mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Saturday, October 22, 2016

Moshi wa sumu umezuka karibu na kambi ya jeshi Mosul


Moshi kutoka kinu cha kemikali ya SulphurImage copyrightREUTERS
Wanajeshi wa Marekani katika kambi ya jeshi karibu na mji uliopo kaskazini Iraq, Mosul wamejifunika nyuso zao kujikinga dhidi ya msohi wa sumu kutoka kinu cha kemikali ya Sulphur ilichotektezwa moto katika mapigano na kundi la Islamic State.
Walichukua tahadhari hiyo baada ya upepo kuusukuma moshi kutoka kwenye moto kuelekea kwenye kambi ya jeshi la anga ya Qayyarah.
Mjini Baghdad, jitihada za Uturuki kujiunga na mashambulio dhidi ya Islamic State hazikufua dafu.
Wakati huo huo, vikosi vinavyosogea vya Iraq vimeingia mji wa Qaraqosh, kilomita 32 kusini mwa Mosul, mji mkuu unaodhibitiwa na IS.
Qaraqosh, ambao ndio mji wa Iraq ulio na idadi kubwa ya waumini wa kikristo kabla ya vita unaarifiwa kuwa mtupu, hauna watu lakini wapiganaji wa IS wametega mabomu ya ardhini katika njia za kuelekea mji wa Mosul.
Wanamgambo hao wamekuwa wakitekeleza mashambulio ya kujitoa muhanga katika maeneo mengine, wakiendesha magari kwa kasi kubwa yaliohamiwa kwa milipuko yakivurumizwa katika maene yanayodhibitiwa na vikosi vya serikali.

No comments:

Post a Comment