Dulla Mbabe kupigana na Mchina Dar
Bondia wa Tanzania Dulla Mbabe tarehe 28 Oktoba anatarajia kupambana na Bondia Chengbo Zheng kutoka Taifa la China Pambano la WBO katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa mwandaaji wa pambano hilo Jay Msangi, mshindi wa pambano hilo atajinyakulia Mkanda wa ubingwa, huku pia kukiwa na mapambano mengine mengi ya utangulizi ambayo yatawakutanisha mabondia kutoka Tanzania na nje ya Tanzania.
Jay Msangi amesema kwa sasa wataandaa mapambano mengi ya kimataifa kwa mabondia wa Tanzania kwa lengo la kuwandaa kufuzu mashindano ya Olimpiki nchini Japan.
No comments:
Post a Comment