Mashambulio yatakelezwa mjini Aleppo
Mashambilizi makali ya angani yamerejelewa katika mji wa Aleppo baada ya muda wa siku tatu wa usitishwaji mapigano uliokuwa umetangazwa na Urusi kukamilika.
Mashambulio ya angani yameripotiwa katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na yale yanayokaribiana na maeneo ya Sheikh Saeed na Salah el-Deen.
Maeneo mengine yanayoshikiliwa na waasi pia yanalengwa katika mashambulio hayo japo haijabainika iwapo yanatekelezwa na ndege za Urusi au Syria.
Umoja wa Mataifa umesema haukufanikiwa kumuondoa mtu yeyote katika maeneo yanayothibitiwa na waasi ambayo yamezingirwa wakati wa kipindi cha usitishwaji mapigano kwa sababu maafisa wake hawakuhakikishiwa usalama wa kuendeleza shughuli hiyo
No comments:
Post a Comment