mazingira

mazingira
kwa pamoja tuyatunze mazingira

Wednesday, October 19, 2016

Kenya yampata jaji mkuu mpya, David Maraga

  • Saa 5 zilizopita
Jaji Mkuu David MaragaImage coK
Image captionJaji Mkuu David Maraga akila kiapo
Jaji David Maraga ameapishwa kuwa Jaji Mkuu mpya wa Kenya baada ya kustaafu kwa jaji mkuu wa awali Dkt Willy Mutunga.
Jaji Maraga atakuwa jaji wa pili kuhudumu nchini Kenya tangu kuanza kutekelezwa kwa katiba ya sasa nchini Kenya, ambayo ilifanyia mabadiliko mfumo wa mahakama, mwaka 2010.
Ameapishwa baada ya kuidhinishwa na bunge siku ya Jumanne.
Moja ya shughuli muhimu anazotarajiwa kutekeleza ni kuwaapisha wanachama wa jopo la kuteua makamishna wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Kenya inapoendelea kujiandaa kwa uchaguzi mkuu Agosti mwaka ujao.
Kama jaji mkuu, atakuwa pia Rais wa Mahakama ya Juu ambayo husikiliza na kutoa uamuzi kuhusu kesi za matokeo ya uchaguzi wa urais.
Jaji Maraga anatazamwa na wengi kama mhafidhina.

No comments:

Post a Comment