mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Friday, October 28, 2016

Afisa aliyemtisha mwandishi wa habari aomba msamaha Kenya


Dola milioni 50 zimetoweka kutoka wizara ya afyaImage copyrightAFP
Image captionDola milioni 50 zimetoweka kutoka wizara ya afya
Afisa wa serikali ambaye ni katibu katika wizara ya afya Nicholas Muraguri, ameomba msamaha kwa kumtisha mwandishi wa habari ambaye alikuwa akichunguza ufisadi kwenye serikali.
Siku ya Jumatano gazeti la Business Daily lilifichua kuwa dola milioni 50 zimetoweka kutoka kwa bajeti ya wizara ya afya.
Kwa mfano dola milioni 7.9 ambazo zilistahili kununua zahanati za afya za kuhama hama hazijulikani ziliko.
Akijibu, bwana Muraguri alimwambia mwandishi huyo wa habari kuwa serikali ina majasusi katika kampuni ya Nation, ambayo huchapisha gazeti la Business Daily.
"Hauielewi serikali, tunaweza kukipata unachokiandika hata kabla hujakichapisha, ikiwemo kupata picha za taarifa. Kama kuna haja ya kudukua mtadao wa Nation tunaweza kufanya hivyo. Tunaweza hata kukuambia ni pesa ngapi ziko kwa akaunti yako."
Kisha afisa huyo akakumbwa na lawama kwa matamshi yake hatua iliyosababisha yeye aombe msamaha.
"Matamshi yangu ni ya kusikitisha na kujutia na hayaonyeshi msimamo wangu kama mfanyikazi wa serikali."

No comments:

Post a Comment