Syria inashutumiwa kwa shambulio la silaha za kemikali 2015
Vikosi vya serikali ya Syria vimetekeleza shambulio la tatu la silaha za kemikali mwaka jana, ripoti ya siri ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa imefichua.
Ripoti hiyo iliyofichuliwa inasema helikopta ziliangusha mabomu yalio na gesi ya chlorine, silaha iliyopigwa marufuku, katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Idlip mnamo Mchi 2015.
Ripoti ya awali ya shirika linalopiga marufuku matumizi ya silaha za kemikali (OPCW) imeishutumu serikali ya Syria kwa mashambulio mengine mawili ya gesi mwaka jana.
Serikali haijatoa tamko.
Syria imekubali kuharibu silaha zake za kemikali mnamo 2013 chini ya makubaliano yaliojadiliwa kati ya Moscow na Washington.
Baraza la usalama liliunga mkono makubaliano hayo kwa azimio kuwa iwapo Syria haitotii, huenda ikakabiliwa na vikwazo au hatua za kijeshi chini ya sheria za Umoja huo.
Matokeo ya hivi karibuni- ambayo ni ripoti ya nne kutoka uchunguzi wa miezi 13 wa Umoja wa mataifa na OPCW - umeshutumu vikosi vya serikali kwa kutekeleza mashambulio ya gesi ya sumu huko Qmenas, katika jimbo la Idlib mnamo Machi 16 2015.
Maokeo yalisababisha kuzuka tofuati kati a matiafa matano yenye kura ya turufu katika baraza la usalama la Umoja wa matiafa waandishi wanasema - Huku Urusi na China zikiipinga Marekani, Uingereza na Ufaransa.
Ripoti ya tatu ya OPCW iliowasilishwa Agosti, ililishutumu kundi la Islamic State kwa kutumia silaha zlizo na kemikali aina ya sulphur.
Wakati huo, Urusi ililalamika kuwa matokeo hayo dhidi yake na serikali hayapaswi kutumiwa kama kigezo cha kuidhinisha vikwazo vya Umoja wa mataifa.
Ni marufuku kutumia silaha za Chlorine chini ya sheria ya mwaka 1997 ya silaha za kemikali ambayo Syria ilijunga kuwa mwanachama mnamo mwaka 2013
No comments:
Post a Comment