasimamisha ubunge wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama chetu  Zitto Kabwe’

’Katikati ya masikitiko hayo tunafarijika kuona wabunge hao wameondolewa kwa sababu ya misimamo yao ya kutetea maslahi ya wananchi’

’Tungesikitishwa zaidi kama mashujaa wetu hawa wangeondolewa bungeni kwa sababu ya ulevi au wawe sehemu ya wagonga mihuri ya masuala ya hovyo hovyo yanayosimamiwa na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM)’

’Kwa sababu hiyo ya kusimamia maslahi ya wananchi sisi kwetu ni mashujaa na kwa maana hiyo Chama chetu kinaandaa maandamano makubwa jijini Dar Es Salaam kuwapokea mashujaa wa wananchi’

Mke wa Trafiki Kinyogori Adaiwa Kukiri Kumuua Mumewe


MKE wa askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani (trafiki), Sajenti Ally Salum (Kinyogori) aliyeuawa hivi karibuni, inadaiwa amekiri kuhusika kwenye mauaji hayo, akidai ilitokana na mumewe kumuacha na kuoa mke mwingine.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mauaji hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Kinyogori, Mkuranga mkoani Pwani.

Wakati huo huo, Kamanda Sirro amezungumzia pia mauaji ya Anathe Msuya yaliyofanyika hivi karibuni Kigamboni na kusema polisi inaendelea kumtafuta msichana wa kazi za nyumbani aliyetoroka siku moja kabla ya kifo cha mwanamke huyo.

Anayetuhumiwa kuua mumewe
Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyojitokeza jijini Dar es Salaam, Sirro alisema katika mahojiano ya awali mke wa Kinyogori amekiri kuhusika.

Kwa mujibu wa kamanda, mwanamke huyo ambaye hata hivyo hakutaja jina lake kwa sababu za kipelelezi, aliamua kumtuma mtu kutekeleza mauaji hayo baada ya mumewe kumwacha na kuoa mke mwingine.

“Ni jambo la kusikitisha kuona mtu anatoa uhai wa mtu sababu ya kuachwa. Tunawasihi wananchi kuepuka kujihusisha na matukio kama haya, eti sababu tu ya kuachwa wanawake wapo wengi na wanaume wapo wengi unaweza kuachwa na ukaolewa na ukaoa kuliko kuondoa uhai wa mtu,” alisisitiza Sirro.

Hata hivyo, Sirro alisema wanaendelea kuwahoji watuhumiwa hao ili waweze kuwataja watu wengine walioshirikiana nao kutekeleza tukio hilo baada ya kuonekana kuwepo kwa wahusika wengine.

‘Hausigeli’ asakwa
Kuhusu mauaji ya Anathe aliyechinjwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, Kamanda Sirro alisema wanaendelea na jitihada za kumtafuta msichana huyo ahojiwe kuhusu tukio hilo.

Aidha alisema mtu mmoja anashikiliwa akituhumiwa kuhusika na tukio hilo huku polisi ikiwa imeandaa timu ya upelelezi itakayoshughulikia tukio hilo kufanikisha kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo.

Sirro alisema msichana huyo aliondoka siku moja kabla ya tukio hilo la mauaji hivyo kupatikana kwake, kunaweza kusaidia polisi kujua kama kuondoka kwake kulikuwa salama au kuna kitu kimejificha.

“Msichana huyu tunaendelea kumsaka tujue kama aliondoka salama na kumhoji zaidi juu ya kuondoka kwake siku moja tu, tukio linatokea nina imani tutafanikiwa kumpata na wote waliohusika na kukomesha matukio haya,” alisema Sirro.

Mamia wajitokeza msibani
Vilio na simanzi jana vilitawala wakati mamia ya wakazi wa Kibada Kigamboni na Salasala walipokuwa wakiuaga mwili wa marehemu Anathe Msuya (30), aliyeuawa Mei 25 nyumbani kwake kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana.

Mwili ulichukuliwa jana asubuhi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na kupelekwa nyumbani kwake Kibada, kwa ajili ya kuagwa na majirani zake kabla ya kusafirishwa kwenda kuzikwa mkoani Arusha leo.

Akizungumza baada ya mamia kumuaga nyumbani kwa marehemu, mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyakwale Kibada, Said Pazi alisema kuwa wao kama majirani waliomba familia wapate fursa ya kumuaga jirani yao ambaye tangu ahamie ana muda wa miezi sita.

“Baada ya kuambiwa msiba upo Salasala tuliomba kama majirani na sisi tupatiwe fursa ya kuuaga mwili wa ndugu yetu ambaye alihamia mwaka jana… kwa kweli msiba wake umetusikitisha sana” alisema.

Akizungumzia tukio hilo alisema kuwa mtoto wa marehemu huyo, Allan Kimario (4) aliwataarifu majirani kuwa mama yake haamki na ndipo walipofika wakakuta ameuawa.

Mwenyekiti huyo alitoa pole na kusema atahakikisha wanaimarisha ulinzi na kuhimiza wenye viwanja ambavyo havijajengwa, wavifanyie usafi ili kuondoa vichaka ambavyo ni hatari kwa usalama.

Maalim Sief Matatani Tena, Atakiwa Kurepoti Polisin Kwa Mahojiano


Baada ya Jeshi la Polisi Zanzibar kuahirisha kumhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, hatimaye hatua hiyo sasa imeelekea kutekelezwa.

Taarifa rasmi ya jeshi hilo visiwani Zanzibar, imemtaka Maalim Seif afike katika Ofisi za Makao Makuu ya Polisi, Ziwani mjini hapa leo saa 4.00 asubuhi.

Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano kwa Umma wa CUF, Salim Bimani alithibitisha Maalim Seif kupokea barua hiyo jana wakati akiwa njiani kuelekea Dunga, Wilaya ya Kati Unguja, akiendelea na ziara yake katika majimbo ya Unguja.

“Ni kweli Maalim amepokea taarifa hiyo na ametakiwa afike Ziwani (mjini hapa) kesho (leo) saa nne asubuhi,” alisema Bimani

Bimani aliongeza kuwa hatua hiyo ya sasa imekuja baada ya jeshi hilo kuahirisha hatua ya wito wa kumhoji Maalim Seif, Ijumaa iliyopita.

Barua hiyo ya kuahirisha iliyosainiwa  na Msangi kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Mei 26, yenye kumbukumbu namba PHQ/ Z/C.5/4/4/TEMP/34 kwenda kwa Maalim Seif ilikuwa na kichwa cha habari ‘Kuahirisha mahojiano’.

“Tafadhali rejea barua yangu PHQ/Z/C.5/4/4/TEMP 26 ya tarehe 22/5/2016 ambapo tulikuita hapa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwa mahojiano maalumu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na Ulinzi na Usalama wa Visiwa hivi,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo ya Msangi.

Kadhalika, barua hiyo ya kuahirisha mahojiano hayo ilisema:

“Tutakujulisha mapema siku ile iliyosainiwa na DCP Salum ya mahojiano itakayofuata mara baada ya kukamilisha taratibu.”

Msangi alithibitisha wito huo wa leo baada ya hatua ya awali, kumtaka kiongozi huyo awasili mbele yao kwa mahojiano kama ambavyo walimuahidi awali.

Sunday, May 29, 2016

MAMBO MATATU YANAYOIPA NGUVU LEBO YA WASAFI KUFIKA MBALI

12545433_984510021656162_873669931_n
Mpaka sasa lebo ya WCB inawamiliki wasanii wanne akiwemo Diamond, Harmonize, Raymond na Q Boy Msafi huku kukiwa na taarifa za chini chini kuwa tayari Rich Mavoko ameshamwaga wino wa kuwa chini ya lebo hiyo huku bajeti yake ikiwa tayari imeshawekwa pembeni na tayari amesharekodi wimbo pamoja na video iliyofanyika huko Afrika Kusini. Lakini pia nje ya kutafuta vipaji kwenye hili analolifanya Diamond ni biashara kubwa ambayo itafanya akaunti zake za benki kujaa kila siku.
Hiki ndicho kitaweza kuipaisha lebo ya WCB kuwa kubwa zaidi.
Ukubwa wa jina la Diamond
Hili halina ubishi kwa sasa Diamond amekuwa ni miongoni mwa wasanii wenye majina makubwa kwenye tasnia ya muziki kwa Afrika kwa sasa. Hicho ni kitu ambacho kimemfanya kujitengenezea fan base kubwa kutokana na kazi zake anazofanya, lakini pia ana uwezo wa kuwatengenezea connection wasanii wa lebo yake [WCB] kufanya kazi na msanii yeyote wa Afrika endapo muda utaruhusu kutokana na jina lake huku yeye mwenyewe akizidi kujitafutia connection za Marekani na Ulaya kama walivyoanza kwa Harmonize kufanya kazi na Korede Bello kutoka Mavin Records lakini pia Harmonize aliwahi kusema ana kazi na Kiss Daniel wa Nigeria.
Mashabiki wanaomsupport Diamond
Diamond ni msanii mwenye washabiki wengi wanaomsupport ambao wapo tayari kupambana na lolote endapo wataona msanii wao anaandamwa na na maneno kutoka upande mwingine. Kutokana na hilo uongozi wa WCB unaweza kutumia pointi hiyo kuifanya lebo yao kuwa juu zaidi kama wanavyofanya sasa kwa Harmonize na Raymond kutembelea nyota ya Dangote.
Menejimenti ya WCB
Uongozi wa WCB ukiongozwa na Salaam pamoja na Babu Tale umefanikiwa kufaulu kwenye suala la mipango na kujiamini kwenye kila wanalolifanya na hawashindwi kujaribu. Kutokana na uwezo wao walionao wanaweza wakaifanya lebo ya WCB kufika mbali zaidi lakini itachukua muda mpaka kufika huko.

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA NIDA, ATOA HABARI NJEMA KWA WATUMISHI 597 WALIOSITISHWA MIKATABA YAO

1Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) akimsalimia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba, wakati alipokuwa anawasili katika ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi.
2Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo katika Jengo la BMTL, jijini Dar es Salaam, jana. Katika hotuba yake, Rwegasira aliwataka watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao waondoe hofu kwani hivi karibuni Serikali itaanza kuwalipa fedha zao baada ya taratibu chache za kiutendaji kukamilika.
3Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Ansigar Chilemba akitoa maelezo jinsi taarifa za muombaji wa Kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa, kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
4Afisa Usajili Kitengo cha Ubora wa Kadi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Jemima Mulokozi (kushoto) akimuonyesha vitambulisho vilivyokamilika vikiwa na ubora unaohitajika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
5Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa tano kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba (wa tano kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka hiyo, mara baada ya Katibu Mkuu kumaliza ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………………………..
Na Felix Mwagara, MOHA
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema fedha za kuwalipa watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zipo na watalipwa hivi karibuni.
Rwegasira alisema kiasi cha shilingi bilioni 2.3 zimetengwa kwa ajili ya malipo ya Watumishi hao waliachishwa kazi Machi 7, 2016 ambapo wanaidai Mamlaka mishahara ya miezi mitatu nyuma, malimbikizo ya fedha katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na makato ya fedha za Bima ya Afya.
Akuzungumza na watumishi wa Makao Makuu ya NIDA pamoja na Maafisa Wasajili wa Vitambulisho vya Taifa, jijini Dar es Salaam jana, Rwegasira aliwataka watumishi hao waliositishiwa mikataba yao, wasipotoshwe na mtu yeyote kuhusu kutokulipwa haki zao kwani wapo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha taratibu ndogo ndogo  kabla ya kuanza kuwalipa.
“Naomba muwaambie waondoe wasiwasi wowote, waache maneno, watulie kwani Serikali ipo makini na fedha tunazo na tutaanza kuwalipa mara tumalizapo taratibu ndogo ndogo zilizobaki.” Alisema Rwegasira.
Aidha, Rwegasira aliwataka watumishi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha ifikapo Desemba 31 mwaka huu Watanzania Milioni 23 wanatakiwa watambuliwe na kupata namba kabla ya kuanza kupewa Vitambulisho vya Taifa.
Hata hivyo, watumishi hao walimuakikishia Katibu Mkuu huyo, kuwa kazi hiyo ya utambuzi  itakamilika kama ilivyopangwa na itafanyika kwa umakini mkubwa kama inavyotarajiwa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kuwatembelea na kuwatia hamasa katika kukamilisha kazi pamoja na kufikisha lengo lao la kukamilisha utambuzi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
“Tunakuahidi Katibu Mkuu kuwa tutatimiza lengo letu na tunakuakikishia tutafanya kazi kadiri ya uwezo wetu tukiongozwa na kauli mbiu ya ‘hapa kazi tu’, alisema Dk. Kipilimba
Katibu Mkuu Rwegasira alifanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza zaidi shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka, hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji.