mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Thursday, October 20, 2016

Uefa: Barcelona yaiua Manchester City ya kocha wake wa zamani


Messi amefunga magoli 10 katika michezo nane ya mwisho ya ligi ya mabingwa Ulaya
Image captionMessi amefunga magoli 10 katika michezo nane ya mwisho ya ligi ya mabingwa Ulaya
Michuano ya klabu bingwa ulaya imeendelea kwa michezo nane kupigwa ambapo Arsenal waliiadhibu Ludogorets Razgrad ya Bulgaria 6-0, wakati Mesut Ozil akipata hat trick.
Barcelona nayo wakiwa nyumbani walimdhalilisha kocha wao wa zamani Pep Guardiola kwa kumpa kichapo cha 4-0, Messi nae akipiga hat-trick, ambapo katika mchezo huo ilishuhudiwa mlinzi wa Man city Claudio Bravo akilambwa kadi nyekundu huku pia mlinzi wa Barcelona aliyeingia akitokea benchi Jeremy Mathieu naye akizawadiwa kadi nyekundu.
Bravo atakosa mchezo wa maruduiano Novemba 1
Image captionBravo atakosa mchezo wa maruduiano Novemba 1
Makosa ya wazi ya mlinzi wa Celtic Kolo Toure yakaipa Borussia Monchengladbach ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini, magoli yakifungwa na Lars Stindl pamoja na Andre Hahn.
Wachezaji wa Arsenal wakifurahia ushindi mnono
Image captionWachezaji wa Arsenal wakifurahia ushindi mnono

Matokeo ya michezo mingine

Bayern Munich 4-1 PSV Eindhoven
Paris Saint-Germain 3-0 Basel
Dynamo Kiev 0-2 Benfica
Napoli 2-3 Besiktas
FC Rostov 0-1 Atlético Madrid

No comments:

Post a Comment