Rooney akiri mambo ni magumu
Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney, amekiri kuwa sasa anakabiliwa na changamoto mpya katika Maisha yake ya Soka lakini amesisitiza bado hajaishiwa na ustadi wa kucheza.
Rooney ambaye Jumatatu atatimiza miaka 31, alitoa kauli hiyo alipoongea na Waandishi wa habari siku chache baada ya Man United kutoka sare tasa 0-0 na Liverpool Jumatatu iliyopita huko Anfield huku yeye akianzia Benchi.
Rooney ameuelezea mchezo dhidi ya Liverpool kuwa ilikuwa muhimu wasifungwe hasa kwa vile wanakabiliwa na mechi ngumu zijazo dhidi ya Fenerbahce Alhamisi jioni , Chelsea na Manchester City.
Rooney, ambaye kwa sasa akiwa na Man United amechezea mechi 4 akitokea benchi, amesisitiza kuwa yeye yupo tayari wakati wowote akiitwa kucheza.
No comments:
Post a Comment