Clinton: Sitojali atakachosema Trump
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Democrat nchini Marekani Hillary Clinton amesema kuwa hatojali tena kile kitakachosemwa na mpinzani wake Donald Trump na badala yake ameamua kuangazia sera zake katika kampeni.
''Tulijadiliana naye kwa saa nne na nusu'',alisema akikumbuka mjadala wao wa wiki iliopita.
''Sifikirii tena kurushiana naye maneno''.alikuwa akizungumza katika ndege yake ya kampeni.
Bwana Trump alitumia mkutano wake huko Gettysburg kuahidi biashara mpya pamoja mazungumzo kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.
Ikiwa imesalia siku 16 hadi uchaguzi,mambo mengi yameangazia utata wake unaohusishwa na kampeni yake.
Siku ya Jumamosi ,aliahidi kuwashtaki wanawake wote waliomtuhumu kuwanyanyasa kingono wakati atakapokamilisha kampeni yake ya urais.
Huku akiwa yuko nyuma ya Clinton kwa umaarufu alipunguza pengo hilo kwa asilimia 4
No comments:
Post a Comment