UN yataka muda wa amani kuongezwa Yemen
Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa pande zinazozozana nchini Yemen kuongeza muda wa usitishwaji mapigano kwa siku tatu zaidi.
Mjumbe maalum, Ismail Ould Cheikh Ahmed, amesema muafaka wa awali wa kusitisha mapigano ulikuwa wa kutoa fursa kwa Umoja wa Mataifa kutoa misaada ya chakula na huduma za dharura katika maeneo ambayo hayakuweza kufikiwa.
Amesema mapigano yamesitishwa tofauti na ripoti kwamba makubaliano hayo yamekiukwa na pande zote mbili.
Serikali ya Yemeni kwa ushirikiano na vikosi vinavyoongozwa na Saudia,imekuwa ikipigana na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran, tangu mwaka 2014 katika juhudi za kuthibiti taifa hilo.
No comments:
Post a Comment