Wanajeshi wa Ethiopia waondoka Somalia
Wanajeshi wa Ethiopia wanaopigana na wapiganaji wa al-shabab nchini Somalia wameondoka katika kambi kubwa ya kijeshi huko Halgan katikatiki mwa jimbo la Hiran.
Walioshuhudia wanasema kuwa wapiganaji hao wa Jihad walichuka eneo hilo muda tu baada ya wanajeshi hao kuondoka.
Mamia ya watu wameanza kulitoroka eneo hilo wakihofia mashambulio ya kundi hilo.
Hii ni mara ya tatu mwezi huu ambapo wanajeshi wa Ethiopia wameondoka katika kambi muhimu nchini Somalia.
Imedaiwa kuwa huenda wanajeshi hao watahitajika kukabiliana na maandamano yanayoendelea nchini mwao.
No comments:
Post a Comment