Jinsi mtoto kutoka Ghana alipata umaarufu mitandaoni
Mtoto mmoja wa kiume ambaye picha yake ilipata umaarufu kwenye mitandao huenda ikasababisha kijiji kizima kupata elimu.
Jake amekuwa mmoja wa wanafunzi maarufu zaidfi nchini Afrika Kusini tangua watu waanze kusambaza picha yake huku wakiifanyia utani picha hiyo
Hata hivyo Jake anaishi umbali wa kilomita kadha kaskazini, katika kijiji kimoja kilicho mashariki mwa Ghana bila ya kufahamu umaarufu alioupata.
Ukweli ni kwamba hadi siku ya Jumatano hata mtu ambaye aliipiga picha hiyo hakuwa na habari kuwa imepata umaarufu.
Mpiga picha Carlos Cortes alisafiri kwenda nchini Ghana mwaka 2015 na kufanya makala kuhusu Solomon Adufah, ambaye ni msanii aliyekuwa akirejea nyumbani kutoka Marekani.
Picha ya Jake ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka minne, ni kati ya mamia ya picha zilizopigwa wakaati Adufah alikuwa akiwafunza watoto sanaa.
Lakini picha hiyo ya Jade ilianza kusambaa mitandaoni baada ya Adufah kuituma kwa akaunti yake ya mtandao wa Instagram.
Wakati aligundua kuwa picha hiyo imeanza kupata umaarufu hakujua cha kufanya.
Hapo ndipo sasa Adufah ambaye ameishi Marekani tangu umri wa miaka 16 alianzisha mchango akiwa na matumaini kuwa Jake atasababisha watu kudhamini elimu yake na ya watoto wengine kijijini.
Ndani ya saa 24 kampeni hiyo ilichangisha dola 2000. Adufa anasema kwa pesa hizo zitatatumiwa kuleta mabadiliko makubwa kwa watoto wa eneo hilo
No comments:
Post a Comment